Jambo la kushangaza kuhusu macho yako na jinsi unavyoiona dunia.
Kila kitu unachokiona duniani kinapitia macho yako, lakini kuna jambo moja la kushangaza sana, huwezi kujiona moja kwa moja kwa macho yako bila kutumia kioo au kamera.
Kwa nini?
Macho yako hufanya kazi kama kamera
Mwanga unaingia ndani ya jicho
Unagonga retina
Ubongo hutafsiri kile kilichoonekana kuwa picha
Lakini ili ujione wewe mwenyewe moja kwa moja, macho yako yangelazimika kujigeuza na kujitazama yenyewe , jambo ambalo haliwezekani kimaumbile.
Lakini hapa ndipo jambo linapozidi kushangaza zaidi
Ubongo wako hauoni dunia kama ilivyo moja kwa moja.
Kile unachokiona ni tafsiri ya ubongo wako ya mwanga unaoingia machoni.
Hii ina maana:
Rangi unazoziona si rangi halisi, bali tafsiri ya ubongo.
Umbali unaouona ni makadirio ya akili yako.
Hata mwili wako unaouona ni ,picha iliyojengwa ndani ya ubongo.
Hitimisho
Kwa namna ya kushangaza.
Wewe hauoni dunia moja kwa moja… unaona toleo la dunia lililotengenezwa na ubongo wako.
Na ndiyo maana:
Watu wawili wanaweza kuona kitu kimoja lakini wakakielewa tofauti
Au mtu mmoja akaona kitu kipo, mwingine asione kabisa.