Sasa rasmi UDART 85% ni hisa za Serikali. Simon Group hoi

Wamechukua Yard zote ile ya Mbagala itakuwa stand kuu ya mwendokasi.
Mabasi yote mmiliki ni serikali. Mifumo yote mmliki ni serikali
Na walianza interview mda flani wakafukuza wale wote waliokwepo kabla
 
Ndiyo maana hata magari hayaendi gereji siku hizi
Kutokana na taarifa ya wizara ya fedha.. serikali imeongeza umiliki wa shirika la.mabasi ya mwendo kasi (Udart) hadi kufikia 85%.

Kumbuka wakati wa Rais Mstaafu Kikwete Simon Group chini ya kisena, waliwahi kusema wanamiliki 100%.

Kisena akitoka gerezani itabidi akalime pamba huko Simiyu.

View attachment 1271614
 
Uendeshe na serikali chini ya watumishi vilaza wanaoshinda wakichati mitandaoni ?
Udart itakufa kibudu.

Hivi sasa hayo magari menyewe tia maji tia maji
Magufuli simuungi mkono kwenye baadhi ya mambo ila sehemu nyingi tuko pamoja...

Usafiri wa umma inabidi uendeshwe na serikali maana ni sehemu ya Huduma za serikali.
 
Uendeshe na serikali chini ya watumishi vilaza wanaoshinda wakichati mitandaoni ?
Udart itakufa kibudu.

Hivi sasa hayo magari menyewe tia maji tia maji
Serikali iongeze magari kama inavyo ongeza ngege..

Au wachina nao wanakamata magari?


Cha pili ni kufanya mpango wachina waanze ku assemble mabasi hapa hapa nchini
 
Kujenga viwanja vya ndege ???
Duh
Unajua sababu ya kukosa ufanisi ni viongozi legelege na tukisema tusubiri sekta binafsi ni kupoteza muda wakati tunaweza kufanya kupitia serikali mbona sects binafsi haikuweza kujenga viwanja vya ndege vikubwa tz wala kununua ndege za maana ? Kiongozi atakiwi kucheka na wafanyakazi wa serikali hata siku moja
 
Hii hii serikali inayoongozwa na watu wenye degree nne za kopi n pest?

Kwani mashirika ya umma yaliyoachwa na mwalimu yalikufaje?
Serikali iongeze magari kama inavyo ongeza ngege..

Au wachina nao wanakamata magari?


Cha pili ni kufanya mpango wachina waanze ku assemble mabasi hapa hapa nchini
 
Naishukuru serikali Kwa kurudisha 85% , huu usafiri ni kero sana sasa boresheni tuachane na magari madogo tuanze kuutumia kama ulaya.
 
Huyo mbia atatoa Huduma kibiashara ila sio kwa manufaa ya jamii, ukiambiwa nauli toka Kimara hadi kariakoo ni 1500 usiilalamikie serikali kwamba imewatelekeza wananchi.!
Waswahili tuna tatizo la kutunza kumbu kumbu.
Tulikuwa na daladala nauli kutoka mbezi posta,mbezi kariakoo bei 600,leo usafiri huo unapanda basi 2 bei 1050.
Kulingana na mawazo yako nauli ya 600 ni kubwa kuliko 1050?
 
Waswahili tuna tatizo la kutunza kumbu kumbu.
Tulikuwa na daladala nauli kutoka mbezi posta,mbezi kariakoo bei 600,leo usafiri huo unapanda basi 2 bei 1050.
Kulingana na mawazo yako nauli ya 600 ni kubwa kuliko 1050?
Nauli inatakiwa isizidi 500 popote ninapo kwenda.. haijalishi nimetoka wapi..hata kama nimetoka maili moja hadi posta .


Mbona nikipanda DIT na kushuka Magomeni hawapunguzi nauli.?
 
Hivi unafikiri Huduma za Maji, umeme, afya na elimu zikimilikiwa na sekta binafsi kwa asillimia mia ni Watanzania Wangapi watakaomudu hizo gharama.?
Mkuu usikariri,Monopoly kwenye huduma za jamii ndio chanzo cha huduma kuwa mbovu na bei ya juu,tujifunze hapo mwanzo wakati kuna posta na simu,kupiga simu tu ilikuwa shughuli pevu,ikaingia Tritel napo balaa katika kupiga simu baada ya kuingia makampuni mengine sasa ukiwa na buku unaweza kuongea mwezi mzima halichachi na mda wowote tu.

XWASA na TANESCO wakipata ushindani kutoka kwenye makampuni binafsi nadhani watatia akili,hivi unajua usumbufu wanaopata wateja wakitaka kuunganinishiwa maji/umeme? Nina kijieneo sehemu flani huu mwaka wa tatu umeme haujafika na ni nguzo 5 tu kufika kwangu lakini kwenye report ya wizara inaonyesha kwamba eneo letu tayari kuna umeme,ukifailia TANESCO wenyewe wanakwambia bado hawajapata fungu serikalini.

Kukiwa na competition kwenye huduma za jamii bei inashuka na kuwa affordable.
 
Huyo mbia atatoa Huduma kibiashara ila sio kwa manufaa ya jamii, ukiambiwa nauli toka Kimara hadi kariakoo ni 1500 usiilalamikie serikali kwamba imewatelekeza wananchi.!
Akiondolewa kodi kwwenye uendeshaji atatoa huduma bora kwa gharama ndogo tu
 
Shida unaangalia ulipoanguka ungeanzia ulipojikwaa! umewahi kujiuliza kwanini watu wanashangilia ndege kukamatwa
Mambo kama haya ndio yanafanya nisimame na JPM. Alafu habari kama hii comments hazitazidi 200 ila ndege ikamatwe sasa
 
Back
Top Bottom