Tunaomba Serikali iingilie kati Hospitali ya Dar Group (T.O.H.S), Mmiliki hajulikani

bwashee2020

Member
Dec 8, 2020
43
59
Kwa siku za hivi karibuni, hospital ya Dar Group (T.O.H.S) imekuwa na mgogoro na wafanyakazi wake, hali inayopelekea mzoroto wa huduma za afya katika hospitali hiyo iliyopo eneo la Tazara ikiwa imetazamana na Azam TV, Mfugale flyover na kupakana na TBC.

Chanzo cha mgogoro katika hospitali hiyo ni ubabe na unyanyasaji wa mkurugenzi mkuu (D.G) wa hospitali hiyo.

Wafanyakazi wamekuwa wakiachishwa kazi kiholela kwa taarifa ya masaa 24 au kupewa shinikizo la kuandika barua ya kujiuzulu ndani ya masaa 24 nakumfanya mfanyakazi kupoteza stahiki zake ikiwemo kiinua mgongo.

Mkurugenzi mkuu amekuwa na kawaida ya kuingilia taaluma adhimu ya udaktari na kuwashinikiza madaktari kutoa tiba nje ya muongozo wa tiba wa taifa (STG) ili kujitengenezea faida zaidi kutoka katika mashirika ya bima za afya.

Aidha inaripotiwa kwamba kumtukana na kumvunjia heshima mtumishi mbele za wateja(wagonjwa) ni kitu cha kawaida kwake, na endapo utahoji basi unaweza kufukuzwa au kuhamishwa kituo cha kazi. Mifano ya wafanyakazi waliokumbana na kadhia hyo ni; daktari daraja la pili (M.D) ambaye amehamishiwa katika DISPENSARY ya shirika iliyopo Mbeya. Pia kuna daktari daraja la pili(M.D) ambaye amesimamishwa kazi kwa kipindi cha mwezi bila kosa lake kubainishwa huku madaktari na wafanyakazi wengine wengi wakiandikishwa barua.

Aidha mkurugenzi ameajiri mtu ambaye kazi yake nikukagua vyumba vya madaktari, na anaingia muda wowote bila taarifa hata kama upo na mteja, jambo linaoharibu usikivu na utoaji huduma bora kwa mteja kwani huduma za kitabibu ni siri baina ya daktari na mteja wake.

Mkurugenzi mkuu amemfukuza kazi mkurugenzi wa fedha(Director of finance) , na kwa kipindi hiki yeye ni mkurugenzi mkuu na msimamizi wa fedha kwa wakati mmoja (monopolisim).

wafanyakazi wamenyimwa fursa ya kukopa pesa kutoka katika bank ambayo mishahara yao inapitia na inasemekana sababu kubwa ya kushindwa kukopesheka ni baadhi ya wafanyakazi wa awali waliokopa kushindwa kumaliza marejesho yao kutokana na kufukuzwa kazi kabla ya kumaliza rejesho la mkopo.

Licha ya likizo ya mwaka kuwa haki ya wafanyakazi lakini wafanyakazi wengi wanayimwa likizo bila malipo yoyote ya likizo zao. mfanya kazi kufanya kazi zaidi ya miezi 18 bila likizo ni kitu cha kawaida na hakuna malipo yoyote kwa mda unaopitiliza bila likizo.
kitengo cha afya ya kinywa na meno ndicho kinaongoza kwa madaktari wake kunyanyasika ma kufukuzwa kazi ndani ya muda mfupi kutokana na mashinikizo makubwa ya kufanya kazi nje ya weledi/miiko ya kitabibu. hujuma katika kitengo hiki ni kubwa sana na daktari ili udumu lazima uuvue udaktari na uamue kuwa mbaka fani ya udaktari.

Kwa ujumla hali za wafanyakazi katika hospital ya dar group zipo matatani, hakuna mwenye uhakika na ajira yake masaa 24 yajayo labda uwe kipenzi cha mkurugenzi mkuu. Wafanyakazi wanafukuzwa na kusimamishwa kazi kiholela kwa utashi wa mkurugenzi mkuu.
sintofahamu inayoendelea hospitalini hapo imepelekea kupoteza morali na hali za wafanya kazi nakupelekea huduma zisizokidhi viwango kwa wateja.

A. DAR GROUP (T.O.H.S) NI HOSPITALI YA NANI??

I. KUANZISHWA

Ilianza kama kituo cha kutoa mafunzo kwa afya za wafanyakazi wa viwandani mnamo mwaka 1967.

Baada ya muda kupita ilionekana hitaji la kufungua hospitali ili ihudumie wafanyakazi kwa wakati na kuwawezesha kurudi kwenye majukumu yao kwa wakati. Mashirika zaidi ya mia moja(100) yalifikia muafaka wa kufungua hospital na ikawa ikiendeshwa chini ya usimamizi wa mashirika hayo. Baadhi ya mashirika ni pamoja na; ORYXY, TANITA, DABREW, KIOO, ARAF, CRDB, NATIONAL BATTERY na IFM ambayo yalitoa wajumbe wa bodi na mwenye kiti wa bodi kwa awamu.

Mnamo mwaka 1971 tar 9 Agosti, hospitali ilifunguliwa rasmi na hayati baba wa taifa Mwl Julius Kambarage Nyerere, wakati huo ikijulikana ka Kliniki wa wafanyakazi.

II. MUUNDO WA T.O.H.S(DAR GROUP) YA AWALI

Hospital ilikuwa ikiendeshwa na bodi yenye wawakilishi kutoka mashirika anzilishi. mwanyekiti wa bodi alikuwa akidumu kwa awamu na kila awamu alkuwa akitoka moja ya shirika anzilishi. Hakuwa mwenyekiti wa milele. Mkurugenzi mkuu aliteuliwa na bodi na alikuwa anawajibika kwa bodi.

III. DAR GROUP (T.O.H.S) CHINI YA DR NELSON.

Huyu alikuwa daktari mwenye asili ya India ambaye wakati wake wa Uongozi kulikuwa na manyanyaso na uvunjaji wa haki za biandamu. pia wakati wake kulikuwa na kashfa ya kuwapa wagonjwa dawa zilizoisha muda wake (expire). Serikali ya awamu ya pili chini ya rais Ally Hassan Mwinyi iliingilia kati nakuagiza daktari huyo( mkurugenzi mkuu) kuacha kazi ndani ya saa 24.

IV. DAR GROUP (T.O.H.S) CHINI YA DR LOUIS MLINGI.

Alifuata baada ya Dr Nelson. Aliongoza kama mkurugenzi mkuu kwa kufuata misingi ya utawala bora hadi mwanzoni mwa mwaka 2018.

V. KUFA KWA MASHIRIKA.

Baadhi ya mashirika yalikufa jambo liliopelekea bodi ya wakurugenzi iliyoundwa na wawakilishi kutoka katika mashirika hayo kufa na kutoa mwanya kwa watu wachache kuichukua hospitali na kuifanya kuwa hospitali binafsi ( private hospital) ambayo mmiliki wake hajulikani.

B. DAR GROUP (TOHS) MPYA.

- Ni hospitali binafsi ambayo mmiliki wake hajulikani.

- Inaundwa na bodi yenye wajumbe amabao ni wafanyakazi (waajiriwa) wa hospital ambao kimsingi hawana uwezo wa kumwajibisha Mkurugenzi Mkuu maana ni bosi wao. hivyo kwa lugha nyepesi ni " bodi hewa".

- Mwenyekiti wa bodi ni mstaafu wa kampuni ya Tanzania Oxygen ambaye anaonekana hana sauti kwa mkurugenzi mkuu kwani umri wake umeenda. mwenyekiti huyu hana hasara na manyanyaso yanayoendelea kwani yeye kila mwisho wa mwezi anapata gawio lake linalosemekana kuwa takriban shilingi milioni tatu za kitanzania.

- Haijulikani mkurugenzi mkuu anapatikanaje na anatakiwa kuwa na sifa zipi.

- Hakuna chama cha wafanyakazi.

- Gharama za matibabu kwa wateja ambao sio wanufaika wa bima za afya zipo juu sana hali inayowanyima fursa raia na walipa kodi wa kipato cha chini kupata huduma.

- Ina zaidi ya miaka 40 lakini bado imedumaa kimaendeleo licha ya kupokea wastani wa wagonjwa 400(mia nne) kwa siku.

- Ni hospitali kongwe lakini haina wodi za kutosha kulaza wagonjwa, hakuna jengo la kuhifadhia maiti, hakuna huduma ya CT-scan, hakuna kitengo cha watoto wachanga. kuna jengo la ICU lakini hakuna huduma mdhubuti za ICU. kuna jengo la huduma ya dharula lakini hakuna vifaa tiba wala dawa zakutosha kuhudumia wagonjwa wa dharula.

- Mapato ya hospitali ni makubwa lakini hospitali haiendelezi huduma zake wala majengo licha ya kuwa na eneo kubwa la takriban hekali nne. Pesa zinatumiwa na watu wachache kwa manufaa yao binafsi na kuacha hospitali ikiwa kama mtoto yatima asiye na msaada.

C. OMBI KWA SERIKALI SIKIVU YA MH Dr JOHN JOSEPH POMBE MAGUFULI YA "HAPA KAZI TU"

I. Iteue tume ya kuichunguza hospitali ya Dar group(T.O.H.S) - Kujua chimbuko lake, uhalali wake wa kuwa hospitali binafsi, umiliki wake na mapato na matumizi ya hospitali hiyo.

II. Iwakusanye waanzilishi halisi wa hospitali hiyo(mashirika anzilishi) na watengeneze bodi ya wakurugenzi yenye meno itakayo simamia mapato na uendelezwaji wa hospitali na upatikanaji wa mkurugenzi mkuu mwenye kariba na weledi wa uongozi.

III. Kwasababu hospitali imeshindwa kujisimamia na dhumuni mama la kuanzishwa... yaani kuhudumia wafanyakazi halifanyiki tena, basi serikali iiteue kuwa moja ya hospitali au taasisi chini ya wizara ya afya ili kutanua wigo wa huduma na kupunguza mzigo kwa hospitali za Temeke na Amana. Hospitali ina eneo kubwa sana ambalo likiendelezwa inaweza kutoa huduma bora kwa wakazi wa wilaya ya Temeke, Ilala na viunga vyake.

NAWASILISHA, MIMI MWANANCHI MVUJA JASHO, MLIPA KODI MWENYE MAPENZI MEMA NA NCHI YANGU MAMA AFRIKA, TANZANIA.

MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU IBARIKI AFRIKA.

1608194489552.png

Habari zaidi, soma;
 
19/6/2016 saa nane mchana nesi wa Dar Group alitokea leba akiwa amebeba kimtu kidogooo akaniangalia akaangalia na kile mtu alichokibèba akatabasamu akaniambia "happy fathers day" furaha yake haikua na kipimo.

Back to the topic mimi kama mdau wa hiyo hospitali nimeguswa na nimesikitishwa sana na huo upimbi unaoendelea hapo mjengoni hope wenye mamlaka watatenda jambo.
 
Acha majungu dogo. Usipofuata standard Treatment Guideline NHIF hawawezi kukulipa.

Halafu siyo kweli kwamba STG ina matibabu yote hiyo ni guideline ambayo baadhi ya maeneo ipo very shallow. Wewe utakuwa ni miongoni wa madaktari wazembe, mpenda majungu kwenye hiyo hospital.
 
Kumbe hospital zisizo na wamiliki ni nzuri aisee. Mimi naifahamu hiyo hospitali, ina huduma nzuri kuliko Amana na Temeke. Nadhani maboresho ni waiwekee bodi yenye nguvu ila wasiichukue serikali maana itaharibika. Imeweza kujiendesha kwa 100% big up mkurugenzi. Ijapo mpigaji ila umehakikisha huduma zinapatikana pia. Hilo ndiyo la msingi, kulingana na maelezo yao inaoneka pia huyu DG ameweka usimamizi madhubuti ikiwa ni pamoja na kuajiri mtu wa surprise monitoring/visit kwa vyumba vya madaktari ili kuzuia uzembe na upigaji (wa watumishi (wenyewe manaitaga CCD)manes na madaktari).

Nadhani Huyo DG angekuwa siyo strick, ingeshakufa zamani hiyo hospitali
 
Mmmh Kuna mengi ya ukweli, nikiwa mteja mzuri hapo hospital kiukweli morali ya wahudumu hasa manesi umeisha sababu wanapunguzwa kazini, nilipiga story na baadhi yao ni kuwa wale wazoefu mkataba ukiisha na chako ndo kimeisha na hakuna ku-renew na hata mafao yao kuandikiwa umekuwa mtihani, kwa sasa Kuna upungufu wa wahudumu na wachache walioajiriwa bado hawajawa na uzoefu. So waliobakiza muda mfupi wanaenda kutimiza tu wajibu Ila hawana morali ndicho nilichoona.
 
Back
Top Bottom