KERO Wanafunzi wa SAUT Mwanza hawajapewa pesa za kujikimu mpaka sasa

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Tunaomba Mtufikishie malalamiko haya Ngazi za Juu

Habari wahusika wa Mtandao wangu pendwa wa Jamii Forums,

Kuna shida Mwanza katika Chuo kikuu cha SAUT ambacho ni takribani miezi minne sasa wanafunzi wanaonufaika na HELSB yaani Mikopo ya Elimu ya Juu Hawajapatiwa pesa zao za Kujikimu.

Wengi wao ni Mwaka wa Kwanza yaani First Year wanateseka sana huku hasa Dada zetu, Tunaomba mtufikishie hili na Ukizingatia Tarehe 04.03.2024 wanafunzi hao wataanza Mitihani yao ya Kufunga.

Tusaidieni kupaza Sauti Watoto wetu wapate Boom yaani fedha za kujikimu.

Majibu wanayopewa ni kuwa Akaunti zao zilikosewa, itakuwa zikosewe ilihali baadhi yao walipata Boom la kwanza kupitia Akaunti hizo hizo
 
Ni aibu sana watoto wa kitanzania kuteseka ktk nchi yao ilihali wazazi wao wanalipa Kodi Kila siku. Nyie HESLB wapeni watoto boom lao fasta, ala!
 
Wapigaji wapo kazini.
SIO SAUT TU
HATA VYOU VINGINE KUNA MADUDU.

BILA SHAKA WAHASIBU WA VYUO HUWA WANAMIRADI, WANAZIPELEKA ZILE PESA KWANZA ZIKAZUNGUKE KWENYE MIRADI YAO TJEN NDO WAZILETE CHUO.

FIRST YEAR WAKIWA WAMESHACHOKA NA WADADA WAKIWA WAMESHACHAKATWA VYA KUTOSHA.

UKIONA TATIZO LIMEFIKIA HATUA YA KULETWA JAMIIFORUMS UJUE HILO TATIZO NI KUBWA NA UONGOZI WA CHUO HUSIKA UMEPUUZIA MALALAMIKO YAO.

VYUONI KUNA MADUDU MENGI SANA KWA HAWA WATUMISHI
INABIDI WACHUNGUZWE.
 
Kuna haja ya muongozo mpya kuwa mwaka wa kwanza akifika chuoni tuu aunganishwe na Fingerprint moja kwa moja nakumbuka mimi nilipofika mwaka wa kwanza chuo boom langu la kwanza nililiona mwezi wa 12 mwishoni
 
Muongozo upi tena wakati sasahv nasikia wana Didis ambao ni mfumo mpya unasaini kwa simu yako.
Ila condition uwe maeneo ya chuo ndo unaweza kusaini.

Hii sio kwamba iko vyuo vya daa tu bali ni inchi nzima.
 
Wapigaji wapo kazini.
SIO SAUT TU
HATA VYOU VINGINE KUNA MADUDU.

BILA SHAKA WAHASIBU WA VYUO HUWA WANAMIRADI, WANAZIPELEKA ZILE PESA KWANZA ZIKAZUNGUKE KWENYE MIRADI YAO TJEN NDO WAZILETE CHUO.

FIRST YEAR WAKIWA WAMESHACHOKA NA WADADA WAKIWA WAMESHACHAKATWA VYA KUTOSHA.

UKIONA TATIZO LIMEFIKIA HATUA YA KULETWA JAMIIFORUMS UJUE HILO TATIZO NI KUBWA NA UONGOZI WA CHUO HUSIKA UMEPUUZIA MALALAMIKO YAO.

VYUONI KUNA MADUDU MENGI SANA KWA HAWA WATUMISHI
INABIDI WACHUNGUZWE.
Jamii forum ipaze sauti tuu
 
Harafu kumbuka huu ni mkopo sio pesa za hisani. Hii ndo Tanzania then kuna watu wanazurula na misafara.
 
Mtoa hoja ,wakusanye waathirika wote hapo chuoni na mfanye push back dhidi ya mhusika, mzuieni mhasibu ofisini kwake hadi afanye malipo, humu JF ni kulalama tu,mkifanya hivyo serikali yote hapo mkoani itahamia hapo including ffu ila msitishike,kudai haki kunaandamana na sacrifice kubwa ,kuna wengine wata pay the highest penalty...death..ili wengine wapate haki
 
Matoto ya sasahv ni maoga mkuu.

Yanaogopa kulala lockup.
 
Back
Top Bottom