Sauti yaleta balaa..

Kasie

Platinum Member
Dec 29, 2013
22,041
39,992
Habari ya kitambo mabibi na mabwana wa jamiiforum. Natumai mnaendelea vyema katika shughuli zenu za kutafuta kipato, salamu ya pili iende kwa familia zenu, waambie Kasie anawapa Hi5!!

Baada ya salamu wacha niende kwenye tukio husika....

Kwa siku mbili tatu hizi ambazo nilipotea hapa nilikuwa mahali flani hivi nje ya South Afrika kuhudhurua moja ya warsha ambazo kampuni nnayofanyia kazi ina maslahi na warsha hizo. Nikiwa pale kuiwakilisha kampuni, niliteuliwa kuelezea makala iliyoandaliwa na kampuni yetu kwenye warsha hiyo na kama wadau wengine walioshiriki wakiikubali basi husaini mkataba wa makubaliano kibiashara hivyo kufanya kampuni yetu kuingiza hela na mie bonasi yangu ya mwaka inapanda.

Wakati uliwadia nikapanda kwenye kizimba kilichoandaliwa, nikaanza kuelezea na kudadavua kuhusu yote niliyoyataiwa kuyaelezea. Hadhira yote ilikuwa makini kunisikiliza na niligundua wengi walikuwa wananakili notsi. Baada ya kumaliza kuelezea makala hayo maswali na maoni yakaanza nakwambia hadi muda niliopangiwa ukapita kwasababu kulikuwa na kampuni nyingine ambazo nazo zilikuwa zinamakala ya kuelezea.

Nilipomaliza na kushuka kizimbani nilipiigiwa makofi na hadhira nzima tena kwanguvu.... hadi nikaona aibu nikawa narudi kwenye kiti changu huku natabasamu. Muda wa mchana ulipofika, kwenye mlo wa mchana wengi walifika kunisalimia na kuomba kadi yenye taarifa zangu (business card) wengi wao wakiwa wanaume. Wakati napata maakuli kijana mmoja alinifata mezani na kuomba jioni baada ya warsha tukae tuongee. Kwakuwa ilikuwa warsha ya kikazi nikakubali maana nikifanikiwa kufunga dili la kibiashara kwa ajili ya kampuni basi na mie mgawo wangu wa bonasi unakuwa mkubwa.

Jioni ya siku hiyo, nikajipara tayari kuongea na mdau, basi blaah blaah zikaanza mara mkaka akaanza kufunguka. Unajua Kasie, wakati uaelezea makala ya kampuni yenu sikuwa nasikiliza kitu wala kuelewa zaidi ya kubembelezwa na sauti yako....

Nikatabasamu na kuishia kucheka... Kaka akafunguka zaidi, kasie sauti yako matata, tamu, sikivu,......mwisho maongezi yakahama kabisaaa na kuelemea mrengo wa kushoto hheheheheee Kasie ni shiiideeerrr....... Huyo kijana alikuwa ni muafrika ila raia wa Ufaransa....

Basi baada ya warsha kuisha kila mtu akarudi eneo lake lazi, na hadi leo huyu kaka tunawasiliana vyema tu..... kimeishia hapo hehehehheeee......

Kilichonifanya niulete huu uzi hapa, nilijiuliza sana... hivi sauti ya mtu inaweza mfanya mwanaume au mwanamke amdondokee kimapenzi mwanamke / mwanaume...??

Halafu kuna ile, uko mahali unasikia sauti ya mtu bila kumuona, kiasi kwamba anakupa shauku ya kutaka kumuona na kutaka kujua mwenye hiyo sauti anafananaje wakati huo ushajenga taswira yako kichwani...

Nakumbuka hii ilishanitokea nikiwa kidato cha tano, siku hiyo nikatumwa kwenda darasa la kidato cha sita kumuita mwalimu wa darasa. Nikiwa nje ya darasa (mlango umefungwa) nikawa nasikia sauti tamu ya kijana akielezea kitu ubaoni, kumbe alikuwa ana present looh ile kuingia darasani basi daaahh ...... acha tu.....


Alamsiki japo wengine ndo tumeamka.
 
Hahaha Kasie huishi kutupa tashwishi kwa threads zako. Hii stori umeikatisha Nakumbuka siku za nyuma kuna mtu nilikiwa nawasilina nae mara kwa mara kupitia simu,ikafikia hatua nimkajengea hadi taswira,siku moja aifika kuchukua bidhaa zake ofisini,ahmad kibondoni,silka zangu ziliniangusha kwa kweli,wajihi wake haukufanana hata kidogo na umbile la sauti yake
 
Ah....hpo ndio nnapowapendea wanawake awe na miaka 18 ama 30 akili zao znafanana yaani hyu kusifiwa tu keshaamini km kweli sauti yke imemvuruga jamaa hakuna cha sauti wala nn jamaa keshakujengea picha kichwani anataka kidoti hcho ndio tabia zetu kiumeni mtoto wa kike ukimsifia lazma avurugwe c mmeona hyu hadi kaja anzisha uzi hp!
 
aliyeimba kinyago cha mpapuri humkumbuki, alipakiwa hadi ndege kwenda arabuni sijui kwa ajili ya mwarabu kasikia sauti tu
 
GENERAL RULE: "A man will say anything just to get in your pants."

HOWEVER: "There are always exceptions to the general rule."

Akili kumkichwa...
Mentor upo? Siku nyingi sanaaaa! Siwezi sahau ile story yako ulotuambia umeathirika. Hahaha you are a very good story teller
 
Back
Top Bottom