SAUT: Wenje ametutelekeza

SAUT: Wenje ametutelekeza

don-oba

JF-Expert Member
Joined
Dec 8, 2011
Posts
1,387
Reaction score
680
Wanafunzi wa chuo kikuu cha Mt. Augustine-Mwanza wamemtupia lawama mbunge wao mh. Wenje kwa kile kinachoelezwa kwamba amewatelekeza.

Ikumbukwe kwamba Mh Wenje wanafunzi wa SAUT ambao idadi yao ni zaidi ya 15000 ndio waliomwezesha kiasi kikubwa kupata ushindi. Pia ni hawa hawa wanafunzi ndio walikesha kwenye vituo kulinda kura zisichakachuliwe.

Chanzo cha kumtupia lawama mbunge wao Wenje ni kutokana na wanafunzi wenzao 215 hadi sasa semister imeisha hawajapata pesa zao za kujikimu kutoka bodi ya mikopo.

Inaelezwa kwamba uzembe mkubwa kutoka uongozi wa chuo na serikali ya wanafunzi SAUTSO inayojipambanua kwamba ni makamanda wapiganaji wameshindwa kufuatilia pesa za wanafunzi hawa kitendo kilichopelekea wawasiliane moja kwa moja na Wenje kupata msaada zaidi.

Lakini hadi sasa si Wenje ambaye amewapa taarifa juu ya hatima yao huku wakidai muda mwingine wakimpigia simu hapokei.Imefikia baadhi yao kuacha chuo, wengine wameanza kujiuza miili yao ili wapate pesa za kujikimu.
 
kwani wenje ni bodi ya mikopo...hapo inatakiwa serikali ya wanafunzi na chuo wasimamie hio kitu sababu iko chini yao na hilo lilikua kosa la chuo wenje hana uwezo wowote wa kubadilisha hio kitu.....kule COET(UDSM) wakati nasoma hapo tushaitisha kunji siku nyingi na hivi uzembe wamefanya chuo mbona kingenuka siku ya pili tu bumu la hao jamaa lingetoka...hapo lazima wahusika ,chuo na serikali ya wanafunzi wakaze kamba ndo mtafanikiwa wala msihamishie matatizo yenu kwa mbunge hana uwezo wowote na kudeal na hio kitu.......nyie wenyewe mnaweza kuunda kamati ikaenda bodi kufatilia.............wakati nasoma coet(telecom 2008) kuna wanafunzi 9 wa civil walidisco lakini kutokana na umoja wetu tuliitisha kunji kuwa wameonewa na tulitumia ugomvi kati ya mkandala na menejiment ya coet kuwarudisha wale washkaji ingawa lecture aliewashika alikataa kuwarudisha lakini VC aliwarudisha na wakarudia mwaka na wengi wao walimaliza na 2nd class bila hivyo tungewakosa......lazima muwe na umoja hilo tatizo ni kubwa la sivyo watu wataacha chuo na acheni kabisa kumlaumu mbunge hahusiki na kitu hio na mkimtumia mbunge magamba watageuza kuwa tatizo la kisiasa na mbunge anataka kujipatia umaarufu mtakosa vyote
 
Umesema ni uzembe wa uongozi wa serikali ya wanafunzi sasa wenje analaumiwa kwa lipi? Yeye alikuwa anatoa msaada wa kulishughulikia suala hili,alaumie kwa lipi
 
Ndiyo tatizo ya title ya "ubunge" Tanzania. Watu hawajui mipaka ya mamlaka ya wabunge ma wajibu wao kitu kinacho pelekea kila tatizo wananchi kudhani inaweza tatuliwa na mbunge. Ndio maana unakuta mtu akikosa ada ya mtoto anaenda kwa mbunge, mtu akitaka pesa za kuanzishia mradi anaenda kwa mbunge, michango ya harusi kwa mbunge, nk. Ila ina sikitisha zaidi pale hata wasomi wa chuo wanapo shindwa kutambua mipaka ya mamlaka ya wabunge wao.
 
Sasa ulitaka wenje ndio awazuie wasifanye ukahaba?! Eti ni akili za mwanachuo hizi?!

Binafsi huwa sikubaliani na mnavyosema kuwa kukosa kwenu mikopo ndiko huleta ukahaba!?

Kuna watu baina yenu wanapata mikopo tena kwa asilimia mia moja lakin bado ni makahaba na wengine wanapewa asilimia 70 na wanasaidia na wadogo zao kiasi katika hizo na bado hata hawauwazi ukahaba!?

Utasemaje juu ya hawa mkuu?
 
Umesema ni uzembe wa uongozi wa serikali ya wanafunzi sasa wenje analaumiwa kwa lipi? Yeye alikuwa anatoa msaada wa kulishughulikia suala hili,alaumie kwa lipi

Hawa ndio wanavyuo wetu mkuu!! Ni janga!!
Hata uwezo kidogo tu wa kupambanua jambo hana! Ni lawama tu!!
 
Hapa ndipo napaga shida na watanzania,tutafika mahali tukinyimwa unyumba tutakwenda kushtaki
kwa wabunge,!!Suala la kuchelewa mikopo haliwezi kuwa ndio sauce ya kufanya ukahaba kuna watu
wanapewa mikopo asilimia mia na kwa wakati na bado wanajiuza, sasa sijui mnataka mbunge aje
kuzuia miguu ya hao wanafunzi wasi.ta.ue?!! au wanaume nao wanajiuza?!!!aaaaagh"
 
Umesema ni uzembe wa uongozi wa serikali ya wanafunzi sasa wenje analaumiwa kwa lipi? Yeye alikuwa anatoa msaada wa kulishughulikia suala hili,alaumie kwa lipi

Hili ni tatizo linalotokana na ukosefu wa mitaala ya elimu inayokidhi mahitaji ya jamii yetu.
 
Kweli madhara ya ukosefu wa mitaala. Na hao wanafunzi wa kiume walokosa mikopo wao wanafanyaje kujikimu? Pia wanafanya ushoga?
 
Kuna ujinga mkubwa sana kwenye vichwa vyetu kuhusu kujua wajibu wetu na kuwajibika kwetu kwenye wajibu huo.
'
Lakini inaonekana hatujui kabisa jukumu la viongozi wetu tunaowachagua na nafasi walizonazo kwenye jamii.
'
Vijana mko chuo mnashindwa kujua namna ya kufuatilia haki zenu mnataka kutumia ushindi wa mbunge wenu ili afanye yale mnayotakiwa myafanye nyie ayafanye yeye!Hii ni ajabu na aibu!
'
Kama nyie mlioko chuo mnashindwa kujua wajibu wenu na mnaenda kujiuza je wale walioko mitaani wafanye nini?
 
kwamba nyie ndo mlilinda au mlioababisha Wenje ashinde mi naona ni uongo,kwa sababu kwa kipindi kile unafanyika uchaguzi kwa hawa waliopo third year ndo walikuwa first year, na ninavojua mwaka 2010 vyuo vingi vilichelewa kufungua sababu ya uchaguzi,na sababu ya ugeni na kuhangaika na mambo ya malazi mara registration sidhani kama mlikuwa na muda wa kulinda kura,pia sidhani kama hata hizo kura mlipiga sababu mlijiandikishia kwenu.
ulichopaswa kusema kuwa Wenje ni just mbunge wenu.Na sifikirii kama hiyo ndio kazi ya Wenje kwa sababu mna loan officer hapo chuo pia mna serikali ya wanafunzi ambao mliwachagua weneywe kwanini hamuwatumii hao mnasubiri wenje? Sidhani kama hiyo ni right strategy
 
Halafu usijustify ukahaba kwa sababu ya ugumu wa maisha unashusha dignity yako je wale wasio na advantage ya ukahaba wanasurvive vipi,kama solution ya hayo matatizo ni ukahaba sidhani kama mnafaa kuaminika kama wasomi,labda nikuombe uthibitishe tena kwa kauli yako maneno haya "SAUT MNAFANYA UKAHABA SABABU YA UKATA"
 
Hawa ndio wanavyuo wetu mkuu!! Ni janga!!
Hata uwezo kidogo tu wa kupambanua jambo hana! Ni lawama tu!!

Moja ya ahadi zake Wenje pindi alipokua akigombea ni kwamba pindi atakapoingia bungeni suala la ucheleweshwaji wa mikopo kwa wanafunzi wa SAUT litakuwa ndoto. Pia aliahidi kuwa karibu na wanafunzi kwa jambo lolote pale watakapomhitaji.
 
Wenje usipokee simu zao.

wanafunzi wa SAUT ni wajinga kweli.
Hebu jiuzeni tu,hata nyie wanaume mjiuze ili muwasaidie
wadada hela za kujikimu.

Yaani nyie hamjuagi kudai hela zenu,mnakalisha makalio chuni tu mnasubiri
wengine wapige kunji na nyie mfaidike. nyambafu zenu,JIUZENI,HAMJAANZA JANA WALA LEO.

Wenje usipokee simu,utakufa njaa,jenga tumbo lako jaduong'
 
kwani wenje ni bodi ya mikopo...hapo inatakiwa serikali ya wanafunzi na chuo wasimamie hio kitu sababu iko chini yao na hilo lilikua kosa la chuo wenje hana uwezo wowote wa kubadilisha hio kitu.....kule COET(UDSM) wakati nasoma hapo tushaitisha kunji siku nyingi na hivi uzembe wamefanya chuo mbona kingenuka siku ya pili tu bumu la hao jamaa lingetoka...hapo lazima wahusika ,chuo na serikali ya wanafunzi wakaze kamba ndo mtafanikiwa wala msihamishie matatizo yenu kwa mbunge hana uwezo wowote na kudeal na hio kitu.......nyie wenyewe mnaweza kuunda kamati ikaenda bodi kufatilia.............wakati nasoma coet(telecom 2008) kuna wanafunzi 9 wa civil walidisco lakini kutokana na umoja wetu tuliitisha kunji kuwa wameonewa na tulitumia ugomvi kati ya mkandala na menejiment ya coet kuwarudisha wale washkaji ingawa lecture aliewashika alikataa kuwarudisha lakini VC aliwarudisha na wakarudia mwaka na wengi wao walimaliza na 2nd class bila hivyo tungewakosa......lazima muwe na umoja hilo tatizo ni kubwa la sivyo watu wataacha chuo na acheni kabisa kumlaumu mbunge hahusiki na kitu hio na mkimtumia mbunge magamba watageuza kuwa tatizo la kisiasa na mbunge anataka kujipatia umaarufu mtakosa vyote

mkuu, ni kweli sio jukumu la mbunge ila nafasi yake ni kubwa aki-push hoja yake ni tofauti na mwanafunzi. Pia ndiye aliyewaahidi wanafunzi kwamba atakuwa karibu nao na akawahakikishia suala la ucheleweshwaji wa mikopo litakuwa ndoto.
 
Wenje si kazi yake. Acheni ujinga

kazi yake ninini?, wanafunzi kutoka jimboni kwake wamepata matatizo yeye yuko karibu na serikali, achukue hoja zao aziwakilishe panapohusika. Linapokuja swala la kamanda mwenzetu kuzembea tusimtetee.
 
Kwani wenje aliwaahidi kwamba atahakikisha mnapata mikopo au vipi? sababu nakumbuka hata Jakaya alidai hakuna mwanafunzi atashindwa kwenda chuo kikuu kwa kukosa mikopo, sasa kama watu wanakosa mikopo wenje ataweza kuleta mabadiriko gani?

Alafu inakuwaje mnataka kumlalamikia wenye huku mnajua namna viongozi na wabunge wa CHADEMA wanavyopigwa vita serikalini na Bungeni? au mnataka kumtoa machozi?

Nyie hamjatelekezwa na wenje, ila mmejitekeleza wenyewe.
 
Yaani mnashindwa kuilalamikia serikali ambayo ndio inahusika mnamlalamikia mtu ambae ni msimamizi wa serikali ila hasikilizwi
 
Back
Top Bottom