lidoda
JF-Expert Member
- Apr 27, 2008
- 641
- 574
SAUTI KUTOKA KHARTOUM SUDANI
.
Nilifika hapa Sudani mwaka jana mwezi wa nane, na kama tujuavyo nci hii iko ktk vita ya mda mrefu. Nilikuja kwa sababu mke wangu anafanya kazi UN na ilibidi nije nikae na familia yangu hapa. Tunaishi hapa Khartoum na hali ya hapa kwa mda wote haikuonyesha kabisa kama kuna vita na kama huangalii vyombo vya habari kama BBC,CNN,ALJEZIRA na vinginevyo utadhani kuwa nchi hii inafanyiwa propaganda na nchi za magharibi na kutaka kuchafua jina la Sudani.
Kuna watanzania kama 100 ambao wanaishi hapa hawana passporti na hawana hata nauli ya kurudi nyumbani Tanzania. Hawa hapa wanabaguliwa kwa sababu ni wageni. Walikuja hapa kama mabaharia. Wengine wanasimulia walikuwa wakitupwa ktk Port Sudani na mwishowe wakaja mpaka huku Khartoum, wengine walitokea Egypty nk.
Kuna wengine wamekata hata tamaa na matokeo yake wanakunywa pombe kali na kutumia madawa ya kulevya kusudi tu wasahau ugumu wa maisha. Watu wengi wamekufa na wamezikwa hapa sababu hawana uwezo wa kurudisha maiti nyumbani. Kiufupi hawa walikuwa ni watafutaji kama wengine walioko nchi mbalimbali za Ughaibuni na hapa wengine walikuwa wanatumia kama ni transit ya kwenda Ughaibuni. Kuna hawa mabaharia wamekaa hapa miaka 15 mpaka miaka 30 na wameoa na wana watoto.
Asante, kwa watanzania wanaofanya kazi ktk UN, ambao wanatoa msaada wa hali na mali, wamewasaidi kuwalipia nauli baadhi ya watanzania na wamerudi nyumbani. Lakini mzigo bado ni mkubwa, na msaada bado ni mkubwa unahitajika ambao hawa jamaa wa UN hawataweza kuwasafirisha. Kalibu wote wangetaka kurudi nyumbani lakini hawana hela.
Bahati mbaya hapa Khartoum hakuna ubalozi wa Tanzania na hivyo hakuna msaada wowote unaopatikana kwa matatizo mbalimbali, ijapokuwa Tanzania kuna ubalozi wa Sudani pale DSM. Kulikuwa na ubalozi wa Tanzania hapa Khartoum, lakini sababu ya kisiasa ikabidi ufungwe.
Lakini hali iliokuwa jana ilibadilika kabisa hapa. Kuna kundi ambao wanaitwa lebels(JEM)kutoka Darfur ambao walifika mpaka nje ya Khartoum na kuanza kushambulia sehemu sensitive za usalama. Tuliambiwa tusitoke kuanzia saa 11 jioni jana jumamosi mpaka leo Jumapili asubuhi saa 4. Haijulikani kama mda utaongezwa. Jana tulikuwa tukisikia mizinga na mabomu ya kipigwa huko na hakuna magari yakitembea sababu ya hali ya hatari ambayo imetangazwa. Kutoka ktk eneo la vita mpaka hapa tunapoishi ni umbali kutoka City center Dar mpaka Ubungo.Nafikiri mkiangalia ktk BBC,CNN na Aljezira mtaziona hizo habari.
Wasiwasi mkubwa ni kwa hawa Watanzaia wengine amabao hawana passport na hawana nauli ya kurudi Bongo. Mie na familia yangu tunaweza tukapelekwa nchi zilizo kalibu ya hapa, Misri,au Sudani au Kenya nk.
Kuna mtu yeyote anaweza akajua tunawezaje kuwasaidia hawa ndugu zetu?.Yaani wapate msaada wa kurudi Tanzania moja kwa moja?