Bongolander
JF-Expert Member
- Jul 10, 2007
- 5,067
- 2,220
Sio kweli Kwamba the 4.5% formula is JFC's brainchild.
JFC ilizaliwa 2003, Wakati formula ya 4.5% ilibuniwa na BOT mwaka 1993.
JFC iliundwa miaka kumi baadae (203) kwa nia moja tu:
Kushauri "serikali Mbili" juu ya uchangiaji wa Mapato na matumizi ya muungano, and fiscal relations baina ya pande Mbili kwa ujumla wake. Maswali kwako:
1. Swali la kwanza:
Kwanini JFC ilidandia formula ya BOT?
Tukumbuke Kwamba - Kwa upande wa Mapato, tangia mwaka 1994, dividend za BOT zimekuwa shared 95.5% kwa bara na 4.5% kwa Zanzibar na haya yalikuwa ni makubaliano ya miaka mitano tu. Cha ajabu ni Kwamba formula hii ambayo haina ushawishi wowote wa kiuchumi, Ikaendelea beyond miaka mitano, na miaka kumi baadae kuja kubebwa na JFC in a copy and paste fashion.
2. Swali la pili kwako:
Kazi ya JFC ni kutoa ushauri kwa serikali Mbili za muungano juu ya masuala ya Mapato, matumizi na uchangiaji. Tunauliza Tena na Tena, utaweza vipi kushauri serikali Mbili juu ya gharama za muungano huku serikali moja wapo (Tanganyika) ikiwa imevaa koti la muungano?
Nadhani Unafahamu Kwamba - tangia mwaka 2003, waziri viongozi upande wa Zanzibar na mawaziri wakuu upande wa JMT(Tanganyika) wameshindwa kutekeleza mapendekezo ya JFC kwa sababu ya kupishana kwenye suala moja tu - juu ya serikali ya Tanganyika ambayo ingesimama kivyake kama ambavyo serikali ya Zanzibar inavyosimama kivyake za kwenye masuala yasiyokuwa ya muungano.
Tusisitize Tena Kwamba hii formula ya 4.5% haijaletwa na JFC, Bali ulikuwa ni ubunifu wa BOT mwaka 1993, Tena ubunifu wa kisiasa, Enzi za Mfumo wa chama kimoja, na Enzi za political interference on taasisi nyeti Kama BOT na Ile ya kodi - Kabla ya kuzaliwa kwa TRA 1995/6. Moja ya sababu za kuundwa kwa TRA ilikuwa ni pamoja na kuondoa siasa kwenye suala la kodi na Mapato ya nchi!
Pamoja na formula hii kukosa economic justifications, balance of payments na general budget support yamefuata hii formula, with 4.5% ya budget support kwenda Zanzibar. Budget support loans pia zinafuata the same formula na hata baadhi ya projects support huku projects nyingine zikiwa negotiated na wizara ya fedha ya muungano na Ile ya Zanzibar, on the basis of their respective needs and priorities. Na Hapa tunarudi pale pale na swali letu lingine:
• Kwanini Zanzibar wana "needs and priorities" za Kwao na bado wapo Katika needs and priorities na watanganyika kwa koti la muungano?
Mmekosa majibu ya maswali ya Nguruvi3 juu ya justifications za 4.5% na 21%, na badala yake mnakuwa na political "roundabouts". Kama alivyodokeza nguruvi3, 4.5% ya pato la taifa Kama gawio kwa Zanzibar ni sawa na (63 trillion x .045%) ambayo ni sawa na 2.8 trilion shillings; Lakini Mapato ya Zanzibar kwa mwaka (tax and non tax based revenues) ni 400 billion shillings, na pato la taifa la Zanzibar ni karibia 900 billion shillings, sasa hii transfer of at least 2.8 trillions kwa Zanzibar ni based on what economic grounds?
Kwanini Zanzibar apate mgao Mara Saba ya Mapato yake kwa mwaka (tax and non tax revenues)?
Kwanini Zanzibar apate mgao zaidi ya Mara Tatu ya pato lake la taifa kwa mwaka (GDP)?
Mwisho kuhusu 21% ya Ajira za muungano kwenda Zanzibar. Jumla ya waajiriwa wa serikali ya JMT ni 340,000 (tusisahau Tanganyika imevaa koti la muungano). Katika hawa, 21% ni nafasi za wazanzibari, equivalent to about 92,000 employees.
Zipo wapi economic justifications??
Takwimu muhimu:
• Proportion ya wazanzibari (1.3 million) Katika total population ya JMT (44million) ni
Kama 3%.
•Watumishi wa Zanzibar kwenye serikali ya muungano, yani the 92,000 ni sawa na 7% (92,000/1,300,000) ya jumla ya wazanzibari wote (total population).
• Jumla ya watumishi Katika serikali ya muungano kutoka Zanzibar ni 21%, huku Katika 79% iliyobakia, pia wakiwepo.
Maswali:
• Kwanini proportion ya wazanzibari Katika utumishi wa serikali ya muungano (at least 7%) ni at least twice of the proportion ya idadi ya wakazi wa Zanzibar kwa total population ya Tanzania - yani 3% (1,300,000/44,000,000)?
Maswali yote haya yanalenga kutafuta economic justifications za 4.5% and 21%, pengine utatusaidia na majibu, baadhi yetu tumeshindwa kuelewa nini kinaendelea.
Cc Nguruvi3, Mag3, JokaKuu, Dingswayo, chama MwanaDiwani, Pasco, Bongolander.
Sent from my iPhone using JamiiForums
Mchambuzi nakushukuru sana kwa kutudondolea hizi takwimu. Member mwenzetu Kobello ambaye anaona tunaotilia viulizo muundo wa Muungano wa sasa tuna matatizo fulani, labda anaweza kutueleza hapa takwimu hizi zinaeleza nini.
Wakuu labda tukubali kuwa hatujui sababu ya muungano, tukubaliane tu kuwa tujaribu kutafuta sababu za CCM kung'ang'ania muungano wa namna hii, na muungano una manufaa gani. Kimahesabu naweza kusema kwa kili yangu fupi naona ni hasara kwa bara, au ni unyinyaji wa wazi. Lakini najua kabisa watu wenye akili timamu wanajua kabisa this is monkey business. But the question is, wanajua kuwa ni ujinga na wakati huo huo wanafanya kitu ambachi wanajua ni ujinga na sisi tunajua ni ujinga, labda kuna kikubwa zaidi ambacho hatukijui ambacho kinawafanya wafikie maamuzi ambayo simple logic na common sense inasema haifai.
Kama Nyerere alivyowahi kusema "mimi sio kuku, sitagi mayai lakini mayai mabovu nayajua".
Sisi si wanahisabati lakini hesabu mbovu tunaweza kuzijua. Nadhani kama make up ya wazanzibar kwenye muungani ni asilimia 3 mgao wa nafasi za ajira kwenye mambo ya muungano uwe asilimia 3 kwa 97? Kama hii haifai basi nufaika ya Zanzibar ilingane na asilimia ya mchango wake kwenye muungano. Zaidi ya hapo ni usanii tu.