Sauti Kutoka Khartoum

Mkandara Unachotaka Kusema Ni Kwamba Siku Hizi Hakuna Kuaminiana Katika Suala La Maliasili Na Nishati Zingine Adimu Duniani Kila Taifa Linataka Nishati Hiyo Hiyo .

Ina Maana Sudan Haina Wataalamu Kama Kwentu
 
Nachotaka kusema ni kwamba nchi zote maskini ni nyasi ambazo fahari wawili hupigana..
Kwa wananchi hakuna mtu wa maana kati yao, sii huyo rais mzalendo Mtawala wala huyo mgeni fahari anayetaka kumiliki zizi..Wote hawa ni wezi wa mali zetu kina Mugabe, Chiluba, Mkapa upande mmoja.
Upande wa Pili pia unakuta madume haya yenye mbegu za kupandikiza kina US, UK, CHINA na kadhalika wote pia nia yao ni kuwa wao madume wa kumiliki chumi zetu.. Hakuna kati yao anaye care kweli maisha ya wananchi sipokuwa wanatumia siasa kututenganisha wananchi wapate kutawala vizuri uchumi wetu.
Vongozi wa nchi zetu maskini wote ni Mafisadi hawatupendi sisi ila umilikaji wa hizo maliasili na hawa wanaokuja na misaada pia hawatupendi macho yao ni hizo hizo mali asili na nishati zetu.... So who you gonna call!..
 
Kuhusu majina na idadi ya Watanzania, niko njiani kuyakusanya halafu nikiyapata ntayaleta ktk mtandao. watu wanaishi maeneo mbalimbali kwa hiyo ntashindwa kuto hiyo orodha. Kwa hawa wanafunzi ni rahisi sababu wanaishi hapa ki uhalali na ``evacuation`` yao ni rahisi sababu wanajulikana ni wapi walipo. Tatizo ni kwamba hapa hawa watanzania hawakuwa na chama chochote kile na hakukuwa na register yeyote ile. Na ntakachokukifanya ni kuorodhesha majina ya watu ambao wangetaka kurudi Tz.

Nitajalibu tena kuulizia njia iliyokuwa ya rahisi(bei poa) ya kurudi Tanzania
Hali ya hatari imetangazwa kuanzia saa 11jioni hii mpaka kesho asubuhi saa 12. Mji ni mtupu kama Bongo inavyokuwa siku ya Jumapili
 
Poleni Ndugu Zanguni Nimeangalia Aljazeera Mambo Si Shwari

Halafu Nnaona Aljazeera Imejikita Zaidi Na Habari Za Lebanon Na Hawa Wanaosema Ni Waarabu Wenzao Wamewatupa Hawana Coverage Kubwa Utadhani Sio Breaking News
 
Je hali inaendeleaje huko Khartoum? Kama kuna watu wanafahamu simu ya Membe basi afahamishwe. Huu ndio uzalendo jamani. Sasa inakuaje tunahoji askari wa Tanzania waliokufa Comoro wakati hawa nao ni watanzania kama wengine? Haijaliki walikwendaje huko lakini walikuwa na haja ya kuongeza kipato kwa familia yao na kwa Taifa kiujumla.Hawa walikuwa ni mashujaa wa aina yake, sababu kama wanamiaka zaidi ya 15, na wakafikilia kuondoka Tz, basi sio mchezo. Enzi hizo kulikuwa na ufinyu sana wa habari za ughaibuni na wapi kwa kupata kazi. huu ni wakati either wa Mwinyi au Nyerere.Kwa hiyo jamani tumesikia SAUTI KUTOKA KHARTUOM basi kila mmoja wetu afanye atakachoweza
 
Mwanakjj..u wapi? ulitetea majeshi ya TZ kwenda Comorro? wapi AU au JK kwa issue ya Sudan? au hadi Sudan waombe msaada?...what diplomacy TZ has reached to assist sudan?..au tusubiri hadi Gov iangushwe?

Back kwa wabongo...its good attempt kuwasaidia baada ya kukwama.

Mkandara mchango wako mkubwa...unahitaji fikra sahihi kuzichambua
 
Poleni Ndugu Zanguni Nimeangalia Aljazeera Mambo Si Shwari

Halafu Nnaona Aljazeera Imejikita Zaidi Na Habari Za Lebanon Na Hawa Wanaosema Ni Waarabu Wenzao Wamewatupa Hawana Coverage Kubwa Utadhani Sio Breaking News
Mtu wa Pwani umecheck aljazeera English or Arabic?..

Siwezi watetea ila naangalia uzoefu wangu tu na Aljazeera English..Aljz English naweza kukubali...as waandishi wao wachache na lazima wawe multilingual...
 
Back
Top Bottom