Selfika na JF: Snap it. Show it

Selfika na JF: Snap it. Show it

Screenshot_20211219-131448.jpg
 
YESU NI MWEMA.

Nimetafakari mpaka nilipo, nami nashindwa kuelewa kabisa,
Binadamu angenipa neema, kesho angechoka kunipa zaidi,
Lakini wewe hauna kikomo, wala mvua yako haina majira,

Bwanaa wanyesha mvua
Bwanaa kwa walio jangwani,
Bwanaa wawasha jua
Bwanaa kwa walio baharini,
Kweli bwana wewe ni mwema sana,

Nitasimulia nchi yesu ni mwema, yesu ni mwema,
Nitahubiri vijiji yesu ni mwema yesu ni mwema,
Nitayafafanua haya yesu ni mwema, yesu ni mwema,
Watu wote wapate kuyajua yesu ni mwema, yesu ni mwema,

Niliwaza kwa ubinadamu mpaka mwisho wa kufikiri,
Ukataka nijipe moyo, nisihofu kitu kamwe
Wanihurumia maana wee wanisaidia,
Ukataka nijipe moyo, nisihofu kitu kamwee.

Nitasimulia nchi yesu ni mwema, yesu ni mwema
Nitahubiri vijiji yesu ni mwema, yesu ni mwema
Nitayafafanua haya yesu ni mwema, yesu ni mwema
Watu wote wapate kuyajua yesu ni mwema, yesu ni mwema

Uzoefu wa maandiko haya, ukaninyima usingizi
Ukataka nijipe moyo, nisihofu kitu,
Dhambi za duniani, zikavunja matumaini
Ukataka nijipe moyo, nisihofu kitu kamwee.

Nitasimulia nchi yesu ni mwema, yesu ni mwema,
Nitahubiri vijiji yesu ni mwema, yesu ni mwema
Nitayafafanua haya yesu ni mwema, yesu ni mwema
Watu wote wapate kuyajua yesu ni mwema, yesu ni mwema

Giza lililotanda mchana, likanifunika usoni,
Ukataka nijipe moyo, nisihofu kitu,
Nikapiga kelele, hofu kuu ilanizonga,
Ukataka nijipe moyo, nisihofu kitu kamwee,

Nitasimulia nchi yesu ni mwema, yesu ni mwema
Nitahubiri vijiji yesu ni mwema, yesu ni mwema
Nitayafafanua haya yesu ni mwema, yesu ni mwema,
Watu wote wapate kuyajua yesu ni mwema, yesu ni mwema,

Naimba leoo,
Naimba leoo,
Naimba leoo,
Naimba mimi.

Ulijua wazi kwaamba mimi sikua nastahili, kwa sababu mimi mdhaifu mwili na roho,
Ukaruhusu juhudi zangu nifanikiwe, makusudi ili nione ukuu wako,
Ndugu wanipende,
Jamaa waniheshimu
Marafiki wanijari, wanisaidie,

Ndio maana leo mimi nakurudushia, utukufu ni wako milele,
Sifa na heshima ni vyako daima, wewe pekee yako unastahili,
Usifiwe na uhimidiwe,

Nakushukuru bwana, kwa kuwa umeniona ahsante,
Nakupa utukufu, kwa kuwa umeniona ahsante,
Milele na milele, kwa kuwa umeniona ahsanteeeeeeeeeeeeeee.

..........

Siku ya leo kwangu ina baraka na rehema tele, imenifanya niwe mpya, na kuanza ukurasa mpya wa mwaka mwingine ktk maisha yangu.

mood.
 
Back
Top Bottom