Sema chochote kwa Baba yako, leo Father's Day

Sema chochote kwa Baba yako, leo Father's Day

Ramea

JF-Expert Member
Joined
Mar 19, 2015
Posts
2,146
Reaction score
4,093
Kama ilivyo siku ya akina Mama/ Wanawake duniani March 8, leo June 21 ni siku ya akina Baba japo husahauliwa sana kwenye Media.

Tuseme maneno mazuri kwa mzazi huyu huyu wa kiume hata kama alishatangulia mbele za Haki.

2434237_Screenshot_20200621-090155.jpg
 
Nilipofaulu darasa la saba kwenda sekondari kuna wapuuzi walimwambia baba asinipeleke shule kwakuwa mimi ni wa kike.

Mzee aliwajibu siwezi kumdhulumu mtoto haki yake ya elimu eti kwakuwa ni wa kike atasoma mpaka atakapochoka mwenyewe.

Pumzika kwa amani baba yangu.
 
Happy father's day to my lovely dad. Upendo wake wa dhati na moyo wa huruma vimenifundisha mengi na kunijenga vema.
Hakusoma sana enzi zake ila amehakikisha watoto wake anatupa elimu bora.

Napenda jinsi alivyotulea na kutufanya kama rafiki zake, he is the coolest dad ever😍 Mungu azidi kumpa afya njema huyu mzee, nampenda sana.
 
Wangu mimi alikuwa kama jogoo wa kuku wa kienyeji. Akishatia mimba anasepa hakuna hata matunzo kwa hao waliikwa wake zake. Pia hakuwa na mpango wa matunzo kwa watoto wala matibabu wala elimu.

Pia hata wakati anakula mtoto ukisogea karibu atakuchapa kwa kigezo kuwa siyo adabu kuwatizama wakubwa wakati wanakula. Hii ni kweli sijatia chumvi hata kidogo.

Na Mungu alimjalia watoto zaidi ya 20 kwa wanawake 4 alobahatika kuzaa nao. Na kama kuna mwanaye mwenye elimu zaidi ya darasa la 7 basi walisomeshwa na wajomba zao.
 
Wangu mimi alikuwa kama jogoo wa kuku wa kienyeji. Akishatia mimba anasepa hakuna hata matunzo kwa hao waliikwa wake zake. Pia hakuwa na mpango wa matunzo kwa watoto wala matibabu wala elimu. Pia hata wakati anakula mtoto ukisogea karibu atakuchapa kwa kigezo kuwa siyo adabu kuwatizama wakubwa wakati wanakula. Hii ni kweli sijatia chumvi hata kidogo. Na Mungu alimjalia watoto zaidi ya 20 kwa wanawake 4 alobahatika kuzaa nao. Na kama kuna mwanaye mwenye elimu zaidi ya darasa la 7 basi walisomeshwa na wajomba zao.
So sad mkuu! Mbaya sana hii ila sihukumu, nasema tu.
 
Back
Top Bottom