Una uhusiano gani na huyo mtu uliyemwamini kukuandikia recommendation letter? Kama ni profesa alikufundisha una uhakika bado anakukumbuka? Mara ya mwisho uliwasiliana naye lini au mtu hamjawasiliana tangu uondoke chuo na leo ndiyo umekurupuka tu kumtafuta baada ya kuomba kazi inahitaji recommendation.
Jenga tabia ya kuwa karibu na watu wachache unaojua kuwa ni wa muhimu katika maisha yako; na usiwatafute tu pale unapokuwa unawahitaji. Hili ni jambo la muhimu sana maishani.