tangu suala la mikopo lianze tanzania, ni matatizo tu jamani
labda tunapaswa kujua mipaka na majukumu ya mbunge
maana kama hata kufuatilia mikopo itakuwa i jukumu lake
basi tujiandae wanavyuo wachumba au wapenzi wakihitilafiana, ajiandae kupokea kesi
kwa serikali tuliyonayo sasa, no maandamano no kupata haki yako
tafakari chukua hatua
Wanafunzi wengi siku hizi huwa hawapendi kuandamana eti wao ni masharobaro na masharomaro watachafuka na jasho, sasa chagueni moja kuandamana kudai mikopo au mkajiuze. Nimesoma UDSM 2005-2008 hakuna mwaka uliopita hatukuandamana kudai bumu. Eti wao wanataka mbunge aandamane kudai bumu, Huyu Mbunge atashughulikia mambo mangapi jamani?. Serikali ya maccm bila mandamano watu hawafanyi kazi. Sisi tulikuwa tukilianzisha VC ofisini hakukaliki. 2005 Nimrodi mkono aliletwa na Waitara mwita pale Nkuruma tulimchana kufika jioni akaunt zikacheka.
Mimi nadhani wanafunzi wa vyuo tofauti na UD hawakustahili kuwa chuo kikuu, ila tu kwa sababu ya wingi wa vyuo vikuu nchini ndo maana. Hili peke yake linaeleza kuwa ni wananfunzi wa aina gani walioko pale SAUT. Sidhani Wanafunzi wa UD tena FOE (achana na COET ya Juzi) wanahitaji kiongozi wa kisiasa kusolve issue ndogo kama ya mkopo patachimbika aisee!
Wafunzi kama hawa sijui wa SAUTi sijui wa VOICE sidhani hata wanaweza kutusaidia kwenye ukombozi wa pili wa nchi yetu maana wameonyesha ulegevu mkubwa kabisa na inaonyesha wazi ambavyo wanaweza kuwa vigeugeu muda wowote. Leo hii wanailaumu serikali ya magamba lakini wakipewa mkopo tu tayari utawasikia wanaenda hata kwenye vyombo vya habari kutoa tamko la kuishukru serikali ya magamba kwa kusikia kilio chao cha muda mrefu!
SAUT ni nini bwana wanafunzi wa Chuo kikuu walikuwa enzi hizo UD tena pale FOE!
Hakuna siku mtafanikiwa wasomi wa leo kwa kuyafanya matatizo yenu kuwa ya kisiasa....
Masuala kama haya yanahitaji fikra huru na wanafunzi wenye moyo wa kujitoa kwa umoja wa kweli....hamuwezi kufukuzwa chuo wote!
Vijana wa IFM,UDSM na baadhi ya vyuo vya Dar es salaam nawasifu kwa kulijua hili....sijawahi kusikia UDSM wakimtafuta mbunge wao na kumbebesha zigo la matatizo....sikuwaona IFM wakimlaumu mbunge wa kigamboni....sikuwahi kuwaona IMTU wakimlilia mbunge wa Kawe..
SAUT tunaamini nyie nao ni wasomi,mna uwezo wa kuchambua mambo na kudai haki zenu kwa kutumia taaluma zenu....tumieni fursa hiyo...hata Nairobi University huwa hawalii kusaidiwa na mbunge..
Jionesheni tofauti yenu as Academicians against Politicians in problem solving!
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.