Ndugu,
Tatizo la watu kama wewe mnaziangalia siasa za Uingereza mkiwa nje na kuanza kujenga hoja ambazo hazina ukweli kiuharisia na kimantiki. Unatakiwa uzichambue kwanza katika historia yake na hali ilivyo kwa sasa.
Bila kufanya uchambuzi fasaha unajenga hoja kama hii hapa chini kutaka kuwaaminisha wanaJF,
Waliokuwa wanataka uhuru kamili ni viongozi wa SNP ambao walijiunga na wananchi wengine katika mwanvuli wa harakati wanaouita Scottish nationalism.
Hoja ya Mamlaka kamili ilikataliwa na wananchi wengi katika kura ya maoni. Wewe bado unaongelea Mamlaka Kamili.
Hoja yako haitofautiani na madai ambayo yamekuwa yanatolewa na baadhi ya wanasiasa nchini walionukuliwa katika mikutano ya hadhara wakidai wanataka Zanzibar na Tanganyika zipewe MAMLAKA KAMILI.
Baadhi ya wanasiasa wa kikundi kinachojiita UKAWA walinukuliwa wakisema,
Kuanza kujenga hoja katika msingi wa kitaifa na kuondoa uchama kwenye siasa za Uingereza ni kupotosha au kutokuzifahamu siasa za Uingereza.
David Cameron hakukubali kufanyika Kura ya maoni kwa sababu ya kusukumwa na mstakabali wa kitaifa bali kwa sababu ya kupambana na chama cha Labour.
Chama cha Labour ambao ni waanzilishi wa devolution nchini Scotland hawakutaka kufanya kura ya maoni badala yake waliamua kuwapa madaraka zaidi lakini waendelee kuwa sehemu ya Muungano kwa sababu Scotland ni ngome yao katika maamuzi ya Westminster.
Kwanza lazima uelewe kuwa chama cha conservative kina mbunge mmoja tu anayetoka Scotland katika Bunge (Westminister) wakati Labour wana Wabunge kama 40, kwa maana kuwa chama cha conservative hakikubaliki Scotland.
Kujitenga kwa Scotland kungenufaisha chama cha Conservative katika bunge la Westminister zaidi ya Labour Party, ndiyo maana kwa sasa unamsikia David Cameron akisema anapenda kuwepo na English votes for English laws, kwa maana kuwa, masuala ya England yawe yanaamuliwa na wabunge wa England ambao kiuharisia, wabunge zaidi ya 40 wa Labour kutoka Scotland hawataruhusiwa kuamua masuala hayo. Kama hili litakubaliwa, basi chama cha Labour hakitakuwa na wabunge wengi watakao weza kupitisha maamuzi ya serikali itakayoundwa na chama cha Labour.
Chama cha Conservative kilikuwa na win win situation katika matokeo ya Kura ya Maoni na siyo kusema kilisimama katika msingi wa utaifa. Conservative walisimama katika msingi wa kichama, vivyo hivyo, Labour nao walisimama katika msingi wa Uchama ndiyo maana wanasiasa kutoka Labour ndiyo walikuwa wanapigana kihoja kwa hali na mali ili Scotland ibakie katika Muungano huku wanasiasa wa Conservative wakiwa wamekaa pembeni wakichekelea mtifuano.
Kinachofanyika katika suala la Scotland ni party politics ambazo kwa mtu asiye chambua kwa undani hawezi kuelewa.
Unafahamu kinachoendelea kwa sasa kuhusu suala hili kwenye Mkutano Mkuu wa Labour huko Manchester?
MwanaDiwani,
Kwanza, Usichanganye Watu kwa kujadili suala la kudai "mamlaka kamili" Kama vile ni sawa na suala la kutaka "kujitenga". Hivi ni vitu viwili tofauti Kabisa. Kaeni mkidanganyana Huko huko kwenye vikao vya chama, sio kutuletea upuuzi huu Kama vile kila mwananchi ni mjinga. Suala la "mamlaka kamili" ndani ya shirikisho sio tatizo, badala yake it's an asset to a federation kwani wananchi get to experience the best of both worlds, on the one hand, "shared Ruled" chini ya a national government, and on the other hand, "self rule", chini ya subnational government(s). Kwa mama nyingine Rahisi, ndani ya mfumo wa shirikisho, kila mshirika Anakuwa na mamlaka yake kamili Katika mambo ambayo hayapo Katika ushirikiano. Hii Ndio maana ya:
1. Fiscal autonomy.
2. Policy autonomy.
3. Political autonomy.
Tukiangalia Hapa kwetu, mshirika mmoja wa muungano yani- Zanzibar, tofauti na mshirika mwenza (Tanganyika), Zanzibar amepewa autonomy Katika maeneo haya. Kwa mfano, Zanzibar Ina:
1. Bajeti yake nje ya bajeti ya muungano.
2. Ina national Economic plan and policies nje ya muungano (mfano MKUZA vis a vis MKUKUTA)
3. Ina Dira yake ya taifa - vision 2020, tofauti na Ile ya muungano (na Tanganyika) ya vision 2025.
4.Ina chagua viongozi na wawakilishi wao nje ya siasa na chaguzi za muungano.
Etcetera.
Scotland iliyapigiania haya na kupewa serikali yake na bunge lake mwisho wa miaka ya tisini. Je tatizo likawa wapi hadi kupeleka kura ya maoni? Tutaelimishana:
Kama ulikuwa haujui, ujio wa kura ya maoni Scotland ulishaonekana miaka zaidi ya kumi iliyopita. Fanya utafiti, usipotoshe Watu. Pamoja na devolution kutokea Katika maeneo husika, Scotland bado hawakuridhika Kwa sababu kuu Mbili:
1. Uncertain future ya UK in the EU. Na utata juu ya Hilo unaweZa kuzaa Tena kura nyingine ya maoni Scotland muda sio mrefu, hasa iwapo UK wataamua kutojiunga na EU. Tuna tatizo Kama Hilo ndani ya muungano wetu kuhusiana nchi washirika and regional intergrarion but let's save this discussion for next time.
2. Pili ni Kwamba pamoja na Devolution to Scotland (serikali na bunge), bado kukawa na tatizo kwani it was more like a self-governing colony arrangement, kufikia kiwango cha kuwa na judicial appeals to the Privy Council katika masuala ya kikatiba. Hata ndani ya muungano wetu, tuna mgogoro mkubwa sana kuhusiana na judiciary issues but also on this one, leta save it for some other day.
Kutokana na haya, lakini hasa hili la pili, mgogoro mkubwa in the union UK was imminent. Lakini kwa vile wenzetu wana uongozi bora (sio sisi wenye bora uongozi) na wanaweka Maslahi ya nchi Mbele, haiku chukua muda mrefu, Wanasiasa wengi wa UK bila ya kujalisha itikadi zao za vyama, wakaanza kuona kwamba an independent Scotland was a real possibility kupitia kura ya maoni, na hii ilikuwa miaka kumi iliyopita. Again, the referendum for independence was noted over ten years ago. Ndio maana viongozi wakaanza kulifanyia kazi suala Hilo na kuambulia 55% "NO". Lakini Kama alivyojadili mleta mada, no vote didn't mean no to change Kama mnavyopotosha.
Katika suala la misimamo ya chama juu ya devolution ya Scotland, hili nalo unapotosha. Kumbuka, viongozi wa upinzani wakati wa Utawala wa Labour Party - 1997 to 2010, (wapinzani wakiwa ni Conservatives), awali they voted against devolution of scotland, lakini baada ya kusoma alama za nyakati, wakaamua kuachana na itikadi na badala yake kuweka utaifa mbele, na wakaamua kuungana na chama cha Labour kuhakikisha kwamba muungano unadumishwa through more devolution. Ni kwa mantiki hii, suala la devolution limekuwa a bipartisan issue Katika siasa za Uingereza. Hata katika elections manifestos za vyama vinavyounda coalition government ya sasa, suala la devolution lilikuwa at the fire front. Nenda kafanye utafiti utaona Hilo. Vyama vyote Vikuu nchini Uingereza vina msimamo mmoja, nao ni Kwamba muungano wa UK utadumishwa kwa kutoa mamlaka kamili kwa washirika wa muungano Katika masuala nje ya muungano - fiscal, policy and political autonomy.
Acha porojo zako juu ya nini kinaendelea Manchester. Hakuna chama kinachopinga "devolution", wanachopishana pengine ni the means to get there, basi.
Sent from my iPhone using JamiiForums