Wakuu
Nguruvi3,
BONGlander,
EMT
Kuhusiana na gharama za muungano, na jingi gani zinanufaisha Zanzibar kuliko Tanganyika:
Kwanza, tuangalie takwimu kwenye bajeti za Muungano na Zanzbiar.
Kwa mujibu wa Bajeti ya Zanzibar, kwa mwaka wa fedha 2013-14, vyanzo vya mapato ya Zanzibar kutoka nje vilikuwa kama ifuatavyo:
1. Ruzuku na mikopo kutoka nje kwa ajili ya program za maendeleo -
shillingi Bilioni 235.
2. Misaada ya kibajeti, shillingi bilioni 40.
Hotuba ya waziri wa fedha wa Zanzibar inatamka wazi kwamba
karibia 90% ya fedha hizi zinalipwa na watanganyika. Kwa maana hii, watanganyika kwa mwaka wa fedha uliopita walilipia karibia
shillingi bilioni 250 kati ya karibia bilioni 280 kwa ajili ya maendeleo ya Zanzibar kupitia mkakati wa kukuza uchumi Zanzibar (MKUZA), kutimiza ndoto za wazanzibari yani - vision 2020 ya Zanzibar, at the expense of MKUKUTA ambayo ni ya kimuungano kuliko tanganyika na vision 2025 ambayo pia ni ya kimuungano kuliko Tanganyika.
Tukiangalia AID per capita, kwa kipindi husika (2013-2014), aid per capita zanzibar ilikuwa ni karibia shillingi
215,000. Je kwa upande wa Tanganyika, hali ipo vipi?
Tukiangalia kwa upande wa Muungano uliovaliwa koti na Tanganyika (ambako Zanzibar pia ni sehemu ya eneo hili), kwa mwaka wa fedha 2013-2014, jumla ya mikopo kutoka nje ilikuwa ni
shillingi trilioni 2.4, na Aid per capita ikiwa ni kama shillingi
53,000. Kwa maana nyingine, AID per Capita kwa Zanzibar ni karibia mara nne kwa Tanganyika, AID ambayo ni mtanganyika ndio amekuwa akienyeshwa kwa karibia 90% with nothing in return.
Tuendelee kuangalia takwimu nyingine (
Kobello, bado naendelea to compile takwimu mbalimbali kwa ajili ya gharama za serikali mbili). Soon nitaweka sources zangu.
| Population
| Ukubwa wa eneo (Square Kilometers)
| Per Capita Income (shillingi)
| Fedha za nje (Miradi ya maendeleo) (Dollars) FY 2011-2012)
| Mchango wa Pato la Taifa (shillingi)
|
Zanzibar
| 1.3 million
| 2,650
| 1,000,000/=
| $56.9 million
| 850 billion
|
Mtwara
| 1.3 million
| 16,710
| 700,000/=
| $1.7 million
| 927 billion
|
Kigoma
| 2.1 million
| 37,040
| 500,000/=
| $298,000 thousand
| 906 billion
|
Sindiga
| 1.4 million
| 49,340
| 480,000/=
| $14.9 million
| 662 billion
|
Tabora
| 2.3 million
| 49,340
| 530,000/=
| $2.5 million
| 1.2 trillion
|
Lindi
| 900,000
| 66,040
| 670,000/=
| $1 million
| 622 billion
|
Ni suala lisilohitaji kutumia akili nyingi sana kubaini kwamba:
Mikoa niliyotaja hapo juu, mikio hii ya Tanganyika ni miongoni mwa mikoa masikini kuliko yote nchini. Kwa maana nyingine, mahitaji ya fedha za maendeleo katika mikoa hii ni makubwa kuliko maeneo mengine mengi sana ya Tanzania. Lakini cha ajabu ni wamba - ukiangalia fedha za nje kwa ajili maendeleo kwa mikoa hii mitano, jumla ya fedha hizi ni chini kidogo ya dollar milioni sita. Kiwango hiki ni sawa na karibia 10% tu ya jumla ya fedha zilizokwenda Zanzibar katika kipindi husika, kwa gharama za mtanganyika (rejea hotuba za waziri wa fedha wa zanziabar). Kwa maana nyingine nyepesi mikoa masikini ya Tanganyika inatengewa fedha chache za maendeleo kuliko Zanzibar kwa ushahidi huu. And this is despite the fact that:
· Mikoa hii mitano ina jumla ya wakazi milioni nane. Idadi ya watu Zanzibar haifiki hata robo ya idadi ya watu wa mikoa hii only 16%.
· Zanzibar wana eneo la ardhi ambalo ni only 1% of the total land size ya mikoa hii mitano ya Tanganyika.
· Zanzibar has a much higher per capita income kuliko mikoa hii, meaning kuna umaskini zaidi katika mikoa hii kuliko umaskini uliopo Zanzibar. Hata hivyo, wao wana MKUZA na DIRA yao 2020 ya kuwatoa kwenye umaskini kivyao (lakini kwa gharama za mtangtanyika) huku mtanganyika yeye akiwa na MKUKUTA na DIRA 2025 kama jamhuri ya muungano wa Tanzania (Zanzibar ikiwa ndani yake).
· Mikoa ya Tanganyika (kwa mfano Mtwara, Kigoma, Tabora), michango yake kwa pato la taifa (GDP) ni mikubwa kuliko ya zanzibar lakini bado Zanzibar wanavuna zaidi katika fedha za maendeleo kuliko mikoa hii. Kwa mfano, hapo juu tunaona kwamba mchango wa pato la taifa kutoka mkoa wa Tabora ni (shillingi 1.2 trilion), Mtwara (927 billion shillings), Kigoma (900 billion shillingi) huku Zanzibar ikiwa ni about 850 billion shillings. Pamoja na haya, badi katika kipindi husika, Zanzibar walipewa karibia $60 million dollars kama fedha za maendeleo kutoka nje (90% zililipiwa na wananchi wa mtwara na sehemu nyingine za Tanganyika), huku mtwara katika kipindi hicho ikiambuliwa kiasi kisichozidi $2 million, Kigoma kama $300,000, mtwara sio zaidi ya $2 million. Tukichukua jumla ya fedha za maendeleo kwa mikoa hii mitatu, fedha hizi hazivuki $5,000,000. Kwa maana nyingine, katika kipindi husika, mtwara, kigoma na tabora fedha za nje kwa ajili ya miradi ya maendeleo zilikuwa ni chini ya 10% ya fedha hizi kwa upande wa Zanzibar!.
· Haya yote yanatokea licha ya the fact kwamba Zanzibar wanayo higher per capita income kuliko mikoa hii miwili, meaning poverty ni kubwa zaidi kuliko Zanzibar.
Uzi wangu wa gharama za serikali mbili utakuja na analysis zaidi, lakini kwa sasa nadhani tayari tunapata picha juu ya nini kinaendelea.
Kuna suala linguine ambalo ningependa pia kulijadili. Miezi kadhaa iliyopita, tulisikia jinsi gani makada wengi wa CCM walivyokuwa wakiwavunjia heshima tume ya kina jaji warioba, kwa mfano kwamba mapendekezo ya rasimu yatamwongezea mwananchi gharama kutokana na uwepo wa marais watatu. Wakaelezwa kwamba sio lazima viongozi hawa waitwe marais, lakini bado wakaja na hoja kwamba hawa watakuwa ni viongozi wakuu wa serikali hivyo gharama zipo pale pale. Walicholenga kina mzee warioba ni kupunguza gharama kwa wananchi kutokana na utitiri wa viongozi uliopo chini ya serikali mbili ambapo kuna:
1. Rais wa Jamhuri ambae wala hana mamlaka kijamhuri.
2. Makamu wa Rais wa Jamhuri ambae hana kazi yoyote.
3. Waziri Mkuu wa Jamhuri ambae hana mamlaka ya kijamhuri.
4. Rais wa Zanzibar ambae sasa ana hadhi sawa na rais wa JMT kwa vile Zanzibar ni nchi, na katika mambo mengine, kuwa na hadhi zaidi ya rais wa jamhuri.
5. Makamu wa kwanza wa rais Zanzibar cheo hiki kipo to accommodate siasa za muungano kuliko uchumi wa muungano.
6. Makamu wa pili wa rais Zanzibar hiki cheo pia ni kwa ajili yaku accommodate zaidi siasa za muungano kuliko uchumi wa muungano.
Hawa ni viongozi sita wa kitaifa, tofauti na idadi ambayo tume ya warioba ilipendekeza.
Wengi tulisubiri kuona iwapo kweli kina Sitta Dodoma wangekujana mfumo ambao ungelenga kumpunguzia mwananchi gharama katika suala la viongozi wa kitaifa kama tulivyojadili hapo juu. Kinyume chake tunaona mwendelezo wa vituko na mazingaombwe. Huu ni ushindi mkubwa kwa Jaji Warioba na wananchi walio toa maoni yao kwa tume ya katiba. Hii ni kwa sababu, badala ya Sitta pale Dodoma kupunguzia wananchi mzigo, wameongeza mzigo huo kwa mependekezo kwamba kuwe na:
1. Rais wa JMT ambae wala hatujui atafanyaje kazi yake ndani ya jamhuri yenye nchi nyingine ya pembeni Zanzibar. Badala ya kutatua tatizo hili, tusishangae CCM ikaamua kuongeza gharama zaidi kwa walipa kodi wa Tanganyika kwa kuunda tume za kutatua migongano ya marais.
2. Makamu wa kwanza wa rais mgombea Mwenza useless kabisa.
3. Makamu wa pili wa rais rais wa Zanzibar ambae ana nchi yake ndani ya JMT;
4. Makamu wa tatu wa rais ambaye pia ni waziri mkuu.
5. Makamu wa kwanza wa rais Zanzibar
6. Makamo wa pili wawili wa rais zanzibar.
Kina Samuel Sitta na Chenge wameleta katiba yenye viongozi wenye hadhi ya urais wapatao sita.
Sasa tuje kwenye gharama:
Hamad Rashid Mohamed ni mbunge mzanzibari. Katika mchango wake kwenye BLK mwezi aprili mwaka huu, alikanusha madai kwamba wazanzibari waliondoka kwenda Dodoma na msimamo wa serikali tatu. Hamad hakusema ukweli kwani kuna ushahidi kwamba sio BLW tu bali hata BLM nalo liliweka msimamo wa serikali tatu. Katika hoja zake za kupinga serikali tatu, Hamad Rashid alinukuliwa akisema haya:
Leo Rais akisafiri anatumia sio chini ya shilling
milioni mia tano, na mara nyingine hadi
shilling bilioni moja. Hizi ni wakiwa madarakani tu, wakistaafu je?
Hamad Rashid Akauliza:
Viongozi hao wakistaafa watatu kwa pamoja itakuwaje? Huu ni mzigo mkubwa kubebesha wananchi.
Sote tunajua kwamba mishahara na posho za viongozi wa kitaifa hugharamiwa na Serikali ya muungano Tanganyika iliyovaa koti la muungano. Swali letu ni je:
Baina ya rasimu ya tume ya Jaji Warioba na rasimu ya Chenge, rasimu ipi ni nafuu kwa walipa kodi wa Tanganyika katika suala la kugharamia viongozi wa kitaifa?
Tunaelezwa kwamba mshahara na posho kwa kiongozi kama waziri mkuu ni shillingi milioni 25 au zaidi kwa mwezi. Na tunajua kwamba hizi zinaenda mfukoni zote, hazilipi kodi. Na mbali ya hilo, waziri mkuu anahudumiwa na serikali kwa mambo yote ya ndani na nje ya nyumba yake, meaning katka shillingi milioni 25, hatoi hata shillingi kumlipa mtunza bustani. Chini ya rasimu ya CCM, waziri mkuu anaongezewa kofia ya umakamu wa rais, hivyo kuwa na hadhi ya ki-urais, na kwa maana hii, mshahara na mmarupurupu yake chini ya rasimu ya chnge lazima pia viongezeke.
Lakini tukiamua kutumia kiwango hiki hiki cha milioni 25 kwa mwezi kiwe ni mshahara na posho kwa viongozi wote wa kitaifa (Rais wa JMT, Makamu wa kwanza, makamu wa pili, makamu wa tatu, makamu wa kwanza Zanzibar na makamu wa pili zanzinar), maana yake ni kwamba chini ya rasimu ya change, watanganyika sasa watalipia mishahara na posho kwa viongozi hawa jumla ya shillingi - not less than 150 million kwa mwezi. Kwa mwaka mzima, sio chini ya shillingi 1.8 billion. Hapo hatujajumlisha matunzo yao ambayo hayagusi mishahara yao, na hatutajumlisha zile shillingi milioni mia tano hadi bilioni moja ambazo hugharamia safari za viongozi hawa (kwa mujibu wa Hamad Rashid). Nadhani hapa tunaona jinsi gani viongozi wanafanya wananchi wajinga. Hivi Hamad Rashid akihojiwa juu ya kauli yake ya mwezi aprili, atajibu nini?
Mniwie radhi kwa typing errors na makosa mengine madogo madogo, nitarudi kufafanua sehemu zote ambazo zitakuwa zimeleta utata. Vinginevyo hoja ya msingi inasimama.
Cc
Barubaru,
chama,
MwanaDiwani,
Gamba la Nyoka,
Mwigulu Nchemba,
Ezekiel Maige,
humphrey chipolepole, dingswayo,
Pasco,
MTAZAMO,
ZeMarcopolo,
MJINI CHAI[MATETa]
Hizi takwimu ulizotoe labda uliandaliwa na wazungu wa unga a.k.a MATEJA
Kuhusu hayo uliyasema eti ni kwa mujibu Wa waziri wa fedha wa Zanzibar ingelikuwa vyema ukadondosha ushahidi hapa vyenginevyo huyo waziri uliemsikia labda mulikaa chemba akakwambia.
Nilisema kabla kuwa kawaida ya watanganyika ni kuropoka tena wanaropoka uongo ambao hata nukta ya ukweli huo
Chuki zenu kwa Zanzibar na wazanzibar zitawafanya mufe huku mnajiona maana mtaikuta Zanzibar na wazanzibar wanasonge mbele.
Hii hapa hotuba ya waziri wa fedha wa zanzibar ya bajeti ya mwaka 2014/ 2015 halafu utuonyeshe hiyo asilimia 90% ya bajeti ya Zanzibar inatoka bara.
Wenyewe njaa zimewajaa hadi kwenye masikio hivyo mnahitaji kusaidiwa leo halafu.
Nyinyi ni njaa kali ambao mnaitegemea Zanzibar muwadhulumu ili mpate alau mlo mmoja, na tokea lini kwenye njaa akamsaidia MTU.
Kiufupi Tanganyika haina uwezo wowote Wa kuisaidia Zanzibar, ila Zanzibar ina uwezo Wa kuisaidia Tanganyika na tayari imeshafanya hivyo wakati wa nyerere! Njaa zilipowazidi watanganyika alimtuma Amir Jamal kwenda Zanzibar kuomba na kwa kuwa wazanzibar ni waungwana sio washenzi walimsaidai na wamepiga kimya mpaka Leo.
http://www.zanzibarassembly.go.tz/budget/2014/ministerial/HOTUBA-WIZARA-FEDHA-2014.pdf