Sasa rasmi UDART 85% ni hisa za Serikali. Simon Group hoi

Ufanyike utaratibu wa kuiingiza UDART kwenye soko la hisa la DSE ili kiasi fulani cha hisa ziuzwe kwa wananchi na makampuni binafsi ili umiliki wa Serikali wa 85% upungue angalau kufikia 70% au hata chini ya hapo.
 
sijui kwanini watu wanashabikia umiliki wa serikali? Serikali haina historia ya kufanya biashara kwa ufanisi.. Mtakuja kushuhudia siku moja
Kwa hiyo unataka shule, umeme, hospital na huduma za maji ziwe mikononi mwa sekta binafsi, maana nazo ni biashara kama biashara zingine.
 
sijui kwanini watu wanashabikia umiliki wa serikali? Serikali haina historia ya kufanya biashara kwa ufanisi.. Mtakuja kushuhudia siku moja
Hivi unafikiri Huduma za Maji, umeme, afya na elimu zikimilikiwa na sekta binafsi kwa asillimia mia ni Watanzania Wangapi watakaomudu hizo gharama.?
 
Tunarudia makosa ya nyerere,wabongo si watendaji blah blah nyingi ndio waliobugia mashirika ya soma ule (SU) leo twarudi kulekule.Heri angekabidhiwa mbia Wa nje aendeshe atoe huduma bora
Huyo mbia atatoa Huduma kibiashara ila sio kwa manufaa ya jamii, ukiambiwa nauli toka Kimara hadi kariakoo ni 1500 usiilalamikie serikali kwamba imewatelekeza wananchi.!
 
Yule Masaburi aliwapa hisa zote kwa bilioni 2
Baadae serikali ikapewa 51... sasa serikali imechukua hadi kufikia hapo.....

Ni vizuri maana upigaji ulifanyika na jiji kwani jiji ndo walikuwa wanamiliki hizo hisa. Wakaziuza hela zenyewe kamati ilikaataaa zitumia
15% ni za nani?
 
sijui kwanini watu wanashabikia umiliki wa serikali? Serikali haina historia ya kufanya biashara kwa ufanisi.. Mtakuja kushuhudia siku moja
Unajua sababu ya kukosa ufanisi ni viongozi legelege na tukisema tusubiri sekta binafsi ni kupoteza muda wakati tunaweza kufanya kupitia serikali mbona sects binafsi haikuweza kujenga viwanja vya ndege vikubwa tz wala kununua ndege za maana ? Kiongozi atakiwi kucheka na wafanyakazi wa serikali hata siku moja
 
Hivi unafikiri Huduma za Maji, umeme, afya na elimu zikimilikiwa na sekta binafsi kwa asillimia mia ni Watanzania Wangapi watakaomudu hizo gharama.?
Huyo jamaa ni chizi achaneni naye sisi tunataka kodi yetu ifanye mambo ya kujenga nchi na biashara hatuwezi kupoteza muda kusubiri sekta binafsi tena za kifisadi kama IPTL
 
Unaongelea yale Mekundu haya ya Blue sio yao.

Hujui hata Mabasi yalikuwa na Wanajeshi kabla ya Usaili wa juzi wa Madereva?

Yale ya Bandarini 70 yanataifishwa kuwa mali ya serikali baada ya kushindwa kulipa kodi?
Sio yote!, labda some. Kisena ni mmiliki wa UDA kwa 100%. alinunua baadhi ya mabasi na kuungana na wengine kuwa mbia Mkuu wa DART.
P
 
Binafsi ningependa kuona serikali inabaki kuwa msimamizi na mdhibiti...

Uendeshaji ufanywe na watu binafsi, tena ikiwezekana routes tofauti ziwe na makampuni tofauti kuweka ushindani...
Magufuli simuungi mkono kwenye baadhi ya mambo ila sehemu nyingi tuko pamoja...

Usafiri wa umma inabidi uendeshwe na serikali maana ni sehemu ya Huduma za serikali.
 
sijui kwanini watu wanashabikia umiliki wa serikali? Serikali haina historia ya kufanya biashara kwa ufanisi.. Mtakuja kushuhudia siku moja
Kwa nchi hii isingekuwa hujuma tunazofanya wenyewe, serikali ndiyo the best. Tatizo la huduma za serikali waliokabidhiwa wanatafuta maslahi yao binafsi kwa hujumu.

Kampuni gani ya usafiri ya binafsi imefanya vizuri nchi hii.

Wakipewa watu binafsi hamkawii kusikia wamepandisha nauli kila kukicha bila sababu za msingi, yote ni kutaka kuonyesha ubabe na kutafuta faida kuubwa ambazo hazina justifications zozote.

Nchi yetu hii bora serikali iendeshe, tatizo la serikali wote tunalifahamu.

Wakurugenzi wanaoteuliwa na bodizinazohusika huona kama wamepewa miradi binafsi, hivyo kuanza kuiba, kujilipa zaidi nje ya utaratibu, yaani kutengeneza mianya ya kuiba, wanasahau hata kuendeleza haya mashirika, mwisho wake yana kufa. ikiwa watasimamiwa vizuri na bodi zinazowateua kuongoza mashirika haya, na kuandaa mipango ya ku repair, kununua vipya na kuendeleza haya mashirikia tunge kuwa mbali sana.

Mkurugenzi ukimpa mradi wa usafiri dar es salaam, ukampa ma bus 10, ujue hayo hayo yatatumika, hata maintenance hakuna, na yakiharibika ndio imetoka. miundombinu haita karabatiwa, na hakutakuwa na uendelezaji wowote. Yani huyo mkurugenzi akimaliza muda wake na mali na thamani zimekwisha na hakuna kilichobaki.
Huo ndio Utanzania.
 
Back
Top Bottom