mbingunikwetu
JF-Expert Member
- Feb 17, 2015
- 13,663
- 18,037
Mazuri ya sekretarieti ya ajira kwenye utumishi wa umma:
1. Imejitahidi kuweka uwanja sawa kwa wote wanaotafuta ajira. Kama ni ugumu basi huo ugumu uko kwa wote!! Kinachotafutwa kwa sasa ni kutaka kuboreshwa uwanja kwa baadhi ya watu almaarufu kama "watoto wa wakubwa". Wanataka kuwapitishia mlango wa nyuma kupitia kinachoitwa eti WALIOJITOLEA WAPEWE KIPAUMBELE. Ieleweke kuwa ni watoto wa wakubwa tu ndio watapewa fursa ya kujitolea kwenye taasisi za serikali zenye maslahi mazuri kama TRA, BOT, NSSF nk
2. Imerahisisha sana namna ya kuomba ajira kupitia recruitment portal. Ukishaweka vyeti vyako huko huhitaji tena kila unapoomba ajira utambatanishe na vyeti!!
3. Kila mwenye sifa huwa anaitwa kwenye usaili hata kama ni wengi. Hii humpa fursa kila mwenye sifa ajaribu bahati yake. Hii inaondoa kabisa hisia ya rushwa! Wengine wamelalamika kuwa sekretarieti huwa inaita watu wengi sana! Lakini ni sawa kwa sababu kama sifa za msingi wanazo acha waje wachujwe kwa usaili.
Mapungufu ya Sekkretarieti ya ajira katika utumishi wa umma:
1.Kutokuweka wazi marks/alama za wasailiwa kwenye ngazi ya oral interview. Hii inasababisha hisia ya upendeleo. Tunawataka sekretarieti waweke waqzi pia alama za wasailiwa kwenye oral interview.
2. Kutokuweka wazi orodha ya wasailiwa ambao wamefaulu usaili lakini hawakupata nafasi na majina yao kuwekwa kwenye kanzidata/database kusubiri upatikanaji wa nafasi ya ajira. Tunawataka sekretarieti waainishe marks za wasiliwa wa oral kama wafanyavyo kwenye written interview. Na orodha ya kwenye kanzidata/database iwe wazi kwa kigezo cha marks za oral. Vinginevyo kanzidata inaweza kutumika kama mlango wa nyuma wa kupitishia watu kwa upendeleo maana hiyo database iko gizani kwa sasa!
Ushauri kuhusu mawazo ya baadhi ya watu (hasa watu wakubwa) kutaka sekretariet itoe kipaumbele kwa waliojitolea:
1. Tusiwatwike mzigo sekretariet kushughulika na watu ambao hawakuhusika katika kuteuliwa kwao kwenye kujitolea kwao. Kama tunataka kujitolea iwe ni sifa mojawapo ya kupata ajira, basi waomba ajira wote wapewe fursa ya kushindania kila nafasi ya kujitolea inapopatikana maana haiwezekani waombaji wote wapate hiyo nafasi ya kujitolea. Kwa hiyo haki ni kuwapa fursa wote kushindania hizi nafasi za kujitolea kwa kufanya usaili wa written na oral. Wanaofaulu wanaingizwa kwenye database na kupewa fursa ya kujitolea. Nafasi ya ajira ikitokea HAKUNA TENA HAJA YA KUWAFANYIA USAILI bali wanapewa ajira moja kwa moja toka kwenye database!!
2. Kila nafasi ya kujitolea ikipatikana LAZIMA itangazwe na wote wapate fursa ya kuiomba na kuifanyia usaili unaofanywa na sekretarieti. Viongozi serikalini na kwenye taasisi wasihusike kabisa kwenye kutoa nafasi ya kujitolea kwa watu ili kutokutoa mwanya wa rushwa na upendeleo.
NAOMBA USHAURI HUU UMFIKIE WAZIRI MWENYE DHAMANA NA UTUMISHI PIA UMFIKIE RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MAMA SAMIA H. SULUHU.
Tujihadhari maana tunataka kupigwa changa la macho kupitia mlango wa nyuma wa ajira kwa kujitolea!!