Yoyooo....!!
No retreat No surrender aluta continue/
Nawashambulia wengi wanajuta kunijua/
Bokonya Boko haram boss wa mistari/
Nakuachia alama kama umepigwa kofi na askari/
Nakupa tahadhali acha pupa na papara/
Tazama shoto kulia kama unavuka barabara/
Mi ni vazi lenye upupu bishoo usinivae/
Niko makini mweusi zaidi ya Joh na wanawe/
(Yooh)..Naponyonga kwa fasihi.......!
Kama rap ni kukohoa mimi ni mgonjwa wa T.B/
Nafungua mdomo nabonga kwa bidii/
Hadi sikio la kufa leo litaonja sauti hii/
Mi ndo emcee mwenye lundo la ujuzi kwenye kichwa/
Hizi tungo zimekazwa kama nyuzi kwenye gitaa/
Nawaficha...maraper wapuuzi nawazika/
Na wenye mistari mbuzi nawaficha.....!!!!