Japo huu ni uzi wa picha ila kwa vile watu wanatoa ya moyoni kidogokidogo sio mbaya na mie nikitumia hii fursa kuweka kachumbari.
Kiranga umekua msaada wa kunifanya nijifunze mambo mengi mkuu. Licha ya tofauti zetu kwenye baadhi yaambo (hii sifikirii ni tatizo) haijawahi kuwa sababu ya sie kukwaruzana.
Kama binadam wengine walivyo, kuna nyakati tunapishana lakini haijawahi kufikia kuvunjiana heshima. Ndio maana nnapokuita kaka, namaanisha.
Unajua kuchambua jambo au kutafakari kitu kabla ya kuchangia. Unatumia lugha ya kueleweka licha ya ukweli kwamba unaupeo ma uelewa mpana wa mambo kiasi unaweza kutumia maneno ya kitaalam tukabaki watizamaji tu.
Naendelea kupata upepo mwanana na tangawizi yangu pembeni
Heshima kwako mkuu