Azarel
JF-Expert Member
- Aug 25, 2016
- 29,020
- 40,791
Nikikumbuka yako...daah!hongera kwa sauti nzuri huo ndiyo ukike sasa
Nikikumbuka yako...daah!hongera kwa sauti nzuri huo ndiyo ukike sasa
Kasie bado umekufa, umeoza kwa Mmasai wako mwenye kirungu au tutume applications?I'll be back later dears .....😉
Hahaha...umenikumbusha mbali mkuu.Mentor upo? Siku nyingi sanaaaa! Siwezi sahau ile story yako ulotuambia umeathirika. Hahaha you are a very good story teller
Mi nadhani angetupiamo kapicha na ka "audio" ili tuhakikishe.Ha Ha Ha a a a....Kwa sauti gani Bibi wewe alikua anataka aonje asali yako tu hakuna lolo
ote
Hheheheheheeee unaona sasaaa....... kumbe wewe ni mtaalam wa vina na mizani na mashairi kwa ujumla eehh... Itabidi nikae karibu na wewe unifundishe... napenda sana hiyo lakini kupangilia hivyo siwezi.... Ila ntajifunza tuu, umenipa nguvu na hamasa ya kujifunza kupangilia vina na mizani.hahaha kiswahili lugha tamu kama maji ya mtungi wala hakiishi hamu
Heheheheheheeeee jamaniii, nimefanye tena...??Kassie wewe Kassie you never cease to amaze me.
Oooohhh thanks.... you know what..... you have all characters...... just like him, I hope its you... yes you are the one....🙂🙂You`re a living,breathing fantasy
Oooh thanks for clarification, shleeep welll....😛Hiyo ni silka=Insticts kwa lugha ya malikia. Alamsiki nuru bi nuur
Kasie bado umekufa, umeoza kwa Mmasai wako mwenye kirungu au tutume applications?
Age never an issue though..,
Wimbo wa Stara,ila ntaipata sauti ya Kasie.Gugo wimbo wowote wa wa Stara uusikilize, utaipata sauti ya Kasie barabara.
Nashukuru kwa salamu babuu, karibuuuu salamu zako nimeziitikia nami nakusalimia pia, hujambooo??!!
Acha banaNikikumbuka yako...daah!
Unapatikana wapi Kasie nithibitishe hiyo sauti. Kama ilimtoa huyo jamaa kimasomasoHabari ya kitambo mabibi na mabwana wa jamiiforum. Natumai mnaendelea vyema katika shughuli zenu za kutafuta kipato, salamu ya pili iende kwa familia zenu, waambie Kasie anawapa Hi5!!
Baada ya salamu wacha niende kwenye tukio husika....
Kwa siku mbili tatu hizi ambazo nilipotea hapa nilikuwa mahali flani hivi nje ya South Afrika kuhudhurua moja ya warsha ambazo kampuni nnayofanyia kazi ina maslahi na warsha hizo. Nikiwa pale kuiwakilisha kampuni, niliteuliwa kuelezea makala iliyoandaliwa na kampuni yetu kwenye warsha hiyo na kama wadau wengine walioshiriki wakiikubali basi husaini mkataba wa makubaliano kibiashara hivyo kufanya kampuni yetu kuingiza hela na mie bonasi yangu ya mwaka inapanda.
Wakati uliwadia nikapanda kwenye kizimba kilichoandaliwa, nikaanza kuelezea na kudadavua kuhusu yote niliyoyataiwa kuyaelezea. Hadhira yote ilikuwa makini kunisikiliza na niligundua wengi walikuwa wananakili notsi. Baada ya kumaliza kuelezea makala hayo maswali na maoni yakaanza nakwambia hadi muda niliopangiwa ukapita kwasababu kulikuwa na kampuni nyingine ambazo nazo zilikuwa zinamakala ya kuelezea.
Nilipomaliza na kushuka kizimbani nilipiigiwa makofi na hadhira nzima tena kwanguvu.... hadi nikaona aibu nikawa narudi kwenye kiti changu huku natabasamu. Muda wa mchana ulipofika, kwenye mlo wa mchana wengi walifika kunisalimia na kuomba kadi yenye taarifa zangu (business card) wengi wao wakiwa wanaume. Wakati napata maakuli kijana mmoja alinifata mezani na kuomba jioni baada ya warsha tukae tuongee. Kwakuwa ilikuwa warsha ya kikazi nikakubali maana nikifanikiwa kufunga dili la kibiashara kwa ajili ya kampuni basi na mie mgawo wangu wa bonasi unakuwa mkubwa.
Jioni ya siku hiyo, nikajipara tayari kuongea na mdau, basi blaah blaah zikaanza mara mkaka akaanza kufunguka. Unajua Kasie, wakati uaelezea makala ya kampuni yenu sikuwa nasikiliza kitu wala kuelewa zaidi ya kubembelezwa na sauti yako....
Nikatabasamu na kuishia kucheka... Kaka akafunguka zaidi, kasie sauti yako matata, tamu, sikivu,......mwisho maongezi yakahama kabisaaa na kuelemea mrengo wa kushoto hheheheheee Kasie ni shiiideeerrr....... Huyo kijana alikuwa ni muafrika ila raia wa Ufaransa....
Basi baada ya warsha kuisha kila mtu akarudi eneo lake lazi, na hadi leo huyu kaka tunawasiliana vyema tu..... kimeishia hapo hehehehheeee......
Kilichonifanya niulete huu uzi hapa, nilijiuliza sana... hivi sauti ya mtu inaweza mfanya mwanaume au mwanamke amdondokee kimapenzi mwanamke / mwanaume...??
Halafu kuna ile, uko mahali unasikia sauti ya mtu bila kumuona, kiasi kwamba anakupa shauku ya kutaka kumuona na kutaka kujua mwenye hiyo sauti anafananaje wakati huo ushajenga taswira yako kichwani...
Nakumbuka hii ilishanitokea nikiwa kidato cha tano, siku hiyo nikatumwa kwenda darasa la kidato cha sita kumuita mwalimu wa darasa. Nikiwa nje ya darasa (mlango umefungwa) nikawa nasikia sauti tamu ya kijana akielezea kitu ubaoni, kumbe alikuwa ana present looh ile kuingia darasani basi daaahh ...... acha tu.....
Alamsiki japo wengine ndo tumeamka.
Basi sawa, Stara Thomas namjua vizuri tu.Unaijua au ulishawahi kuisikia sauti ya Stara Thomas?? kama ulishawahi kuisikia, basi sauti ya Kasie iko hivohivo,kama hujawahi kuisikia sauti ya Bi Stara, basi itafute, gugo wimbo wowote wa Stara uusikilize hapo utakuwa umepata sauti ya Kasie mubashara.
Bravo!!!GENERAL RULE: "A man will say anything just to get in your pants."
HOWEVER: "There are always exceptions to the general rule."
Akili kumkichwa...
Ah....hpo ndio nnapowapendea wanawake awe na miaka 18 ama 30 akili zao znafanana yaani hyu kusifiwa tu keshaamini km kweli sauti yke imemvuruga jamaa hakuna cha sauti wala nn jamaa keshakujengea picha kichwani anataka kidoti hcho ndio tabia zetu kiumeni mtoto wa kike ukimsifia lazma avurugwe c mmeona hyu hadi kaja anzisha uzi hp!

Alitembea vizuri sana, kumbe alifananisha hadi sauti yako na ya stara??Unaijua au ulishawahi kuisikia sauti ya Stara Thomas?? kama ulishawahi kuisikia, basi sauti ya Kasie iko hivohivo,kama hujawahi kuisikia sauti ya Bi Stara, basi itafute, gugo wimbo wowote wa Stara uusikilize hapo utakuwa umepata sauti ya Kasie mubashara.
Haya wenye sauti zenu mpite hapa!!Ha Ha Ha a a a....Kwa sauti gani Bibi wewe alikua anataka aonje asali yako tu hakuna lolo
ote
Acha kunywa bia na wewe uwatetemesheehongera kwa sauti nzuri huo ndiyo ukike sasa
