Selfika na JF: Snap it. Show it

Haha wala sijavutiwa na muonekano wake mkuu kwa sababu mimi sioni kama ni sifa sana mwanaume kuwa mzuri wa sura dogo kipaji anacho. Mimi kati ya Messi na Ronaldo namkubali Messi na wakati Ronaldo ndiyo ana muonekano mzuri.

Watu wengi hasa sisi wanawake ukiwauliza wanamkubali nani kati ya hao watakuambia Ronaldo kwa sababu tu ni mzuri sijui mrefu na wanamchukia Messi eti kisa mfupi. Sie tunaofuatilia mpira hatuangalii hayo tunaangalia kazi uwanjani.

Anyway siyo mbaya yawezekana huyo naye yuko vizuri lakini mimi simkubali sana maana kwenye mpira kila mtu na machaguo yake. Kuna mwingine atakuambia Allan ndiyo yuko vizuri kwenye assists kuliko Bukayo ni mtu tu vile anaona.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…