Selfika na JF: Snap it. Show it

Selfika na JF: Snap it. Show it

View attachment 2400721

I can't get over of this moment..

Actually one of the toughest moment of my life...

Hapa nilikuwa nimekimbia kazi nzuri sana ktk Kampuni kubwa sana hapa nchini...

I wrote my resignation letter nikawaambia naenda kujiendeleza kielimu lkn kiukwel I was running away...

Nobody knew what i was going through... Nakumbuka kuna jamaa aliniuliza dogo una uhakika na unachofanya... Nikamwambia Bro nina uhakika lkn moyoni nilikuwa na maumivu makali sana maana kazi nilikuwa naihitaji ukizingatia mazingira ya home lkn sikuwa na jinsi...

Baadae kwel nilienda kuchukua kikozi fulani cha muda mfupi ili kupotezea muda na mawazo kwa kutumia vile vijisenti nilivyokuwa nimekusanya pale jobuni...

Tulikuwa na eneo la familia la heka kadhaa katika mkoa fulani hapa nchini... Actually ni nje ya mji hasa porini... So Baada ya kugonga pepa nilimweleza Mama nataka niende huko nikafanye maendeleo ukizingatia sikuwa na kazi... Lakini moyoni hoja ni kustay away from people... Na niliona nikienda kule itakuwa sehemu sahihi ya kukaa mbali na viumbe waitwao watu... I just wanted to stay away from people intensively... Kila mtu nilikuwa namuona kama adui yangu...

Ukizingatia toka nilipopata bahati ya kuja hapa Duniani sikuwahi kuishi kujijini wala kujishughulisha na shughuli zenye mlengo wa kijijini... Maisha yalikuwa magumu sana kwangu... Kazi kubwa kule ilikuwa ni kulima na kufyeka mapori so nilijifunza kutumia jembe kwa ajili ya kulima na kutumia panga, shoka kwa ajili ya kufyeka vichaka na mapori...

Katika eneo letu hakukuwa na nyumba so nilifikia kwa Mwenyeji mmoja pale... Hivyo nilijenga nyumba kwa mikono yangu mwenyewe huku nikielekezwa na mwenyeji pale... Nilikata miti ya kujengea, nilichimba mashimo ya kusimikia miti, nilichimba udongo wa kukandia, nilifuata maji ya kuchanganyia udogo na maji yalikuwa shida kwel na kupatikana mbali.... Kwa upande wa kufunika boma na kuweka mlango nilipata usaidizi wa moja kwa moja kutoka kwa mwenyeji wangu...

Baada ya nyumba kukamilika nilihamia pale, nikatengeneza kitanda cha miti ili nipate mahali pa kuegesha mgongo... Hahahahaha

Niliishi hapo kijijini kwa takriban miezi 7 without serious interactions, nilikuwa nashinda hapohapo kuanzia asubuhi hadi siku hadi siku... Nyumba pale zilikuwa mbali mbali sana so kwa sehemu kubwa miji ilikuwa imezungukwa na mapori makubwa so nyoka wakubwa walikuwa wamejazana sana na kuna siku wanaamua kuja kukutembelea...

I can't forget that day nimetoka kufuata maji, ile nimerudi nyumbani nafungua mlango nasikia kitu kama kimekurupuka na kujificha mahali, nikajivuta kwenda kuchungulia nikaona nyoka mkubwa(Cobra).....

Katika yote bado najitahidi kuwapenda watu ambao Mungu aliamini ni sahihi kwa ajili yangu na kunifanya niwe karibu yao... Namshukuru tu!

Bado sijaget over but i am trying as much as possible kurejea...

Mkiona maisha yenu yanasonga smoothly just thank God.

Picha credit kwa dogo langu alikuja kunisabahi kaka yake so akatake that photo.
Bado unaishi huko mkuu?
 
Thimbaaa
Sisi tunamtaka Mgunda
Screenshot_20221028-120543.jpg
Screenshot_20221028-090100.jpg
 
Back
Top Bottom