Selfika na JF: Snap it. Show it

Ushauri mzuri Mkuu.

Kutengeneza scheme za umwagiliaji kunahitaji fedha nyingi kidogo.

Kule kwenye korosho hatuhitaji maji mengi, kwahiyo mvua za wastani zinatosha, muhimu matumizi ya Viutalifu.

Kule kwenye miwa Kilombero, tunahitaji maji ya wastani, hasa unapoanza kulima kwa mara ya kwanza. Kule nimefunga pampu hivyo napata maji kadri ya mahitaji.

Kule Mbarali tunatumia scheme za umwagiliaji, ambazo tunapata maji kadri ya zamu tulivyojiwekea.

Ukitaka kufanikiwa kwenye kilimo, ni muhimu u-invest kwenye kilimo chenye tija.

Karibu shambani Mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…