Idimi
Platinum Member
- Mar 18, 2007
- 15,506
- 11,439
Nini kiliiua hii kampuni ya mabasi??w
Kuna wengine wanasema ni 'Politics', kwamba kuna vigogo walikuwa na hisa zao mle, sasa waliziondoa.
Sababu za kifo cha Scandinavia (possible)
Ila mie nime-base zaidi kwenye uchumi. Scandinavia walikuwa na mikakati mibovu ya upanuzi wa soko.
1. Walikuwa wanasafirisha abiria wachache kwenda maeneo ya mbali, mfano basi la abiria 60 linasafirisha abiria 15 kutoka Dar hadi Arusha (650 km), au Dar hadi Kyela (1000 km), eti kwa sababu wanajali muda. Hii iliwagharimu sana, kwa sababu kusafirisha abiria kwa idadi hiyo ndogo kwa umabli huo ni hasara sana. Hilo hawakuliona, walijali muda zaidi.
2. Walijiingiza kwenye usafirishaji wa fedha na mizigo midogo (parcels) bila kujipanga. Mara nyingi sana walilazimika kulipia upotevu wa fedha na mizigo hiyo kutoka wizi wa wafanyakazi wao na ajali za mara kwa mara za magari yao, kutoka na huduma mbovu (poor vehicle services). Hili nalo liliwagharimu sana.
3. Walipanua masoko ya Uganda na Kenya bila kujipanga (waliongeza mabasi na routes) bila kuwa na mkakati wa kuimarisha routes zilizopo. Ushindani ukawa mkubwa, kwa hiyo wakawa kicked out of the market.
Matokeo yake, suppliers wa mabasi, mafuta, magurudumu na vipuri wakaanza kudai madeni yao, ambayo yalipelekea mabasi mengi kupigwa mnada kufidia madeni.
All in all, hii ilikuwa ni moja ya kampuni kongwe kabisa za usafirishaji abiria na mizigo kwa nchi yetu, ilikuwa ni icon kubwa kwa nchi.
I stand to be corrected.
Nawasilisha