Dear
Sisi ni binadamu na tunakosea kwa maana hakuna aliye mkamilifu. Najua ile siku wakati tunakusema humu uliumia na ulijisikia vibaya kwa kuwa ulisingiziwa.
Binafsi naomba nisamehe kwa kukusingizia kuhusu ile ishu. Nakiri kuwa mimi ndiye mwenye makosa kwa kukutuhumu na kukusema vibaya na kukaa kimya pia.
Na niliona nikae kimya kwa sababu nilihisi kama ningeongea tena ningezua ugomvi mwingine mkubwa zaidi. Haya yote chanzo ni mimi wala asilaumiwe mtu mwingine yeyote.
Once again im very sorry. Naomba nisamehe yaishe.