Upendo ni amri kuu na ya kwanza iliyojumuisha amri zote.
Injili Kama ilivyoandikwa na Marko Mtakatifu 12:30
"Nawe mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote,na kwa roho yako yote,na kwa akili zako zote,na kwa nguvu zako zote."
Kuhusu kujali
Marko12:31b
"Mpende jirani yako Kama nafsi yako"
Sifa za upendo;
Soma waraka wa kwanza wa Paulo Mtume kwa Wakorintho 13:4-8
Upendo;
•Huvumilia
•Hufadhili
•Hauhusudu
•Hautakabari
•Haujivuni
•Haukosi kuwa na adabu
•Hautafuti mambo Yake
•Hauoni uchungu
•Hauhesabu mabaya.
•Haufurahii udhalimu bali hufurahi pamoja na kweli
•Huvumilia yote
•Huamini yote
•Hutumaini yote
•Haupungui neno wakati wowote;bali ukiwapo unabii utabatilika;zikiwapo lugha zitakoma;yakiwapo maarifa,yatabatilika..
. . . . . . . . .
Huwa nashangaa Sana mtu anakwambia anakupenda halafu sifa ya kwanza kabisa ya upendo ambayo ni uvumilivu hana.