Sauti yaleta balaa..

Sauti yaleta balaa..

Mmmm Sauti ya Stara Thomas v/s Barnaba ...Kweli Stara anasauti ya presentation na yaki business,ndiomana wakakupigia makofi,ila kwa kichumbanichumbani anafunikwa na yule sijui Barnaba(japo ni man)
 
Habari ya kitambo mabibi na mabwana wa jamiiforum. Natumai mnaendelea vyema katika shughuli zenu za kutafuta kipato, salamu ya pili iende kwa familia zenu, waambie Kasie anawapa Hi5!!

Baada ya salamu wacha niende kwenye tukio husika....

Kwa siku mbili tatu hizi ambazo nilipotea hapa nilikuwa mahali flani hivi nje ya South Afrika kuhudhurua moja ya warsha ambazo kampuni nnayofanyia kazi ina maslahi na warsha hizo. Nikiwa pale kuiwakilisha kampuni, niliteuliwa kuelezea makala iliyoandaliwa na kampuni yetu kwenye warsha hiyo na kama wadau wengine walioshiriki wakiikubali basi husaini mkataba wa makubaliano kibiashara hivyo kufanya kampuni yetu kuingiza hela na mie bonasi yangu ya mwaka inapanda.

Wakati uliwadia nikapanda kwenye kizimba kilichoandaliwa, nikaanza kuelezea na kudadavua kuhusu yote niliyoyataiwa kuyaelezea. Hadhira yote ilikuwa makini kunisikiliza na niligundua wengi walikuwa wananakili notsi. Baada ya kumaliza kuelezea makala hayo maswali na maoni yakaanza nakwambia hadi muda niliopangiwa ukapita kwasababu kulikuwa na kampuni nyingine ambazo nazo zilikuwa zinamakala ya kuelezea.

Nilipomaliza na kushuka kizimbani nilipiigiwa makofi na hadhira nzima tena kwanguvu.... hadi nikaona aibu nikawa narudi kwenye kiti changu huku natabasamu. Muda wa mchana ulipofika, kwenye mlo wa mchana wengi walifika kunisalimia na kuomba kadi yenye taarifa zangu (business card) wengi wao wakiwa wanaume. Wakati napata maakuli kijana mmoja alinifata mezani na kuomba jioni baada ya warsha tukae tuongee. Kwakuwa ilikuwa warsha ya kikazi nikakubali maana nikifanikiwa kufunga dili la kibiashara kwa ajili ya kampuni basi na mie mgawo wangu wa bonasi unakuwa mkubwa.

Jioni ya siku hiyo, nikajipara tayari kuongea na mdau, basi blaah blaah zikaanza mara mkaka akaanza kufunguka. Unajua Kasie, wakati uaelezea makala ya kampuni yenu sikuwa nasikiliza kitu wala kuelewa zaidi ya kubembelezwa na sauti yako....

Nikatabasamu na kuishia kucheka... Kaka akafunguka zaidi, kasie sauti yako matata, tamu, sikivu,......mwisho maongezi yakahama kabisaaa na kuelemea mrengo wa kushoto hheheheheee Kasie ni shiiideeerrr....... Huyo kijana alikuwa ni muafrika ila raia wa Ufaransa....

Basi baada ya warsha kuisha kila mtu akarudi eneo lake lazi, na hadi leo huyu kaka tunawasiliana vyema tu..... kimeishia hapo hehehehheeee......

Kilichonifanya niulete huu uzi hapa, nilijiuliza sana... hivi sauti ya mtu inaweza mfanya mwanaume au mwanamke amdondokee kimapenzi mwanamke / mwanaume...??

Halafu kuna ile, uko mahali unasikia sauti ya mtu bila kumuona, kiasi kwamba anakupa shauku ya kutaka kumuona na kutaka kujua mwenye hiyo sauti anafananaje wakati huo ushajenga taswira yako kichwani...

Nakumbuka hii ilishanitokea nikiwa kidato cha tano, siku hiyo nikatumwa kwenda darasa la kidato cha sita kumuita mwalimu wa darasa. Nikiwa nje ya darasa (mlango umefungwa) nikawa nasikia sauti tamu ya kijana akielezea kitu ubaoni, kumbe alikuwa ana present looh ile kuingia darasani basi daaahh ...... acha tu.....


Alamsiki japo wengine ndo tumeamka.
Mkuu, sio sauti tu hata huu mwandiko wako tu unatosha kuleta mfadhaiko. I bet pm yako iko very busy although hawajawahi kusikia sauti yako.
 
lov u kasie...thou makala zako nyingi ni za kufikirika! unajitahidi kuweka mawazo yako kwenye mtiririko unaofaa !!! najarbu kukadiria umri wako nachemka ila utakukua unachezea hapa 30- 39 right ?
 
Wimbo wa Stara,ila ntaipata sauti ya Kasie.

Ni sauti tu au na vitu vyako vingine vipo kwa watu?

Hhahahahahahaaaaa Analyse acha uchokozi banaa... najua wataka sikia sauti yangu na kuona na vinavyoambatana na sauti ya Kasie.... siwezi iweka hapa ila kweli tena sitanii, ukimsikia Bi Kasie anaongea waweza sema ni Bi Stara....

Kasie yuko full equipped kila kitu anacho ....
 
Mmmm Sauti ya Stara Thomas v/s Barnaba ...Kweli Stara anasauti ya presentation na yaki business,ndiomana wakakupigia makofi,ila kwa kichumbanichumbani anafunikwa na yule sijui Barnaba(japo ni man)

Looohh...... tobaaaa!!!! 😀😀😀
 
Mkuu, sio sauti tu hata huu mwandiko wako tu unatosha kuleta mfadhaiko. I bet pm yako iko very busy although hawajawahi kusikia sauti yako.

Hhahahahahahaaaa jamaniii kweli mwandiko wa Kasie unaleta mfadhaiko...!!? hehehehee usinifurahishe bana looh.

PM yangu waalaah haiko busy,na uzee huu nani anataka kuchat na kibibi ajuza? mie natabasamu tuu...🙂🙂
 
lov u kasie...
Love you too...
thou makala zako nyingi ni za kufikirika! unajitahidi kuweka mawazo yako kwenye mtiririko unaofaa !!!
Unawaza visivyo, simulizi za Kasie zote ni za uhalisia wa matukioa anayokutana nayo, yaweza usiamini, sina la kufanya ili uamini ila ukweli utabaki kuwa huo ni uhalisia wa Kasie.

najarbu kukadiria umri wako nachemka ila utakukua unachezea hapa 30- 39 right ?
Hhahahahahahhaaaa, why so interested with numbers? Anyways, Kasie's age has never been a secret.. am between 45 - 50. 😉
 
Hhahahahahahaaaa jamaniii kweli mwandiko wa Kasie unaleta mfadhaiko...!!? hehehehee usinifurahishe bana looh.

PM yangu waalaah haiko busy,na uzee huu nani anataka kuchat na kibibi ajuza? mie natabasamu tuu...🙂🙂
Vijana wenye ujasiri na wenye kuthubutu huku wakienda sambamba na kauli mbiu ya HAPA KAZI TU wapo wengi sana. Wakiongozwa na ile imani ya ng'ombe mzee hazeeki maini. Ni wewe tu bibie Kasie kuwakaribisha pm wapate kujifunza mambo ya wahenga.
 
Vijana wenye ujasiri na wenye kuthubutu huku wakienda sambamba na kauli mbiu ya HAPA KAZI TU wapo wengi sana. Wakiongozwa na ile imani ya ng'ombe mzee hazeeki maini. Ni wewe tu bibie Kasie kuwakaribisha pm wapate kujifunza mambo ya wahenga.

Hhahahahaaa Kasie sio mkufunzi banaa...😛
 
Back
Top Bottom