#SELF_DEFENCE_USIKAE_KINDEZI_NDEZI
1- Unatembea ngumi hujui, pistol huna, kisu huna hata peni kama speedo huna, ukikabwa unalia lia, ata kama husomi weka peni mfukoni kama huna silaha nyingine.
2-Hata kama huvuti, weka kibiriti hasa cha gesi mfukoni. Mtu kakukaba shingo kiwashe mchome nguo au sehem yeyote sepa.
3-Geto usikose Nondo, panga , bisbis, kamba au waya .
4- Usisahau nguo nzito kama blanket na maji incase of fire.
5- Unapoenda sehem mgeni unamsubir mtu, sio unakaa sehemu moja lisaa lizima tena kiboya boya hadi wahuni wajue we mgeni.
6-Uwe na mbio maana kuna time ndio zinakuwaga suluhisho
7-Unaelekea ktk uchochoro unaona kuna watu huwaelewi nao wanakuja, nawe unaenda tu, utalizwa, subiri kwanza au tafuta njia nyingine.
8--Kila siku ukienda misele unapita njia moja hiyo hiyo , ata washirikina wakikuotea hukwepi, jichek, jifunze kupita njia tofauti tofauti.
9--Ukiingia kwenye nyumba/ jengo mara ya kwanza, angalia na sehem za kutokea, sio unaenda kma mbuzi, kuwa kama mbwa mark sehem mlizopita na mbadala wake pia.
10-Mtoto wa kiume usilale ukavua nguo zote, utaja zalilika
11- jifunZe kubana punzi kwa muda usiopungua dk tatu, zile robbery za kitoto utazimudu.
12-- kama hujui kuogelea na unaenda maeneo ya maji, beba kudumu cha mafuta kilichoisha cha lita tano chene mfuniko, incase of anything, kiweke kifuani ukuwa umekifunga mfuniko maji yasiingie ndani, kishikilie haswa, hutazama miaka mia
NB: NI KWA WEMA TU, USITUMIE VIBAYA.