Selfika na JF: Snap it. Show it

Babu ni sehemu gani kuna mashamba bei nafuu na ardhi yake inakubali mazao aina mbalimbali😁😁
Ardhi nyingi zinakubali mazao ya aina mbalimbali, changamoto ni hali ya hewa ya hayo maeneo.

Mathalani, Mkoa wa Morogoro unakubali mazao aina nyingi ni wewe kuchagua lipi lina faa Kwa wakati huo Kwa kuangalia hali ya Soko.

Kama unataka kulima angalia mazao ya biashara.

Iwe Ufuta, Miwa, Karanga, Mpunga, Choroko n.k

Mikoa ya Morogoro, Rukwa, Katavi, Ruvuma, Mbeya inasapoti mazao tofauti kulingana na hali ya hewa nzuri.

Fanya utafiti Kwa kutembelea huko.

Ukiwatumia wenyeji una uhakika wa kupata ardhi Kwa bei nafuu zaidi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…