Mkuu Mkandara
Idadi ya wabunge hai determine maamuzi kwa mfumo wetu wa bunge.
1. Zanzibar imepewa 2/3 katika masuala ya muungano. In other words ni 2/3 ya 84 au 2/3 ya 15 bado itabaki 2/3
2. Kuna wawakilishi 5 kutoka BLW wanoingia bunge la JMT. Hao wanabeba maamuzi ya wawakilishi wa znz ndani ya bunge
Hoja yetu kubwa ni kuwa, kwavile wanakuja kwa sababu mahususi ya znz na wamepewa prerogative power ya 2/3 si kama wabunge wa Mwanza au Kigoma, SMZ inawajibika kuwalipia wao na si JMT ambako hawana mchango.
Ni weird idea lakini ukitazama ukweli kuwa hawana mchango wowote, basi huo ungekuwa mchango wao.
Kobello, tunaposema znz ichangie hatuna maana ichangie sawa. Tunajua ukubwa wa uchumi wake.
Msome
Bongolander kaeleza kinaga ubaga kuhusu dhana halisi. kama hawezi ku raise 1 trillioni,
Kuchangia kwa namna nyingine kunaweza kuwa kupunguza gharama anazobeba Mtanganyika.
Mfano, znz ina Maritime organization yake, hakuna sababu ada zake kule International maritime (IMO) zilipwe na solely Tanganyika huku znz ikikusanya mapato yasiyoingia muungano.
@Bongolander pia kazungumzia dhana ya wazanzibar kudai haki bila kuangalia uwiano au uwajibikaji.
Wznz wanataka fursa sawa, wanataka haki katika mgao. Je, wanawajibika kiasi gani katika muungano?
Mfano, kama miaka 30
Mchambuzi) kaonyesha na gavana kathibitisha hawachangii hata ile sehemu wanayopaswa, wapi wanapata haki ya kudai wasichochangia tena kwa usawa. Kumbuka kauli yao ya muungano wa haki na usawa
Leo wamedai asilimia 21 ya ajira, labda mtueleze ni formula gani imetumika kuwapa na kwanini formula hiyo isitumikekuchangia muungano.
Imefika mahali kwamba wanadai haki hata zisizowahusu.
Kwanini shirika lao la umeme likusanye kodi, bill ya umeme wa znz alipe Mtanganyika kwa kutumia jina la JMT. Hivi kama wangelipa bill zao, huo si mchango katika muungano kwa kumpungiza mtanganyika zigo nene analohema nalo mgongoni.
Na mwisho, Kobello, kama unaamini znz hawawezi kuchangia muungano, ni kwanini basi tumeungana.
Huwezi kusema suala la kuoleana maana Scotland na England wameoleana miaka 300 na bado walikuwa watengane.
Mchambuzi, hao wanaosema mikopo na misaada, lazima pia waeleze, deni la ndani la znz linalipwa na nani?
Wapi bajeti ya znz ina usalama na ulinzi, mambo ya ndani na nje.
Kwa maana kuwa deni la kukopa la Mtanganyika linatumika kwa huduma za znz kama ulinzi na usalama.
Je, deni lao ambalo Mtanganyika analipa kwa asilimia 90 kama ulivyosema, linatumikaje kwa Mtanganyika?