Sayari nyingine saba sawa na Dunia zagunduliwa

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,410
_94807780_44569e0e-c8e0-4e98-8d5d-a4d5df73990d.jpg

Wataalamu wa masuala ya anga za juu wa Marekani wakishirikiana na wengine duniani, wamefanya ugunduzi mkubwa wa sayari saba zenye ukubwa sawa na wa Dunia ambazo zinaizunguka nyota mojawapo kama ilivyo kwa dunia kulizunguka jua.

Wanasayansi hao wa anga za mbali kutoka Marekani, Uingereza na Ubelgiji, wamebainisha kuwa sayari hizo saba walizozigundua zinaizunguka nyota ijulikanayo kwa jina la Trappist One.

Hata hivyo wanasayansi hao wamesisitiza kuwa kwa teknolojia iliyopo sasa inaweza kuwachukua maelfu ya miaka kuzifikia sayari hizo.

Thomas Zurbuchen kutoka shirika la NASA lenye makao yake makuu Washington nchini Marekani, amewaambia waandishi wa habari kuwa haya ni mafanikio hayo ni makubwa kisayansi na yanajibu maswali makubwa ya kisayansi

"Ugunduzi huu unatupatia vidokezo muhimu vya kuitafuta 'dunia ya pili', na kwamba sasa si jamba la kusema kama ingelikuwa hivi, bali sasa tunasema ni lini. Wanasayansi wanaamini kwamba takribani katika kila nyota moja kuna uwezekano wa kuwepo sayari moja. Chukulia sasa nyota tatu, nne, tano hadi saba, jiulize ni idadi ya dunia ngapi zilizopo pale,'' amesema Zurbuchen.

Michael Gillion ni mmoja wa wanajopo hilo la wana sayansi kutoka chuo kikuu cha anasema sayari tatu kati ya hizo saba zilizogundiliwa zipo karibu na nyota hiyo na zina sifa tofauti.

"Inaonyesha kuwa sayari hizi tatu kati ya hizo saba zilizogunduliwa zipo katika ukanda unaoweza kuruhusu viumbe kuishi, kwani maji yanaweza kupatikana na maisha ya viumbe hai yanaweza kuendelea, chakushangaza zaidi ni kwamba maisha yanaweza kuwepo hata katika uso wa sayari hizo," amesema Gillion.

Ugunduzi huu unatajwa na wanasayansi hawa kuwa ni mafanikio makubwa na umewaingiza katika ukurasa mwingine na kubakiwa na swali moja tu kwamba ni lini watazifikia sayari hizo badala ya kujiuliza kuwa katika anga hillo kuna nini.

Hata kuzifikia sayari hizo ni mtihani mwingine wani umbali wake hata mwendokasi wa mwanga, unaoongoza hapa duniani kwenda kwa haraka, unaweza kuzifikia sayari hizo baada ya miaka 40.

Chanzo: BBC
 
Sayari nyingine saba sawa na Dunia zagunduliwa

Saa 3 zilizopita

Mshirikishe mwenzako
Sayari zingine saba zagunduliwa anga za mbali

Wataalamu wa masuala ya anga za juu wa Marekani wakishirikiana na wengine duniani, wamefanya ugunduzi mkubwa wa sayari saba zenye ukubwa sawa na wa Dunia ambazo zinaizunguka nyota mojawapo kama ilivyo kwa dunia kulizunguka jua.

Wanasayansi hao wa anga za mbali kutoka Marekani, Uingereza na Ubelgiji, wamebainisha kuwa sayari hizo saba walizozigundua zinaizunguka nyota ijulikanayo kwa jina la Trappist One.

Hata hivyo wanasayansi hao wamesisitiza kuwa kwa teknolojia iliyopo sasa inaweza kuwachukua maelfu ya miaka kuzifikia sayari hizo.

Sayari inayofanana na Dunia yagunduliwaMambo muhimu kuhusu sayari ya Mars

Thomas Zurbuchen kutoka shirika la NASA lenye makao yake makuu Washington nchini Marekani, amewaambia waandishi wa habari kuwa haya ni mafanikio hayo ni makubwa kisayansi na yanajibu maswali makubwa ya kisayansi

"Ugunduzi huu unatupatia vidokezo muhimu vya kuitafuta 'dunia ya pili', na kwamba sasa si jamba la kusema kama ingelikuwa hivi, bali sasa tunasema ni lini. Wanasayansi wanaamini kwamba takribani katika kila nyota moja kuna uwezekano wa kuwepo sayari moja. Chukulia sasa nyota tatu, nne, tano hadi saba, jiulize ni idadi ya dunia ngapi zilizopo pale,'' amesema Zurbuchen.

Michael Gillion ni mmoja wa wanajopo hilo la wana sayansi kutoka chuo kikuu cha anasema sayari tatu kati ya hizo saba zilizogundiliwa zipo karibu na nyota hiyo na zina sifa tofauti.

"Inaonyesha kuwa sayari hizi tatu kati ya hizo saba zilizogunduliwa zipo katika ukanda unaoweza kuruhusu viumbe kuishi, kwani maji yanaweza kupatikana na maisha ya viumbe hai yanaweza kuendelea, chakushangaza zaidi ni kwamba maisha yanaweza kuwepo hata katika uso wa sayari hizo," amesema Gillion.

Kemikali inayounda sehemu ya ndani ya dunia

Ugunduzi huu unatajwa na wanasayansi hawa kuwa ni mafanikio makubwa na umewaingiza katika ukurasa mwingine na kubakiwa na swali moja tu kwamba ni lini watazifikia sayari hizo badala ya kujiuliza kuwa katika anga hillo kuna nini.

Nasa imetoa bango la "kusafiri" kwenda kwenye mfumo huo wa nyota

Hata kuzifikia sayari hizo ni mtihani mwingine wani umbali wake hata mwendokasi wa mwanga, unaoongoza hapa duniani kwenda kwa haraka, unaweza kuzifikia sayari hizo baada ya miaka 40.
 
Uu ugunduz mbona niliusikia muda sana kama five years nyuma, ila kiukwel hata mm naamini kuna second earth kwenye uulimwengu,
 
Ina maana zipo mbali zaidi ya Pluto? Mbona kuna kifaa kilishafika pluto kwa miaka minne na speed inayoizidi speed ya light.
Au wanadhani tumesahau?
Itakuwa ipo mbali zaidi ya pluto kwa maana pluto ipo ndani ya solar system yetu...
Ila hii ipo kwenye system ya nyota nyengine na tunaambiwa nyota tuliyokaribu nayo zaidi ya "alpha centauri" ipo umbali wa miaka minne na nusu ya mwanga.
 
tambua unaweza kuona kitu na usijue unachokiona ni kitu gani, hapo ndo linakuja suala la ugunduzi kwamba kumbe hiki ninachokiona ni ngedere sio nyau
MKuu neno sayari lipo siku nyingi tu huo ni muendelezo wa kuona na kuona kitu si ugunduzi, wewe umewahi kuona vingapi ! hivyo wewe ni mgunduzi au? Sikatai uzi wako ila tofautisha kuona na kugundua.
 
Ina maana zipo mbali zaidi ya Pluto? Mbona kuna kifaa kilishafika pluto kwa miaka minne na speed inayoizidi speed ya light.
Au wanadhani tumesahau?
Mkuu hizo sayari zilizogunduliwa zipo nje kabisa na mfumo wetu wa jua(solar system).. Pluto iko ndani ya mfumo wetu wa jua so hizo sayari zipo mbali mno.. Ukifuatilia utajua kuwa hizi sio sayari za kwanza kugunduliwa kuna mifumo yenye sayari inaitwa Kepler ina sayari nyingi tu zinazofanana na dunia na kuna moja ndo imelingana kwa karibu kila kitu sawa na dunia(wanaitwa twin Earth) inaitwa Kepler 186f (ipo 500 light years away) ila zote zipo mabilion ya kilomita huko na iliyokaribu nakumbuka ni kama 40 light years away.. Sasa 1 light year kumbuka ni umbali ambao mwanga unasafiri kwa mda wa mwaka mmoja sasa pigia mara 40...kwa haraka kumbuka mwanga unatumia kama dk 8 kusafiri kutoka kwenye jua mpaka duniani..
Kepler-186f - Wikipedia
 
Wakati sisi mioyo yetu ikiwa imebeba visasi wenzetu wamebeba zana kuelekea sayari ya Mars.
Wanachokifanya NASA ni ile asili ya mzungu ''Exploration''
Wazungu hawakubali kabisa kwamba kuna limits zinazoweza kuwazuia kutafiti.
Hata zamani walifanya ugunduzi wa mabara na leo wameadvance zaidi kwa kutafiti sayari.
Africa ni majanga tu maana kama kitu ni kikwazo basi kwa mtu mweusi ndo mwisho wa Dunia.
 
Mkuu hizo sayari zilizogunduliwa zipo nje kabisa na mfumo wetu wa jua(solar system).. Pluto iko ndani ya mfumo wetu wa jua so hizo sayari zipo mbali mno.. Ukifuatilia utajua kuwa hizi sio sayari za kwanza kugunduliwa kuna mifumo yenye sayari inaitwa Kepler ina sayari nyingi tu zinazofanana na dunia na kuna moja ndo imelingana kwa karibu kila kitu sawa na dunia(wanaitwa twin Earth) ila zote zipo mabilion ya kilomita huko na iliyokaribu nakumbuka ni kama 40 light years away.. Sasa 1 light year kumbuka ni umbali ambao mwanga unasafiri kwa mda wa mwaka mmoja sasa pigia mara 40...
Nimekuelewa sana mkuu ila hayo maneno niliyoandika aliwahi kuyaimba Mrisho Mpoto kwenye wimbo wake mmoja hivi.
 
Back
Top Bottom