Tunaita kinaka/kikanda.
Watu wa nyanda za juu kusini watakuwa wanaelewa zaidi.
Kinaota ardhini,kinachimbwa km viazi,kinaanikwa kinatwangwa,kinaanikwa tena, kinachekechwa ,inakuwa kama unga hivi.
Upikaji wake watu huchanganya na karanga zilizotwangwa na kuchekechwa .
Kinawekwa magadi, na chumvi,,wengine huweka pilipili kuongeza ladha.
Kinasongwa kama ugali ..
Waweza kula na ugali ama chenyewe kama hivyo.