Sema chochote kwa Baba yako, leo Father's Day

Sema chochote kwa Baba yako, leo Father's Day

Kama ilivyo siku ya akina mama/wanawake duniani March 8, leo June 21 ni siku ya akina Baba japo husahauliwa sana kwenye Media.

Tuseme maneno mazuri kwa mzazi huyu huyu wa kiume hata kama alishatangulia mbele za Haki.

View attachment 1484889
happy fathers day to my father may almighty GOD bless him for all that he has done to me up to now i pray to God so that one day i can be a good father......Jah bless
 
Wangu mimi alikuwa kama jogoo wa kuku wa kienyeji. Akishatia mimba anasepa hakuna hata matunzo kwa hao waliikwa wake zake. Pia hakuwa na mpango wa matunzo kwa watoto wala matibabu wala elimu. Pia hata wakati anakula mtoto ukisogea karibu atakuchapa kwa kigezo kuwa siyo adabu kuwatizama wakubwa wakati wanakula. Hii ni kweli sijatia chumvi hata kidogo. Na Mungu alimjalia watoto zaidi ya 20 kwa wanawake 4 alobahatika kuzaa nao. Na kama kuna mwanaye mwenye elimu zaidi ya darasa la 7 basi walisomeshwa na wajomba zao.
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
 
Mungu akupumzishe mahali pema peponi baba yangu ulinifaa Sana maishani kitabu chako ulichokiandika ambacho hukukimalizia nitakimalizia baba yangu pumziko la milele akupe ee bwana ..!
 
Nakushukuru mzee wangu kyaka kwa kunifundisha maisha ..nakumbuka ulipokea kipensheni chako 2012 Ila nilichoambulia ni pagara la vyumba vitatu ukasepa zako..mungu akuongoze na akuponye na mkeo huko ulipo..
Hilo pagara mwandalie chumba kimoja hapo atarudi tu akishakamuliwa vya kutosha huko
 
Mungu akupe maisha marefu zaidi BABA yangu, Wewe ni kila kitu kwangu, Zaidi sana nawaombea BABA zetu wote waliotangulia mbele za haki. Mungu azidi kuwarehemu. Nami najiombea kwani mda si mrefu nitakuwa BABA mtarajiwa.Kama BABA yangu alivyohangaika huku na huko kutafuta fedha kwa ajili yangu na MAMA yangu na wadogo zangu, Basi nami nikafuate mkondo huo huo wa BABA.



MUNGU AWABARIKI BABA ZETU WOOOTE TANZANIA NA DUNIANI KWA UJUMLA.


[emoji1292][emoji1292][emoji1292][emoji1292][emoji1292][emoji1292][emoji1292][emoji1292][emoji1292][emoji1292][emoji1292][emoji1292][emoji1292][emoji1292][emoji1292][emoji1292]
 
Back
Top Bottom