Napo naweza yaani usafiri wowote ule ili mradi tu niwe nasafiri ila najua kuwa air hostess itaendelea kubaki kuwa ndoto tu sababu ya sura na umbo kwahiyo labda meli au treni lakini basi hapana
haki vile natamanigi sana hiyo scene inikute siku moja ila tu isisababishe ajali,, tena nikiwa ndani ya dude moja la uarabuni kati ya emirates au etihad siyo hutu tupanzi twetu..
Sasa wewe safari ya ndege tu unachoka?? Wakati wengine tunatamani hata ndege zipate hitilafu ili safari iwe ndefu??
Kuna dereva mmoja wa shuttle kule mbeya alinisimulia walipanda fast jet kutoka dar kuenda mbeya wakafika mbeya wakakuta mvua kubwa inanyesha wingu zito limetanda anga haliko shwari hivyo hawawezi kutua
Rubani akaambiwa arudishe ndege dar wakalale dar watarudi mbeya kesho kwa ticket zile zile na hakutakuwa na gharama zozote za ziada labda sehemu za kulala kwa siku hiyo ndiyo abiria wangejitegemea
Nasikia wakarudi dar kesho yake wakaanza tena safari kuenda mbeya ndiyo wakafika salama,, nikasema looh mimi mbona na kusafiri kwangu kote na ndege sijawahi kukutana na kadhia kama hizo jamani ili safari iwe ndefu maana dar mbeya lisaa limoja tu mmefika sipendi mimi..