Saudi Arabia mbioni kufilisika

Na kumbuka misikiti inayozungumziwa hapa sio msikiti wa Kichangani au Nungwi kule. Wala sio msikiti wa Kazimzumbwi; bali ni "the Two Holy Mosques"; sijui hata kama unaelewa maana yake.[/QUOTE]

Na hiyo misikiti naifahamu vizuri mufti tena nimeshafika mpaka huko
Wao kuwa custodian haimanishi kuwa ndo waislamu swafi.huo ucostodian wamejipa wenyewe.Hyo kaaba yenyewe ishawahi kuwa chini ya waabudu masanamu na masanamu yakawekwa ndani kabla ya mji kutwaliwa na waislamu.
Pili nchi haiwi ya kiislamu kwavile tu watawala wameamua iwe hivyo.Inatakikana iwe inafuata misingi yote ya kiislamu kitu ambacho serikali ya saudia haijatimiza.
Tatu investment portfolio ya Saudi family na nchi ambazo ina uhusiano nazo ni totaly against the interest ya uislamu.Huwezi kuwa kiongozi wa kiislamu alafu marekani ikawa ndo your bigest aly,
 
Sasa hizi ulizotaja hapa mbona ni faida zaidi kuliko hasara? We huoni kama mwanamke hapo anathaminiwa? Kubeba gunia la viazi kariakoo ndo unaona sawa kwa mwanamke, au pale uwanja wa fisi ndio unaona Mungu anapenda??
Kila mtu anamtazamo wake kama ni faida basi sawa mi cna pingamiz nawe
 
S
Wachumi wanasema baada ya miaka mitano hazina ya Saudi Arabia itakuwa imekauka.

Kutokana na kushuka kwa bei ya mafuta, Saudi imekopa dolla billioni 10 kutoka kwenye masoko ya kimataifa wiki hii.Hii ni mara ya kwanza katika miaka 25 iliyopita.

- Kuanzia mwaka jana Saudi imetumia dollar bilioni 100 kutokana kwenye hazina yake.
-Kubalance bajeti bei ya mafuta inatakiwa iwe zaidi ya dollar 100 kwa pipa, kwa sasa pipa moja ni dola 40. Wataalamu wanasema pipa kufika dola 60 tu itakuwa ni muujiza.
-Kwa sababu hiyo Magufulinism ( kubana mtumizi) ya serikali kumeshaanza kodi za petrol n.k

Hii hali ni hatari hapo mbeleni , kuna wasiwasi wa kutokea instability hasa middle east kutokana na ugumu wa maisha kwa sababu ya kushuka kwa bei ya petroli.
Sio saudia tu na Uchina uchumi umeanza kudorora WB wameanza kujadili ili nchi zinazotegemea uchina kwa uchumi zipate nafuu ya maumivu.
 
Iran baadaa ya kuondelewa vikwazo vya kiuchumi yeye anauza mafuta yake kwa bei anayotakaa na ukumbuke nayeye anahazina kubwa ya mafuta....kagoma kujiunga na opec ili waweze kushirikiana kupanga bei ya mafuta sasa hii inamuwia vigumu waarabu wadubai
So hana ujanja inabidii sasa kishusha bei yake kwa pipa coz bithaa imekuwaa nyingi sokoni na technology imekuarahisi...
...Chanzo kinachofahamika rasmi cha kushuka kwa bei ya mafuta, ni Marekani kuanza kuzalisha shale oil kwa wingi. Baada ya kuona hivyo, Saudia akaongeza uzalishaji ili bei ishuke zaidi na kuua uzalishaji wa shale oil Marekani.

...Saudia amefanikiwa kuua uzalishaji wa shale oil, kwasasa. Makampuni mengi yana mikopo na yameshindwa kulipa, mengine yanafilisika. Production ya shale oil ime drop, ila new entrant, Iran, anajaza nafasi.
 
Mimi ninachojua mwarabu alikubali kushusha bei ili kumkomka mrusi na kumsikiliza mmarekani kwenye vikwazo vyao, sasa mrusi kaumia sana lakini hata wao kumbe wanaumia. Sasa sijui hiyo OPEC wamekubaliana nini na mmarekani kwani anapanga kushusha tu. Huku wanajikaanga wenyewe.
 
Siku za mwanzo za utawala wa Obama aliwaambia live kama wanaleta nyodo na mafuta yao dunia itatafuta alternative source ya nishati au mafuta. Marekani kaanza kujichimbia yake, Norway, Russia, China, n.k. Ya Uganda yataanza kumiminika miaka miwili ijayo kupitia Bandari ya Tanga hivyo soko la ukanda huu wa Mashariki na Kusini mwa Afrika litaachana na mafuta ghali kutoka Middle East.
...Labda alikuwa hajaisoma game vizuri, au his talk was meant to a different audience.

...Refineries zilipo ndio zinapelekea kuamua soko na mteja, bila kusahau bei. For a long time, we'll still buy oil products from more or less same sources.

...Saudia, is among the lowest cost producers. Ndio maana ana pump more oil ili awa drive wengine out of business. Shale producers in the US, wanalia na wengine of course.

Kama waliendekeza starehe wakaacha kutumia mapato ya mafuta kuwekeza kwenye brains za watu wao ili wazalishe bidhaa na huduma mbadala na badala yake wakawekeza kwenye dini yao ya taifa kwenye mataifa ya ng'ambo imekula kwao. Dunia imebadilika sana; hivi kwa mfano vile viwanda vya Uswisi vya kutengeneza saa ghali aina ya Oris enzi hizo siku hizi bado vipo? Maana hata hizo saa sijui kama zina soko tena siku hizi baada ya dunia kutawaliwa na digital.

Oris watakuwa walibadili bidhaa zao ili kuendana na mahitaji yanayobadilika kwa kasi ya ajabu kila uchao. Saudia waendelee kukandamiza wanawake na kuwaweka misukule ndani simply wana pesa za mafuta kuna siku watawatafutia wanaume overseas hayo mafuta yatakapokuwa priceless siku sio nyingi zijazo.
...Prince Mohammed anafanya hayo sasa. Kuna post hapo juu, kama hutajali unaweza isoma, ina link ya mambo hayo.

...Its harder to make reforms in Saudia, ila huyo Prince ameanza. Wanahitaji kubadilika.
 
In short siku za waarabu / waajemi kutawala dunia kupitia uchumi wa mafuta unakaribia ukingoni kama si kumalizika kabisa.

Nchi za Ulaya na USA waliwekeza sana katika elimu science & technology wakati nchi za kiarabu zilikuwa busy kupromote ugaidi,kukandamiza haki za wanawake,viongozi kulazimisha kubaki madarakani hadi mauti na wakati mwingine kurisisha uongozi kwa watoto wao.

Mafuta yamegunduliwa sehemu nyingi dunia katika kipindi cha miongo miwili iliyopita Afrika pekee yake nchi za Nigeria zimezidisha uzalishaji wa mafuta hadi 2.2 million barrels kwa siku,Algeria 2.1 barrel kwa siku,Angola 1.9 barrel kwa siku,Libya 1.7 barrels kwa siku,Misri 680,000 kwa siku,Sudan 480,000 barrels kwa siku,Equitorial Guinea 340,000 barrels kwa siku,Congo DRC 270,000 barrel kwa siku,Gabon 240,000 barrels kwa siku. Nchi tatu za Afrika nilizozitaja mwisho mafuta yake hayana miongo miwili tangu yagunduliwe bado kuna Uganda na Kenya very soon wataingia kwenye soko la dunia.Bado nchi za Msumbiji na Tanzania zimegundua gas nyingi ambayo inaweza kutumika kuzalisha umeme,mitambo na hata magari.

Nchi ya Brazil ni nchi ya pili kwa kuzalisha ethanol kwa wingi duniani (nishati mbadala) ya kwanza ni USA.Ethanol inayozalisha Brazil utumika kuzalisha umeme,kuendesha mitambo mbali mbali,matumizi ya magari na tren.........

Dunia ya waarabu / waajemi imefikia ukingoni.
 
Kama technologia itazidi kukua hamna muarab atapata shida kama msaudi kutokana na lifestyle yao.Ngoja na sisi tuanze kuchimba yetu...

...Saudia ni moja ya wazalishaji wenye gharama ndogo kwa pipa, ukizingatia ni mzalishaji mkubwa kabisa. Hii blog post ni very informative kwenye mjadala huu. Nawashauri muisome, mkiwa na nafasi.

...Teknolojia ikikuwa, nani zaidi ya Aramco atakayeweza kuinunua na kuitumia kwa haraka. Pengine, anahusika hata na uendelezaji wa hiyo teknolojia.
 
Akili ya mswahili mbaya sana eti unafurahia Saudia ifilisike ili wote muwe sawa...dah kweli ubinadamu kazi....kwa taarifa yenu Saudia kama akifilisika mtakaoadhirika ni nyie wabongo maana ugaidi utaongezeka na watakuja kubanana hapa hapa bongo na mademu zenu wawagongee
...Dah!
 
S

Sio saudia tu na Uchina uchumi umeanza kudorora WB wameanza kujadili ili nchi zinazotegemea uchina kwa uchumi zipate nafuu ya maumivu.
...Tatizo mChina hataki kukiri na kuweka mambo wazi. Hivi sasa, ana finance growth kwa mikopo. Worse enough, makampuni ya maana kwenye sekta mbalimbali, yana madeni yasiyolipika.

...Wost case scenario, Yuan inaweza anguka.
 
  • Thanks
Reactions: Lab
Saudi wana nyodo sana Mungu anawaadhibu.Ujue katika nchi zote za Khalij ni Saudi pekee wanasheria ya kuchinja watu.??Mwanamke saudi hathaminiwi kabisa mwanaume ndo kila kitu Saudi Arabia.Yani kuna vitu ukisikia unaweza kuhisi kama masihara lakin ni kwel
1.Mwanamke haruhusikii kula ice cream hadharani
2.Mwanamke haruhusiwi kukimbia hadharani hata uwe na haraka vip.
3.Mwanamke haruhusiwi kusalimiana hata na kaka yake wa damu hadharani kwa kushikana mikono au kugusana kwa style yoyote
4.Mwanamke haruhusiwi kudai talaka kama nchi zngne wanawake wanavyopewa kipaumbele.
5.Mwanamke harusiwi kushout hadharani yani upuuz puuz tu
Inahusiana nini na kushuka/kupanda kwa bei ya mafuta?
 
Mkuu nakushauri kwanza ukaipitie historia ya Hijaz(now saudi arabia).unafahamu kwanini ikabidilishwa jina.unaifahamu vizuri Saudi family,Asili yao na historia yao na jinsi walivyoweza kuitawala hyo inchi.Alafu nenda kasome ujue uongozi wa kiislamu unatakiwa uweje.kwa kukusaidia tu zipo nchi nyingi pamoja na majimbo ya nchii.(i.e naigeria) ambazo zina abide by Sheria law lakini sio nchi za kiislamu.
Pia inawezekana nikawa sijui baadhi ya maswala kuhusu hii dini,kwahiyo si vibaya nikadurusu mawili matatu kutoka kwako.

Mkuu unaweza kuwa uko sahihi, ila point ya dudus hapa ni kuwa huwezi kuutofautisha uislamu na Hijaz, kwa kuwa mkuu (His majesty) wa formerly Hijaz ndio mkuu wa Nyumba Kuu za Ibada (The Holy Mosques) za waislamu duniani na ndio maana wote mnasali kuelekea Kule.
So uko sahihi on your perspective, and dudus is also right on his.
 
Mkuu unaweza kuwa uko sahihi, ila point ya dudus hapa ni kuwa huwezi kuutofautisha uislamu na Hijaz, kwa kuwa mkuu (His majesty) wa formerly Hijaz ndio mkuu wa Nyumba Kuu za Ibada (The Holy Mosques) za waislamu duniani na ndio maana wote mnasali kuelekea Kule.
So uko sahihi on your perspective, and dudus is also right on his.
Nmekuelewa mkuu ila sisi tunaelekea kule wakti wa ibada regardless nani anatawala lile eneo.Point yangu kuu ni kuwa the saudi kingdom sio sehemu ya kuitolea mfano kama utawala wa kiislamu.wale ni madhalimu wa kutupwa afadhali hata ya kikwete
 
Saudi wana nyodo sana Mungu anawaadhibu.Ujue katika nchi zote za Khalij ni Saudi pekee wanasheria ya kuchinja watu.??Mwanamke saudi hathaminiwi kabisa mwanaume ndo kila kitu Saudi Arabia.Yani kuna vitu ukisikia unaweza kuhisi kama masihara lakin ni kwel
1.Mwanamke haruhusikii kula ice cream hadharani
2.Mwanamke haruhusiwi kukimbia hadharani hata uwe na haraka vip.
3.Mwanamke haruhusiwi kusalimiana hata na kaka yake wa damu hadharani kwa kushikana mikono au kugusana kwa style yoyote
4.Mwanamke haruhusiwi kudai talaka kama nchi zngne wanawake wanavyopewa kipaumbele.
5.Mwanamke harusiwi kushout hadharani yani upuuz puuz tu
Suala hili la kuporomoka kwa uchumi wa Saudia una uhusiano gani na hizo sheria za saudia....??

Unaonekana una chuki kali sana dhidi ya dini ya kiislamu....??
 
Nmekuelewa mkuu ila sisi tunaelekea kule wakti wa ibada regardless nani anatawala lile eneo.Point yangu kuu ni kuwa the saudi kingdom sio sehemu ya kuitolea mfano kama utawala wa kiislamu.wale ni madhalimu wa kutupwa afadhali hata ya kikwete
Hahahaaa wee jamaa eti afadhali ya kikwete
 
Back
Top Bottom