Uchaguzi 2020 Majibu yangu kwa maswali kumi niliyoulizwa,baada ya kutangaza nia ya kugombea ubunge katika jimbo la Morogoro Mjini

Leslie Mbena

JF-Expert Member
Nov 24, 2019
207
677
MAJIBU YANGU KWA MASWALI KUMI NILIYOULIZWA,BAADA YA KUTANGAZA NIA YA KUGOMBEA UBUNGE KATIKA JIMBO LA MOROGORO MJINI.

Leo 11:45am 05/07/2020

Rejea maswali haya na mwisho nitayatolea majibu,moja baada ya lingine,

1. Utatumia njia gani kuifanya hiyo Morogoro Mjini kuwa na Soko kama Kariakoo?

2. Je utaweza kuigeuza Morogoro Mjini kuwe na soko kama Kariakoo kwa muda gani na kwa bajeti gani?

3. Morogoro mjini kuna changamoto kubwa ya maji, je umeweka mikakati gani kuondoa hilo tatizo ikiwa hata Mbunge wa sasa, Abood kashindwa?

4. Huduma za elimu na afya ni changamoto haswa magari ya kubeba wagonjwa na vituo vichache vya afya. Umejipanga vipi kutatua hilo wakati hata Abood kashindwa?

5. Barabara nyingi ni za vumbi una mkakati gani kuboresha barabara hizo kuingia katika mpango wa mitaa yote ya Morogoro Mjini iwe na lami?

6. Je una sera gani kuhusu mazingira yaliyoharibika ya Morogoro kama ukipewa dhamana ya kuwa mbunge wa hapa Morogoro Mjini?

7. Je mipango yako ya kuibadilisha Morogoro inaendana na sera ya uchaguzi ya Chama ya mwaka 2015-20 au unaitoa tu kichwani kwako?

8. Morogoro ni mkoa ambayo ni Big 6 ya kulisha nchi kwa kupitia kilimo. Kwa nini unataka uibadilishe kuwa mji wa wachuuzi tofauti na mipango ya Serikali?

9. Je unafahamu kazi za Mbunge ukiwa kama msomi wa Chuo Kikuu?

10. Je mipango unayopanga ina chanzo cha mapato ya kuiwezesha kuifanya na vyanzo hivyo ni vipi?

-MAJIBU YANGU NI KAMA IFUATAVYO,

1. Nikiri wazi haya ni mawazo yangu toka moyoni mwangu naamini pia sera za kwenye ilani nitakayopewa na chama changu,Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuhusu Morogoro itaniongezea mawazo na namna nzuri zaidi ya kufanya Morogoro iamke na kuwa Jiji la kikazi,kilimo na kibiashara,

Ni wazi kugeuza Morogoro Mjini hub ya biashara ni wazo zuri ... Hadi sasa tayari nina majibu na tayari nimefanya utafiti vipi Morogoro itavutia uwekezaji kwenye kilimo,biashara na Utalii hasa Watalii wakitokea Morogoro Mjini kwenda kutalii katika Milima ya Uluguru, Morning sites,Bahati Camp,Rock Garden,Hifadhi ya akiba Matombo, Mbuga ya Mikumi,na maeneo ya kihistoria kama Kibungo,Kisaki na

2.Tayari nimepata ramani ya wapi soko litakuwa,Open space, kubwa na watu wengi kuingia kama wholesalers na wanunuzi wa jumla.

Naamini Soko kubwa jipya lina vigezo vya kuwa kama Kariakoo lakini halitaweza ku- facilitate hiyo hali,hivyo basi maeneo ya Msamvu hadi Nana nane nitaomba kwa Mh Rais John Magufuli kama ikimpendeza atupe ekari kumi ili tuweze kujenga Soko la mfano katika Afrika Mashariki kwa ajili ya Mazao ya Chakula,Matunda,Mboga mboga,bidhaa za Viwandani,Soko la jumla la Nguo,viatu,Vyandarua,mapazia,Mashuka na mablanketi,

Kuna bandari kavu inajengwa Morogoro Mjini,nitauza wazo ijengwe Kihonda na Nanenane,nitakapoingia bungeni,nitaanza kuuza wazo hilo na kusimamia hilo,Nitasisitiza Bandari kavu sambamba na Soko la mazao ya jumla kama ilivyo Soko la Mahindi Kibaigwa,Nitauza wazo bungeni liwepo soko la mazao yote hasa matunda Morogoro,Chakula na mboga mboga.

3.Kuhusu kero ya Maji,tayari tumepokea bilioni 175.6 kutoka shirika la Maendeleo la Ufaransa kwa ajili ya kutatua changamoto za maji katika Jimbo la Morogoro Mjini na kuwapatia Wananchi maji safi na salama na kuchochea Maendeleo ya kipato cha Mwananchi mmoja mmoja,

Nitasimamia hizo pesa zitumike vyema kurudisha miundo mbinu ya Maji iliyochakaa na kujenga hifadhi nyingine kubwa ya Maji ili kuongeza upatikanaji wa maji utaongezeka katika mji wa Morogoro kutoka mita za ujazo 33,000 kwa siku hadi kufikia mita za ujazo 89, 000 kwa siku baada ya kukamilika kwa mradi.

4.Kuna suala la ku- imvest kwenye maisha ya watu binafsi, kuwekeza kwenye maisha ya watu.Nikiwa kama mtaalam wa Masoko na biashara za kimataifa,nitatoa elimu ya biashara kwa watu wa hali ya chini,ikiwamo ku facilitate,kuwezesha watu waweze kukopa na kurudisha ili kuboresha maisha yao na kutengeneza kipato cha mtu mmoja mmoja kwa kutoa mitaji,

Naamini mbunge wa sasa,Abood kwa miaka kumi amefanya ila hajafanya kwa weledi na ufanisi sawa sawa na miaka kumi aliyokuwa mbunge,Mimi Leslie Oscar Mbena naleta mawazo na maono mapya,Miaka kumi ya Abood imetosha na maono yake yameishia hapo,

Nitawekeza kwenye mifuko ya mikopo kuwapa watu m Iitaji Vijana na akina Mama.I can still do my way, Nitakuwa nakutana na wananchi mtaanj wenye biashara ndogondogo na kubadilishana mawazo,

Kuangalia wapi kuna changamoto,je wanunuzi au bidhaa,je ni mtaji duni?je ni hitaji au usambazaji,je ni miundo mbinu inayosababisha soko la bidhaa kudorora,yote tutatembeleana na kutatua matatizo,

5.Nitaingia kwenye maisha ya elimu za watoto na vijana ikiwamo kuhamasisha elimu, kuwatafutia mahitaji nk.Nitatumia taasisi za kimataifa kuomba misaada kwa ajili ya Elimu,

Nitatengeneza international scholarships programs ambazo ziko nyingi online,nitaomba Vijana watakaofaulu na kupenda kwenda kusoma Ulaya na Marekani,nitasaidia kupatikana kwa ufadhili wa masomo nje ya nchi.

6.Zipo changamoto ya barabara za pembezoni kama Lukobe, Mkundi, Tungi, Mzinga na Kauzeni ambazo zinahitaji mtu mwenye maono ya dhati ya Maendeleo kupigia debe bungeni hadi miundo mbinu hiyo ipatiwe fungu la ujenzi,

7.Nitahamasisha vijana kujiajiri hasa biashara ndogondogo kupitia mikopo nitakayowapa,

8.Sambamba na kuhamasisha utunzaji wa Mazingira katika Milima ya Uluguru,ambapo ni sehemu ya vyanzo vya Maji kwa Mkoa wa Morogoro na Dar es Salaam,

Nitaitangaza Morogoro kwa vivutio hii sio option but part of my life,nimeitangaza Morogoro kila nilipokuwa kila niliposoma kila nilipoishi,Upo utalii mkubwa sana matombo, bahati camp, Rock garden,

Nitaandaa matamasha na youth parties na zinakuwa broadcasted kwenye social medias,nitafanya Mpango part hizo ziwe zinarushwa kwenye mitandao ya Kijamii,Instagram,Jamii forum,si kwa anasa bali kutangaza Vivutio lukuki vinavyopatikana katika Jimbo la Morogoro Mjini.

9.Nitahamanisha frelance journalism,kila atakayepiga picha nzuri au video nzuri akiwa mbugani ama katika Milima ya Uluguru,nitamlipa.Yeyote atakayeandika historia nzuri ya Morogoro toka enzi za akina Mbaraka Mwishehe na Moro Jazz na Cuban Marimba hadi Afande Sele na Ghetto Boys nae nitamlipa,

Watu waitangaze Morogoro kwa matukio ya kila siku na mambo mazuri ili ivutie,kupitia Mimi nataka Morogoro iamke usingizi iwe sehemu ya fursa ya Kiuchumi na kiuwekezaji,kupitia Mimi nataka Morogoro ionekane kama London.

Kuna dhana ya waandishi waliopo siku hizi wanaandika mambo machafu tu ama yale wanayoyataka waajiri wao.Lakini kwa Sasa vijana can use their own smartphones,Vijana wanaweza kutumia simu zao kujipiga picha na kujichukua video wakiwa katika Utalii wa ndani,kupiga picha na kufanya freelance journalism kama ajira binafsi nami nitawalipa wakipiga picha nzuri zitakazotangaza Mkoa wa Morogoro.

10.Nitaunda shirika la vijana la kuendeleza Morogoro ambapo vijana watatoa maoni na kutafuta namna ya kufanya Morogoro ishine kama miji mingine,mfano Arusha,Dar,Mwanza na Dodoma.

11.Nitashirikiana na halmashauri kuhamasisha usafi mjini hata kwa kusimamia volunteering ya usafi hata once a month,Mara moja kwa mwezi tutafanya usafi ili Morogoro iwe safi kama Mji wa Moshi,Mkoani Kilimanjaro.

12.Nimalizie na burudani ya mpira na muziki,Wakazi wa Morogoro kwa asili ni wapenzi sana wa burudani haswa muziki na soka. Kulikuwa na timu ya mji maarufu Reli kiboko ya vigogo hii ilikuwa daraja la kwanza ambayo ni ligi kuu ya siku hizi,

Alikuwa akija Simba au Yanga hatoki,anapigwa mbili bila au tatu moja,Walikuwepo wafadhili kama Adolph Ghikas na Mh Oscar Mloka aliyekuwa Mbunge wa Morogoro 2000 2005,walikuwa wanasafiri Mbeya,Iringa,Arusha kuiangalia timu ya Reli ikicheza,

Hiyo Reli naizugumzia ya kina Duncan Butinini, David Mihambo, Fikiri Magoso, Mohamed Mtono hapo kuna mshangiliaji maarufu sana kuwahi kutokea katika Soka hapa Tanzania,aliitwa "Ya Mungu" ambae ndio shabiki wa kwanza Mtanzania kujichora mwilini.

Licha ya Reli mtaani kulikuwa na team nyingi sana za mchangani kama chama langu Jamaica, kulikuwa na Black Viba, Small boys, Zaragoza baadae ikawa Moro United, Uruguay, Paraguay, Burkina Fasso, Rhino nk mtaani ilikuwa ni hatari.

Kwenye muziki Moro ina historia ndefu kidogo siwezi kuzungumzia enzi za kina Mbaraka Mwishehe kwa kuwa sikuwepo mimi nilikuwepo enzi za shimoni Morogoro Hotel na Rock Garden na maonyesho ya Forest Hill.

Hapa kuna mtu anaitwa DJ Sweet Coffee alikuwa pale mtaa wa Konga,Alikuwepo Mtoto mwingine wa Morogoro Dj John Dilinga enzi hizo akiitwa John Mkimbizi sababu baba yake alikuwa mkimbizi kambi ya Solomon Mahlangu lakini Mama yake ni Mluguru wa Matombo.

Disco lilikuwa linapigwa shimoni na mara nyingi alikuwa anakuja DJ Joseph Kusaga akimfundisha kazi DJ Peter Moe.Hii ndio Morogoro iliyofanya kila Mfanyakazi wa Serikali kuomba uhamisho akafanye kazi Mjini Morogoro,

Hii ndio Morogoro ambayo ilizileta bendi zote za muziki kutoka Afrika ya Mashariki kuja Morogoro kushindana na bendi ya Mbaraka Mwishehe na Juma Kilaza,Cuban Marimba na Moro Jazz,Hii ndio Morogoro ninayotaja kuirudisha nikipata ridhaa ya kuhudumu kama Mbunge wa Morogoro Mjini Mwaka 2020-2025.

Nikiishia hapa,Mimi ni
Leslie Oscar Mbena,
Morogoro Mjini.
0755078854.

-Bachelor of Business Administration in International Business.
-Master's in Leadership and Management.

-Research; Assessing Effects of Micro-Financing on Poverty Reduction.
 
Nimeyapenda hayo maswali, kumbe inakuwa hivi kila uchaguzi au?

Inanikumbusha ujuzi wangu kwenye mengi..
 
Haya msalimie mama yake John mkimbizi aka mama mzungu hpo manzese ukimkosa hpo manzese basi Atakuwa shambani kwake magole....
Any way ww utakuwa umechungulia Yawezekana umesiikia abood hato gombea round hii ili apumzike
Tupa tu karata yako

Ova
 
Magufuli AMESHINDWA kuwapa walimu laptop zao, 50m Kila Kijiji.

Wewe hizo ahadi zote utazitekeleza na majibu yako hayo TU??, Anyway nikutakie mafanikio na uwakumbuke watakaokuchagua.
 
Hakuna mbunge mkweli hata mmoja
Tz inahitaji kutawaliwa na mkoloni/mzungu kwa mara ya pili
Hatujitambui Hatujielewi
Kutia nia ni mradi ni biashara
Hakuna mwenye uchungu na WaTz
 
Hakuna mbunge mkweli hata mmoja
Tz inahitaji kutawaliwa na mkoloni/mzungu kwa mara ya pili
Hatujitambui Hatujielewi
Kutia nia ni mradi ni biashara
Hakuna mwenye uchungu na WaTz
Hii ya kutawaliwa na Mkoloni naunga mkono hoja.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom