Mjanga
JF-Expert Member
- Feb 13, 2011
- 1,238
- 325
Asalam aleikum, ni majira ya kuelekea kufunga mwaka 2012 na kuingia 2013;Happy new year to all!
Mwisho wa mwaka huu tunashuhudia mambo mazito ya kutia simanzi na majonzi mazito, katika yote linalovutia hisia za watu duniani ni hiki kifo cha mwanafunzi wa Udaktari aliyebakwa huko India, angalau wahindi wenzake wamepaza sauti na kuonessha ni jinsi gani wamechukizwa na tendo hilo huku moja ya bango likisomeka "REAL MEN NEVER RAPE"! na nyingine: "DEHLI IS THE HQ of RAPE" hii ni baada ya mtu mmoja tu kuwa mhanga! angalau dunia yote imeonesha masikitiko yake juu ya huyu dada: maswali mengi yanaibuka; je watu wanasikitika kwasababu victim alikuwa ni Daktari mtarajiwa, au kweli watu wameguswa?
Hoja yangu ya msingi ni: vipi waafrika Wanawake na Mabinti wanaobakwa kila kukicha, hata hapa kwetu tunaona kwenye magazeti; wale wanaobakwa huko Congo DRC; wale wanaobakwa huko Sudan na kwingineko? Jamii zetu za kiafrika wamefanya nini kuiambia dunia kwamba hatufurahishwi na jambo hili, wanaSIASA wetu wamefanya nini kuondoa hili tatizo, wahasi(wanaojiita wakombozi) na wadai haki wamefanya nini juu ya hili? Au kwa sababu ni wanawake wa mashambani wasio na thamani hivyo ni haki yao kubakwa??? Serikali zetu zinafanya nini?? au kwa kuwa ni Afrika kila kitu tunamwachia Mungu??
manake tunapojaribu kukemea matatizo kama rushwa, ufisadi na matumizi mabaya ya ofisi: utawasikia viongozi wa kisiasa na wa kidini wakiandaa mikesha ya kuiombea taifa: hivi matatizo yetu yatatatuliwa na sala pekee??
Sauti ya Wanawake wa kiafrika wanaobakwa kila kukicha itapazwa na nani na lini????