Basi bwana majuzi nimeenda kunyoa, likaingia lidada moja hivi linanukia kweli limepaki Crown mpya nje. Yule muhudumu wa kike wa saloon akaliita pembeni, akaanza kuliambia, eti shost ile namba ya mganga wa Bagamoyo nimeshaipata. Likasema shost ahsante hebu nipe, umeona tayari yule mwanaume kashaniachia gari hilo hapo nje, sasa ntahakikisha atamwacha hata mke wake. Likapewa namba ya mganga, likaamua kuita boda-boda alikimbize Bagamoyo, gari likamwachia yule mwenzake wa Saloon.
Nikasema Hiiiiiiiiii Bagoshaa, kuna mwamba ashalizwa na hili tandam. Haya ndiyo maisha ya Darisalamu....