Kuna watu watakutia moyo kipindi unapoanza harakati za kimaisha, ila ukishaanza kufanikiwa wataanza kukuwekea vikwazo. Kumbuka sio wote wanafurahia mafanikio yako, na ukifeli tuu wataanza kusema alikuwa anajiona sana. Usifanye jambo kumfurahisha mwanadamu hata siku moja maana maadui ni wengi sana na huwezi kuwatambua.