Pona
JF-Expert Member
- May 26, 2014
- 1,099
- 647
Mkuu hujajibu hoja za Cameron kuhusu aliyosema. Hapa unajaribu kubadilisha mjadala.
Halafu unadai tunapotosha, wakati tumetumia hoja za Cameron na yaliyotokea.
Tunataka devolution yenye kutoa haki na usawa kwa Tanganyika kama ambavyo Wales, England na Ireland zinavyokwenda kupewa haki sawa na Scotland.
Usichokijua kutoka Scotland ni sawa na kinachotokea Zanzibar. Kwamba, mafuta yamewatia kiwewe.
Hata hivyo, bado wanahitaji ulinzi wa kiuchumi na usalama na hilo ndilo limepelekea wengi kuogopa kujitoa.
Na znz ni hivyo hivyo, kwamba wanahitaji kubaki na jina la Tanzania ili wapate ulinzi wa kiuchumi na Uslama.
Tatizo ni kuwa znz wanadai hayo kwa gharama za Mtanganyika.
Ni upuuzi wa hali ya juu sana kudai devolution za mikoa wakati kuna wznz 84 wanaochukua rasilimali zaidi ya mikoa 10 hadi 20 ya Tanganyika.
Ni upuuzi kudai devolution wakati znz yenye watu 1.2 inachukua kiasi cha takribani bilioni 500 kutoka Tanganyika kwa jina la Tanzania. Wewe unaficha unyonyaji unaofanywa kwa jina la Tanzania na ili kufikia lengo hilo hutaki kusikia Tanganyika.
Tanganyika inahitajika kwa utambulisho na fiscal autonomy yake na si vinginevyo
Mkandara, hatuwezi kuishi na Tanzania ambayo ni mzigo mkubwa sana kwa Watanganyika.
Tunataka fiscal autonomy kama wznz ili kuondoa kama si kukomesha upuuzi wa kupora kwa kutumia jina la Tanzania.
Leo tumeshaeleza mchango zero wa znz, na muungano kubebwa na Tanganyika kwa jina la Tanzania.
Hiyo TRA ya Tanganyika inakusanya kodi na kuzipeleka znz, wakati huko znz ZRB haina mchango kwa Mtanganyika.
Huwezi kuzuia hilo kwasababu jina la Tanzania linawahusu wznz, la waznz ni lao. Huu upuuzi tunaukomesha sasa.
Devolution lazima ianze na nchi na hapa uwepo wa Tanganyika. Halafu tutaangalia maeneo ya kusaidia wazanzibar
Nasisitiza kuwasaidia wznz kwasababu sisi hatuwahitaji.
Unachopigania wewe kama ulivyowahi kusema huko nyuma ni kutorudi kwa Tanganyika.
Ulisema Tanganyika ikirudi Wazanzibar watapata taabu sana(nukuu ipo kama unaitaka)
Hivyo usilaghai watu kwa kujifanya ni Mtanzania kuliko Mtanganyika. As long as znz ipo, Tanganyika inahitaji haki yake
Lazima tukubaliane kuwa znz ni mzigo na tatizo kubwa, na kwamba wao ndio wanapaswa kuji-adjust kuishi na sisi kwasababu wanatuhitaji kuliko tunavyowwahitaji.
Ndivyo Scotland ilivyoamua, kwamba itabaki katika muungano lakini washirika wengine wapewe haki kama wao.
Niseme kuwa hujaweza kujibu au kufafanua hoja za Cameron kama nilivyokuuliza.
Hiyo maana yake ni kukubaliana na aliyosema. hatuoni kwanini unaendelea kubabaisha watu.
Jibu hoja si kutuondoa katika mada kwa vioja.
Kwani wewe ndugu yangu unaichukuliaje Zanzibar Kama Zanzibar?
Zanzibar kuwa na watu 1.2 na udogo wa eneo lake sio sababu ya kuipotezea hadhi Zanzibar hadhi yake! Kama unaipima nchi kwa idadi ya watu wake, mapana na marefu yake basi kwanini hamkuungana na Sudani, Kongo Kinshasa au naijeria!!??
Hebu msikilize baba wa taifa lako kuhusu Zanzibar halafu uje na hii post yako.
Nyerere Hidden Speech:Zanzibar and Tanganyika are : http://youtu.be/hyO1_ro_UDg