Selfika na JF: Snap it. Show it

Kwa anaethubutu kumuuwa mtu kwa sababu zozote zile,I mean zozote zile kama ni kuchukuliana wake au sijui kudhulumiana pesa au kunyang'anyana vyeo iwe yoyote ile inampasa kujua kwamba furaha yake haitoletwa kwa kumtoa yule anayemchukia duniani,tujifunze kuishi katikati ya maadui zetu!

Yeye ameondoka ila duniani wapo watu kuishi kwao walitegemea uwepo wa huyu mtu,watoto walitegemea Baba yao awaletee chakula kama wanao wanavyokutegemea wewe,awalipie school fees kama unavyofanya wewe,Baba/Mama yake pengine ni wazee sana tayari wana maradhi sugu yanayotaka pesa kununua dawa na ilikuwa zitoke kwa huyu marehemu sasa hawazipati ni wengi huwahitaji wapendwa wao pale wanapofariki hii dunia tunategemeana so kila mmoja wao niliowataja atakapokosa huduma atamkumbuka huyu mtu na kila anapomkumbuka nafsi yake huugua na kila atakapoumia machozi yake hulipwa directly kwa muuwaji kwa njia mbalimbali ambazo anaweza azione au asizione hili huwa kama fumbo na hutembea na kizazi cha muuwaji.

Tuheshimu nafsi za watu,inanifaa nini kuuwa mtu kwa kitu ambacho sina guarantee ya kuki-maintain hata miezi miwili ijayo?maana hata kama nitachukua pesa je nikifa kesho then zitanisaidia nini?kazi?je nikifukuzwa?tamaa ya mali nikiondoka mwaka mmoja baada ya kuuwa nitaondoka nazo kiasi gani?

Inasikitisha?Mungu Mwenyezi amrehemu apate pumziko la milele.
 
Tuheshimu nafsi za watu,inanifaa nini kuuwa mtu kwa kitu ambacho sina guarantee ya kuki-maintain hata miezi miwili ijayo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…