Selfika na JF: Snap it. Show it

Selfika na JF: Snap it. Show it

(ndoto yake ni kuona tunajenga jamii ambayo tunasukumana kwenye mstari wa ushindi...”. )

Aiseeee maneno mazito Sana haya

I wish binadam wote tungekua na roho
Kama ya huyu jamaa
Hii kitu kwetu Africa imekuwa changamoto sana,ujitoa sana kwenye jamii unaonekana unakiherehere,ukiwa bandidu una roho mbaya. Yaani kunawakati hatueleweki tunataka nini.

Lakini kwenye jamii bado kuna watu wema na waaminifu na wenye kuona mafanikio ni kijiti cha kupokezena. Tuendelee kuombeana tuone huo umuhimu wa kutembea pamoja kwenye mafanikio.
 
Mkuu huku tukiendelea kumuombea st Anne,nguvu ya kuvuka salama katika kipindi hiki kigumu,hii imenikosha sana.
Naomba niiweke kidogo kwenye lugha yetu mama.

Huyu ndugu mweusi anaitwa Abel Mutai, ni mwanariadha wa nchi ya Kenya. Wa nyuma yake (huyo mzungu) anaitwa Ivan Fernandez, ni mwanariadha wa Hispania.

Mwaka 2013 kwenye mbio za Burlada, Ivan Fernandez alifanya kitendo cha kibinadamu, kimaadili na cha heshima kubwa sana. Hakushinda mbio mahala ambapo kwa tamaa zetu za kibinadamu angeweza kushinda.

Ni kwamba, walipokaribia ‘finish line’, Mutai, ambaye alikuwa anaongoza mbio hizo, alikosea sign ya ‘finish line’ akatoka mchezoni kwenye race na kuanza kushangilia kuwa ameshinda, kitendo ambacho kingempa Ivan fursa ya kuwahi kwenye finish line na kuchukua medali ya dhahabu na kumfanya Mutai ajute, alie na kusaga meno.

Ivan hakutaka ushindi wa kinyemela, ambao angeupata tu kutokana na makosa ya Mutai.

Alimfuata Mutai kule nje na kumrejesha kwenye ‘lane’ huku akimuongelesha kihispaniola kuwa bado hawajafika, japokuwa Mutai alikuwa haelewi lugha hiyo lakini alifuata maelekezo ya Ivan na kufika kituo cha mwisho akachukua ushindi wake. Na Ivan akabaki kwenye nafasi yake ‘halali’ ya ushindi wa pili. Watu hawakumshangilia sana Mutai lakini Walimheshimu sana Ivan.

Sababu ikiwa ni moyo wake wa kibinadamu wa kumsukuma Mutai kwenye mstari wa ushindi mpaka akapata haki yake. Ivan alipohojiwa alisema “ndoto yake ni kuona tunajenga jamii ambayo tunasukumana kwenye mstari wa ushindi...”.

Mwandishi wa habari akamuuliza, “lakini kwa nini ulimuacha Mkenya akashinda wakati ungeweza kuwa mshindi?”, Ivan alijibu “sikumuachia ushindi. Alikuwa ameshinda. Ushindi ulikuwa haki yake”.

Mwandishi akasisitiza, “lakini ungeweza kushinda?”. Ivan akajibu: “lakini ningepata raha gani juu ya ushindi huo? Nini ingekuwa heshima ya medali hiyo? Mama yangu angefikiria nini juu ya hilo?”

Mungu atujaaliye tupate watoto wema kama Ivan, watakaokuwa tayari kushinda kwa mbinu halali za ushindi, watakaokuwa tayari kusimama kwenye kanuni za maadili, heshima na uaminifu.
Mungu atujaaliye tupate watoto wema kama Ivan, watakaokuwa tayari kushinda kwa mbinu halali za ushindi, watakaokuwa tayari kusimama kwenye kanuni za maadili, heshima na uaminifu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii kitu kwetu Africa imekuwa changamoto sana,ujitoa sana kwenye jamii unaonekana unakiherehere,ukiwa bandidu una roho mbaya. Yaani kunawakati hatueleweki tunataka nini.

Lakini kwenye jamii bado kuna watu wema na waaminifu na wenye kuona mafanikio ni kijiti cha kupokezena. Tuendelee kuombeana tuone huo umuhimu wa kutembea pamoja kwenye mafanikio.
Hakika muhimu n tuzid kuombeana
Tu na walau binadam wa Africa Sisi
Tunaweza kubadilika siku moja
Na tukawa Kama Ivan
 
!!
20210603_184918.jpg
 
Mbunge Viti Maalum, Josephine Genzabuke: Naomba niishukuru serikali ya CCM inayoongozwa na Jemedari, Mheshimiwa Rais, mama yetu Samia Suluhu kwa kufanikisha mkopo wenye Masharti nafuu kutoka benki ya maendeleo ya Afrika tukaweza kuahidiwa pesa dola za Kimarekani 140 sawa na shilingi laki tatu elfu ishirini na nne point nne Bilioni.

Na meza zikagongwa kushangilia, hivi anazijua pesa alizotaja!
 
Back
Top Bottom