Sauti ya KIGOGO katika Space ya Maria Sarungi ina lafudhi ya Iringa to Mbeya

kifupi kirefu

JF-Expert Member
Oct 29, 2018
539
3,507
Ni muda mrefu watu wamekuwa wakijadili kuhusu kiumbe asiyefahamoka anayejiita shemasi au Kigogo. Wengi walidai ni kundi la kina nape, Makamba nk na kwamba siyo mtu mmoja. Ila Sasa nadhani ameamua kujitokeza adharani kupitia sauti. Kitendo Cha yeye kuchangia mada kwenye SPACE kupitia sauti halisi kimeondoa utata uliokuwepo na Sasa ni huyu ni Mtanzania anayekerwa na namna serikali inavyoendeshwa.

Lakini pia ni mtu mwenye uelewa mkubwa kulingana na mchango wake kwenye hoja, ni muda Sasa wa serikali kuacha kutumia fedha kumtafuta mtu ambaye kumbe ni Mtanzania na maleengo yake yapo wazi kwamba nimkosoaji wa mambo ya ovyo.

Chakufanya nikujitahidi iwezekanavyo kuchukua positive comments zake na kupuuza negative comments zake.

Anaongea lafudhi ya Chalamila😀😀


 
Ile sauti inafanana na jamaa ambaye nadhani bado anaishi UK. Ni mtu wa Kaskazini lakini alikulia Dar!!

Lakini sidhani kama ndiyo Kigogo mwenyewe! Hivi kwanini Kigogo2014 ameweka bendera ya Kenya kwenye profile yake?
 
Baadhi ya taarifa anazotoa haiwezekani akawa ni mtu mmoja, hakuna cha udukuzi, hakuna cha ujuaji ila ni watu wengi walio na source ndani ya mfumo.

Kama kuna mtu amesikika akichangia mijadala huko pengine ni mmoja wa vigogo tu.
 
Back
Top Bottom