Selfika na JF: Snap it. Show it

Na halafu sijuagi kama ninakuwaga na hayo majibu..😁😁kya..
Basi nitajitahidi kuwa nayachuja na chujio la tui bubu ili nisiudhi watu😁😁😁

Huyo uliomtaji hapo namuonaga mjeur sana ingawa kuna wakati nikisoma comments zake naishia kucheka sana najiulizaga Hivi huyu alikuwa anawaza nini maana ni vituko aiseh 😁😁😁
 
Nami nimeshangaa sana! Haya magonjwa ya mlipuko yanasababishwaga na mambo kama haya haya ya watu kutaka kula kila kitu sijui popo sijui nyoka sijui kenge wooiii!
Haki mpka muda huu bado mate yananijaa mdomon utafikiri mjamwepesi kha...
Hivi inamaana don amekosa hata kadigidigi au kaswala kweli mpka ale hicho kiumbe apo🤭🤭🤭🤭magonjwa ya mlipuko nje nje
 
Duuh pole sana aise next time bora upande treni utaenjoy sana! Ila last time nilivyopanda treni kulitokea ajali ile section ya mlimba kuna treni ya mizigo mbele huko ilipata ajali kwahiyo treni yetu ikapigwa stop mlimba pale tukaambiwa tusubiri hadi lile treni liilopata ajali litolewe na reli itengenezwe ndiyo tuondoke uliza tulikaa masaa mangapi!

Tulisimama asubuhi tukaja kuondoka kesho yake asubuhi muda kama ule wenye ndugu au jamaa zao pale mlimba hawakulala kwenye treni walienda kulala huko na sisi abiria tulioanzia safari dar wakatugaia hela za msosi sababu ya muda tuliopoteza! Ninachoshukuru ni kwamba tulisimama sehemu yenye mtandao pale pale mlimba stesheni vinginevyo tungekoma maana si unajua treni zinakopitaga!

Mimi wote nawakubali ila Heaven Sent namkubali zaidi sana since day one na ndiye ninayetamani sana nifahamiane naye nje ya JF ila nawaza namuanzia wapi! Ukizingatia HS siyo mwepesi kumuamini mtu yaani hadi akuamini aisee basi ujue ni kakupenda sanaaaaa ila Mtende ndiyo kabisaaa hata nikitaka kufahamiana naye nitajisumbua tu maana hapa jukwaani hatuna mazoea kabisa!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…