Hongera Maria Sarungi, mmeanza vyema kupata wajumbe wa Kamati ya Katiba lakini nadhani mmekosea fanyeni maboresho

Beatrice Kamugisha

JF-Expert Member
May 18, 2019
757
1,000
Awali nilipokuwa naangalia ujio wa SPACE kama njia ya kufanya bunge la wananchi sikuona Kwa upana ukubwa wa forum Hii. Nikiri Kwamba Maria Sarungi ni Moja ya mtu aliyenufaika kiubunifu na utawala wa awamu ya Tano. Alipofungiwa online TV yake hakukata tamaa alifanya research ni namna gani atakwenda hewani bila kuomba leseni TCRA Wala mamlaka ya Serikali.

Finally akaja na space na nikiri Kwa watu wanaopenda kujifunza na ambao siasa za vyama siyo priority ukiingia space kupitia YouTube au tweeter na kusikiliza utagundua kwamba wapo Watanzania wenye maono makubwa na kwao Madaraka siyo kipaombele Bali wanahitaji Uhuru wa kujadiliana. Utabaini akili timamu nyingi hazipo serikalini zipo sekta binafsi, utabaini watu wanaomwamini MUNGU na wanaoishi MUNGU apendavyo siyo viongozi wala watawala bali watu wanaopata vipato vidogo vya haki kupitia akili, maarifa na ubunifu waliopewa na mwenyenzi MUNGU

Nirudi kwenye mchakato wa Sasa wa Kupata rasimu ya Katiba unaoendelea kwa Sasa. Nimeona Kwa awali wamepatika au kupigiwa Kuru watu 73, well and good. Waliopigiwa Kura wote Wana sifa ya kusaidia maoni na kujitolea lengo litimie. Ila niombe mfanye maboresho yafuatayo

1. Naomba mpate wawakilishi wa vyama vya siasa vinavyoamini kwenye katiba Mpya, Kila chama kitoe mjumbe mmoja. Vipo vyama kama CcM from the very beginning wao katiba Mpya siyo àgenda na hivyo tusijidanganye kwamba memba kutoka ccm atawakilisha msimamo wa chama bila chama kuridhia. Chagueni watu ambao wanakiri kwa dhati kwamba Tanzania inahitaji katiba Mpya. Naelewa hizo ni kura lakini kumbukeni na simamieni vigezo mlivyotoa,Mmesema atakayepigiwa kura awe ni yule ambaye anaamini nchi inahitaji Katiba Mpya. Jielize ni lini Nape, Kagasheki, na wengine wa aina hii wamewahi kutoka adharani wakasema wanahitaji katiba Mpya? Kwa kifupi watu Hawa ni vigumu kuwa wajumbe wa mchakato huu Kwa sababu pamoja na mawazo na misimamo Yao kuhusu katiba Bado wanaamini msimamo wa chama kuliko maslahi ya Taifa. Watu wa aina hii hata Chadema na ACT wapo,wao wanasikiliza mwenyekiti anasema Nini kitu ambacho kwenye katiba ya nchi uwezi kuwatumia watu wa aina hii lazima watakukwamisha Kwa sababu wataleta maoni ya katiba ya chama yawe maoni ya nchi

2. Mkitekeleza hoja ya kwanza mtakuwa tayari mmeondoa wana Chadema kwenye hiyo timu. Siyo afya na napinga chadema kuwa na wawakilishi wengi, awepo mmoja na siyo lazima atoke kwenye top ranks wa chama.

3. Tuwe na mwakilishi mmoja kutoka TLS kama wanaamini Katiba Mpya, LHRC na mashirika mengine yanayotetea haki za makundi Mbalimbali yanayoamini kwamba tunahitaji katiba Mpya

4. Tuwe na wawakilishi wawili mmoja mwanaume na mmoja mwanamke wanaowakilisha wazee

5. Tuwe na mwakilishi wa makundi maalulumu ,

6. Tuwe na mwakilishi wa viongozi wastaafu wakitaifa.

7. Mwakilishi wa vijana, wanahabari, diaspora wanaoamini tunataka katiba na wanaharakati mmojammoja kill kundi

8. Mwakilishi wa Kila Dini,

9. Wawakilishi wawe kutoka pande zote za Muungano.

10. Tuweke nafasi ya wajumbe waalikwa ambao watakuwa watu Wanaotoka kwenye katiba strong na jukumu lao nikushare expirience kuhusu operationalization za katiba kwao.wanaweza kuwa Watanzania au wageni.

Mkitumia makundi haya na mwengine kuomba kura itawasaidi zaidi kwamba kwenye kila kundi atakayepata kura nyingi ndiye anakuwa mwakilishi wa kundi husika.

Then hii kamati au timu kwenye kukusanya maoni ndipo sasa itakwenda kila kona ya nchi kukusanya maoni, haitabagua Wana CCM wala chadema wala wakiristo wala waislam Wala watoto Wala wazee itakusanya maoni ya wote wanaotaka na wasiotaka. Hapa naamini hata wanaccm watatoa maoni badala yakiwaweka kwenye uongozi ukiamini umepata ushiriki wao kumbe umeweka jina tu lisilo na kazi kwa sababu hakuna mwenye utashi wakusaliti msimamo wa chama na kubeba msimamo binafsi wakitaifa.

Kuhusu sekretariet pia mnatakiwa kupata watu huru watakaofanya desk revieq na kuchakata maoni bila biasness.

Naamini kwa mchango huu mtakuwa mmepata jipya lakuongoze na kupunguza. Hii rasimu ni muhimu sana

Next time nitakuja na maoni yangu kuhusu maeneo nyeti ya katiba yanayohitaji uangalizi mkubwa.
 
Bulesi

Platinum Member
May 14, 2008
12,534
2,000
Mnataka tuanze upya ili hali nchi ilishatumia fedha chungu nzima kupata maoni ya wananchi mpaka tukafikia karibu na mwisho mkafanya uhuni wenu!!! Rasimu ya katiba ya Warioba ipo na hiyo ichukuliwe na hapo ndio tuanzie kazi iliyokuwa imebaki na hiyo imalizwe ili tupate katika mpya!!

Hoja ya kuwa referéndum haiwezi kufanyika kwasababu ya corona ni hoja MFU kwasababu tutangoja hiyo corona itakwisha mwaka gani? Watu wataishi na ugonjwa wa corona kama mafua mengine na hata huko ulaya Hivi sasa wamesalimu amri kuwa chanjo zao hazitibu hizo variants za hiyo corona hivyo Maisha yetu yaendelee kama kawaida tufanye REFERUNDUM tupate katiba mpya!!!

CCM hawataki katiba Mpya kwasababu hawapendi Nchi hii iendelee hivyo watajaribu kila Njia ili ile Rasimu ya Warioba isitumike kupata katiba mpya!! Hilo jopo walilounda eti kushauri juu ya kuipata katiba Mpya imejaa ccm sympathizers toka huyo Mwenyekiti wao MUKANDARA ambaye ni surrogate wa Kikwete na wengine wengi ambo Kiukweli wamo humo kwa ajiri ya posho tu, hivyo Sidhani kama wataleta mapendekezo yatakayofanikisha kupata katiba wananchi waipendayo!! Kisingizio kwamba hatuwezi kufanya referundum kwasababu ya corona ni upuuzi tu kwani sasa hivi huo ugonjwa umetambulika Kuwa Kama mafua tu hata hizo chanjo zao hazizuii tena!!! Kwahiyo tuendelee na Rasimu ya Warioba pale tulipoishia.

PLEASE DO NOT WASTE OUR RESOURCES DOING AN EXERCISE THAT HAS ALREADY BEEN DONE
 
Kibingu

JF-Expert Member
Jan 6, 2022
1,031
2,000
Uchaguzi wa skipa wa bunge utaionyesha mawazo ya wana-CCM kuelekea kuipata au kuikosa katiba mpya na/au tume huru ya uchaguzi.
 
jebs2002

JF-Expert Member
Sep 3, 2008
7,987
2,000
Awali nilipokuwa naangalia ujio wa SPACE kama njia ya kufanya bunge la wananchi sikuona Kwa upana ukubwa wa forum Hii. Nikiri Kwamba Maria Sarungi ni Moja ya mtu aliyenufaika kiubunifu na utawala wa awamu ya Tano...
Aise kwa yanayoendelea ya Chief Hangaya na Mzee wa Msoga yanatia hasira, aibu, umaskini na ufukara.

Kwa mara ya kwanza nakubali. Tunahitaji KATIBA mpya. Tena leo leo.
 
Behaviourist

JF-Expert Member
Apr 8, 2016
38,048
2,000
Utabaini akili timamu nyingi hazipo serikalini zipo sekta binafsi, utabaini watu wanaomwamini MUNGU na wanaoishi MUNGU apendavyo siyo viongozi wala watawala bali watu wanaopata vipato vidogo vya haki kupitia akili, maarifa na ubunifu waliopewa na mwenyenzi MUNGU
Rafiki yangu Beatrice ngoja nikuonyeshe akili zilizopo serikalini🤡🤡🤡
 
mbarika

JF-Expert Member
Apr 1, 2015
3,457
2,000
Aise kwa yanayoendelea ya Chief Hangaya na Mzee wa Msoga yanatia hasira, aibu, umaskini na ufukara.
Kwa mara ya kwanza nakubali. Tunahitaji KATIBA mpya. Tena leo leo…
Kila mbuzi atakula urefu wa kamba yake
 
Bejamini Netanyahu

JF-Expert Member
Aug 7, 2014
60,612
2,000
Mnataka tuanze upya ili hali nchi ilishatumia fedha chungu nzima kupata maoni ya wananchi mpaka tukafikia karibu na mwisho mkafanya uhuni wenu!!! Rasimu ya katiba ya Warioba ipo na hiyo ichukuliwe na hapo ndio tuanzie kazi iliyokuwa imebaki na hiyo imalizwe ili tupate katika mpya!!
Hoja ya kuwa referéndum haiwezi kufanyika kwasababu ya corona ni hoja MFU kwasababu tutangoja hiyo corona itakwisha mwaka gani? Watu wataishi na ugonjwa wa corona kama mafua mengine na hata huko ulaya Hivi sasa wamesalimu amri kuwa chanjo zao hazitibu hizo variants za hiyo zorona hivyo Maisha yetu yaendelee kama kawaida tufanye REFERUNDUM tupate katiba mpya!!!

CCM hawataki katiba Mpya kwasababu hawapendi Nchi hii iendelee hivyo watajaribu kila Njia ili ile Rasimu ya Warioba isitumike kupata katiba mpya!! Hilo jopo walilounda eti kushauri juu ya kuipata katiba Mpya imejaa ccm sympathizers toka huyo Mwenyekiti wao MUKANDARA ambaye ni surrogate wa Kikwete na wengine wengi ambo Kiukweli wamo humo kwa ajiri ya posho tu, hivyo Sidhani kama wataleta mapendekezo yatakayofanikisha kupata katiba wananchi waipendayo!! Kisingizio kwamba hatuwezi kufanya referundum kwasababu ya corona ni upuuzi tu kwani sasa hivi huo ugonjwa umetambulika Kuwa Kama mafua tu hata hizo chanjo sao hazizuii tena!!! Kwahiyo tuendelee na Rasimu ya Warioba pale tulipoishia.

PLEASE DO NOT WASTE OUR RESOURCES DOING AN EXERCISE THAT HAS ALREADY BEEN DONE
CCM wao wanataka madaraka
 
dolevaby

JF-Expert Member
Aug 25, 2013
12,663
2,000
Wanaandika Katiba ya kikundi cha kufa na kuzikana? Au cha SACCOS? Watanzania kwa kujipa umaarufu!! Yaani tayari wameunda timu ya Katiba mpya ya Nchi ya kufikirika.
Wee akili yako umekabidhi kwa shaka hamdu kichwa kiko kitupu hutaelewa
 
Ng'wanamangilingili

JF-Expert Member
Aug 22, 2015
4,240
2,000
Mnataka tuanze upya ili hali nchi ilishatumia fedha chungu nzima kupata maoni ya wananchi mpaka tukafikia karibu na mwisho mkafanya uhuni wenu!!! Rasimu ya katiba ya Warioba ipo na hiyo ichukuliwe na hapo ndio tuanzie kazi iliyokuwa imebaki na hiyo imalizwe ili tupate katika mpya!!
Hoja ya kuwa referéndum haiwezi kufanyika kwasababu ya corona ni hoja MFU kwasababu tutangoja hiyo corona itakwisha mwaka gani? Watu wataishi na ugonjwa wa corona kama mafua mengine na hata huko ulaya Hivi sasa wamesalimu amri kuwa chanjo zao hazitibu hizo variants za hiyo zorona hivyo Maisha yetu yaendelee kama kawaida tufanye REFERUNDUM tupate katiba mpya!!!

CCM hawataki katiba Mpya kwasababu hawapendi Nchi hii iendelee hivyo watajaribu kila Njia ili ile Rasimu ya Warioba isitumike kupata katiba mpya!! Hilo jopo walilounda eti kushauri juu ya kuipata katiba Mpya imejaa ccm sympathizers toka huyo Mwenyekiti wao MUKANDARA ambaye ni surrogate wa Kikwete na wengine wengi ambo Kiukweli wamo humo kwa ajiri ya posho tu, hivyo Sidhani kama wataleta mapendekezo yatakayofanikisha kupata katiba wananchi waipendayo!! Kisingizio kwamba hatuwezi kufanya referundum kwasababu ya corona ni upuuzi tu kwani sasa hivi huo ugonjwa umetambulika Kuwa Kama mafua tu hata hizo chanjo sao hazizuii tena!!! Kwahiyo tuendelee na Rasimu ya Warioba pale tulipoishia.

PLEASE DO NOT WASTE OUR RESOURCES DOING AN EXERCISE THAT HAS ALREADY BEEN DONE

Resources gani wanakupotezea ammmiiiy kwani wameomba posho kutoka mfuko wa walipa kodi?
 
Sir curiosity

Senior Member
Oct 2, 2021
153
250
Upo sawa kwa upana wake....kimsingi isinge pendeza sana.

Kama suala isingeingiliwa na kuzungumzwa kisiasa zaidi kama vyama tanzu wanavyotaka kuweka watu wao... kwa ajili ya maslihi ya vyama vyao.. CCM , CDM wote kila mmoja watavutia kwao.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom