Pole Mkuu kukwazika!
Kwa uzoefu wangu humu wa miaka 13, mtu anaweza kupost yupo Kigoma, kumbe yupo Botswana, ama mwingine akapost Mkono wa kike, kumbe nje ya Keyboard ni Mwanaume
Mwingine kupitia maandishi yake humu, mkadhani ni Kijana wa miaka 30, kumbe ni Mzee wa miaka 63
Wengine tunaweza kupost tunakunywa Chai holiday inn hotel, kumbe tupo tunafakamia mihogo ya kuchemsha huku Ifakara
Mathalani, nimepost hiyo picha lakini mlaji alikuwa ni mtu mwingine tu
Sisi Wazee kazi yetu ilikuwa kulipa bill tu 😜
Hoja yangu ni kwamba, ili kuendana na maudhui ya mada tajwa, hadhira ya hapa chitchat huposti picha yoyote ili kuibua mijadala na kusogozana tu.