Nilipelekwa kwenye park mkuu na nikashawishiwa kupanda kwenye hiyo ride. Yaani mnapanda mpaka huko juu kabisa sijui ghorofa ngapi huko halafu mnarudi chini upside down almost vertical fulu fosi mpaka kuna kimuda hapo mtu unajihisi kama vile huna uzito kabisa (zero gravity). Yaani kabisa kifo unakiona laivu hiki hapa, kichwa kinakuuma, moyo unausikia kama vile unataka kuchomoka, matumbo yanakusokota ali mradi vurugu tu. Wengine mpaka wanapoteza fahamu. Aliyenishawishi kupanda mpaka sasa hatuongeleshani