Sasa nimeelewa hoja/shida ya wana-UKAWA

Sasa nimeelewa hoja/shida ya wana-UKAWA

Sasa Je kama muhimu ni kuondoa CCM tu, Na tuseme Lowasa akawa raisi wa JMT halafu ghafla akageuka kuwa Museveni (raisi wa Uganda) akafuta Upinzani na kuweka Udikteta kwa kufuta vyama vingi, akatumia Katiba iliyopo inayompa madaraka makubwa na kujimillikisha gesi na rasilimali zote yeye na wenzake tunawezaje kuirudisha tena nchi yetu ktk kwake?

Nasema hivi kwa maana mpaka sasa hivi hakuna chochote kinachoonyesha ni nini Lowasa anasimamia, ni ipi itikadi ya Lowasa/UKAWA hivyo ni kama kamari kuna kupata na kukosa ndivyo unavyotaka kusema?
Lakini kama ni hivyo huwezi kucheza kamari na Nchi hapa tunaongelea Nchi na siyo Kampuni au familia bali ni nchi yenye Watu milioni 45 sasa kutaka tu kubalisha Uongozi kwa kutegemea kamari kwangu mimi ni hiyo haitoshi!

Subiri ilani.
 
Baada ya kupata shida sana kwa muda sasa kuwaelewa wafuasi wa UKAWA/Lowasa mwishowe nimekuja kuwaelewa ni kwamba wao wanachokitaka Chama Cha Mapinduzi kiondoke madarakani na kinaondokaje na nani anakuja baada ya CCM kuondoka hilo kwao siyo muhimu ila cha muhimu tu CCM iondoke!

Kitu kilichokuwa kinanipa shida kuelewa ni kwamba ni kwanini maswali magumu hawataki kuyajibu? Maswali kama Je, kama CCM ndiyo mbaya iweje tena muwe tayari kuwaamini Watu wale wale waliokuwa CCM na wengine bado wapo wajibadilishe Jina nakujiita UKAWA badala ya CCM halafu mseme mnataka kuindoa CCM madarakani hamuoni kwamba mtakuwa mmefanya kazi bure?

Jibu la hili swali ni kwamba tutajua mbele kwa mbele cha muhimu CCM iondoke!

Sasa baada ya majibu kama haya basi nimeamua kuwaelewa na kutambua kwamba wana UKAWA wana Intelejensia ndogo na hamna kitu mtu utafanya kuwashawishi vinginevyo kwa maana hata hawako tayari kwa majadiliano yenye maswali mgumu!

Kwao haijalishi nani anakuja lkn Cha muhimu CCM Iondoke!

Well said brother. Binafsi kadri siku zinavyoenda ukawa/chadema inazidi kupoteza mwelekeo. Ukweli chadema ya July /Augost 2015 sio ile tuliyozeoa! Hata wafuasi na wakereketwa wake walichobakiwa Nacho ni kukumbatia viongozi wao na kumeza wanayolishwa bila kuhoji! Ukombozi wa watz hautakuja leo wala kwsho bcoz - THE BEAUTIFUL ONES ARE NOT YET BORN!!

Ni afadhali kubaki na zimwi ulijualo kuliko shetani ambae hata sura yake huwezi ku-imagine!!!
 
Yes,ccm iondoke kwanza!Win the war first and go back pick up the pieces!That's how its done!Kama na hawa wataendeleza yaleyale na wao tutapiga chini mpaka apatikane mtu sahihi,hakuna haja ya kuendelea kukumbatia chama kile kile kilichpoteza dira,tunataka mabadiliko!Chama kikiharibu kinapigwa chini

Nikama mpiga ramli tu, unajaribu chama? Kwa nini usiwe na uhakika na chama unachochagua. Haya ndio mawazo ya kina mbowe wawajaribu wana ccm labda watawasaidia. Hakuna cha mabadiliko ccm waendelee tu. Wana watu wazuri wanaoweza kuifikisha tanzania pazuri sio hao ukawa wazee wa kununuliwa.
 
CCM ipo, na itakuwepo, mwageni sera, hizo siasa za kijinga za kutaka aondoke hatuwapi nchi.

Hao hao mnatawaita mafisadi wakija kwenu mnawapokea na mnawaita Malaika.

Kwani Slaa alikuwa chama gani kabla ya huko? sasa kafanya nini zaidi ya kupiga porojo miaka yote na mmetema kwa pesa.

Watanzania hawadanganyiki.
 
CCM imenunuliwa chadema imenunuliwa
 
Baada ya kupata shida sana kwa muda sasa kuwaelewa wafuasi wa UKAWA/Lowasa mwishowe nimekuja kuwaelewa ni kwamba wao wanachokitaka Chama Cha Mapinduzi kiondoke madarakani na kinaondokaje na nani anakuja baada ya CCM kuondoka hilo kwao siyo muhimu ila cha muhimu tu CCM iondoke!

Kitu kilichokuwa kinanipa shida kuelewa ni kwamba ni kwanini maswali magumu hawataki kuyajibu? Maswali kama Je, kama CCM ndiyo mbaya iweje tena muwe tayari kuwaamini Watu wale wale waliokuwa CCM na wengine bado wapo wajibadilishe Jina nakujiita UKAWA badala ya CCM halafu mseme mnataka kuindoa CCM madarakani hamuoni kwamba mtakuwa mmefanya kazi bure?

Jibu la hili swali ni kwamba tutajua mbele kwa mbele cha muhimu CCM iondoke!

Sasa baada ya majibu kama haya basi nimeamua kuwaelewa na kutambua kwamba wana UKAWA wana Intelejensia ndogo na hamna kitu mtu utafanya kuwashawishi vinginevyo kwa maana hata hawako tayari kwa majadiliano yenye maswali mgumu!

Kwao haijalishi nani anakuja lkn Cha muhimu CCM Iondoke!

Tanzania haitabadilika kwa katiba tuliyonayo. CCM haitatupatia katiba mpya. Tunahitaji Umoja wa Katiba wa Wananchi aka UKAWA. Lengo letu ni kupata katiba mpya. CCM iondoke kwanza ili kuwe na fair play. Tukiwa wote saizi moja hamna atakayemdumaza mwenzake.
 
Cha muhimu CCM iondooooooke tuuu haijalishi inaondokaje
 
Tanzania haitabadilika kwa katiba tuliyonayo. CCM haitatupatia katiba mpya. Tunahitaji Umoja wa Katiba wa Wananchi aka UKAWA. Lengo letu ni kupata katiba mpya. CCM iondoke kwanza ili kuwe na fair play. Tukiwa wote saizi moja hamna atakayemdumaza mwenzake.

Ccm haiwezi kuondoka kwa kumteua EL kugombea uraisi!!!!
 
Kwani unazuia ccm kuondoka kwa kutumia keyboard.Hao unaowaita malofa,nyumbu nk.subiri hasira yao Oct.25. Baada ya hapo rudi kwenye keyboard na mrejesho.Usitokwe povu hapa.
 
Sijakuelewa lengo lako maana umejiuliza na kujijibu ie. umejitekenya na kucheka mwenyewe ila elewa tu kwamba ULOPO TUPO, tukutane October.
 
Ccm haiwezi kuondoka kwa kumteua EL kugombea uraisi!!!!

Itaondoka tuu; wewe unadhani nani ataweza kama sio LOWASA
Huyo ndio mwiba kwenu ndio maana mnamtaha taja saaana
Hamna makapi au matapishi hapa
Sie tunawaachia matapishi ya kadi zenu za kuchanwa tuuu
Vijijini washaamua sijui mtaibaje
 
Baada ya kupata shida sana kwa muda sasa kuwaelewa wafuasi wa UKAWA/Lowasa mwishowe nimekuja kuwaelewa ni kwamba wao wanachokitaka Chama Cha Mapinduzi kiondoke madarakani na kinaondokaje na nani anakuja baada ya CCM kuondoka hilo kwao siyo muhimu ila cha muhimu tu CCM iondoke!

Kitu kilichokuwa kinanipa shida kuelewa ni kwamba ni kwanini maswali magumu hawataki kuyajibu? Maswali kama Je, kama CCM ndiyo mbaya iweje tena muwe tayari kuwaamini Watu wale wale waliokuwa CCM na wengine bado wapo wajibadilishe Jina nakujiita UKAWA badala ya CCM halafu mseme mnataka kuindoa CCM madarakani hamuoni kwamba mtakuwa mmefanya kazi bure?

Jibu la hili swali ni kwamba tutajua mbele kwa mbele cha muhimu CCM iondoke!

Sasa baada ya majibu kama haya basi nimeamua kuwaelewa na kutambua kwamba wana UKAWA wana Intelejensia ndogo na hamna kitu mtu utafanya kuwashawishi vinginevyo kwa maana hata hawako tayari kwa majadiliano yenye maswali mgumu!

Kwao haijalishi nani anakuja lkn Cha muhimu CCM Iondoke!

Peleka ujinga huko Huna adabu gamba ww
 
Kwa hiyo ni nini kinafwata hilo siyo muhimu? ila cha muhimu tu (kwa mujibu wa Lowasa/UKAWA) CCM iondoke kama nimekuelewa vizuri ndivyo ulivyomaanisha?
Kwa kawaida huwa sipotezi muda kujibu upuuzi lakini kwa leo naomba nivunje mwiko wangu huo kwa kukupa somo dogo tu. Sababu ya uchaguzi ni kupata uongozi bora kuliko uliopita. Kwa bahati mbaya Watanzania huo ustaarabu wa kuondoa utawala ulioshindwa na kuweka utawala mpya bado hatuna sana. Sababu kubwa ni kwamba tunaogopa mabadiliko na tupo tayari kuendelea na utawala mbovu hata kama unalipeleka taifa kaburini.

Tungekuwa tumezoea kubadilishana uongozi kwamba ukichaguliwa halafu ukaboronga unawekwa benchi na watu wengine wanachukua nafasi yenu. Hata hao wapya watakaoingia kama hawakutimiza malengo waliyotuahidi katika uchaguzi unaofuata wanawekwa benchi. Ni hali kama hii peke yake ndiyo inaweza kuleta uwajibikaji katika kusukuma maendeleo, kama hukuwajibika, wananchi watakuwajibisha kwa kukunyima kura...if you dont deliver, you are out.

Hapa Tanzania tumekuwa na timu ile ile mpaka umefikia wakati wanaamini tu ni wao wanayo hatimiliki ya uongozi na watatumia kila mbinu kubaki madarakani hata pale wananchi wamewachoka. Kwa sababu wanaelewa hawatoki madarakani, hawajitumi kama ilivyotakiwa wakiwaaminisha wananchi kwamba bila wao amani itavurugika, kwamba wao ndio wanao uwezo wa kulinda amani. Watatumia vyombo vya dola kulazimisha washinde uchaguzi na mwananchi anakuwa amenyimwa haki yake ya kumchagua kwa uhuru wanayemtaka.

Duniani kote kulikozoeleka kupokezana madaraka kwa njia hii, hofu ya kuingia kwenye machafuko hutoweka na uchaguzi hauwi tena na sintofahamu kama hapa Tanzania. Baada ya miaka hamsini na ushee ni lazima tukubali kwamba tunakoelekea siko na njia iko moja tu, kugeuza njia. Bila CCM kupumzishwa na wao wakae pembeni wakishuhudia wenzao kazini, hali ya ushindani katika misingi imara ya mabadilkiko haitabadilika na siku zote tutaendelea kuwa kichwa cha mwenda wazimu. Atakayeingia baada ya CCM naye kama hakutimiza matakwa ya wananchi, na yeye out.
 
Nikama mpiga ramli tu, unajaribu chama? Kwa nini usiwe na uhakika na chama unachochagua. Haya ndio mawazo ya kina mbowe wawajaribu wana ccm labda watawasaidia. Hakuna cha mabadiliko ccm waendelee tu. Wana watu wazuri wanaoweza kuifikisha tanzania pazuri sio hao ukawa wazee wa kununuliwa.

Hao watu wazuri wanao toka lini?wametufikisha wapi?Unaweza ukasema una uhakika na ccm?Umedanganywa Mara ngapi?Je,unadhani walichokifanya kinafika hata robo ya kile ambacho wangeweza kukifanya kama walikuwa na dhamira ya kweli?Kama wewe si mnufaika wa moja kwa moja basi ni mjinga,na ndio mtaji wa hiki chama!Miaka 50 kimeprove failure bado tuwakumbatie,wa nini?Hebu angalia utajiri wa ndugu na maswahiba zao ukoje,angalia rasilimali zinavyochotwa bila kuleta tija yoyote kwa wananchi,ona wanyama wanavyoisha,angalia ufisadi ulivyokithiri!Unahitaji kuwa mjinga kukielewa hiki chama,period!
 
hao watu wazuri wanao toka lini?wametufikisha wapi?unaweza ukasema una uhakika na ccm?umedanganywa mara ngapi?je,unadhani walichokifanya kinafika hata robo ya kile ambacho wangeweza kukifanya kama walikuwa na dhamira ya kweli?kama wewe si mnufaika wa moja kwa moja basi ni mjinga,na ndio mtaji wa hiki chama!miaka 50 kimeprove failure bado tuwakumbatie,wa nini?hebu angalia utajiri wa ndugu na maswahiba zao ukoje,angalia rasilimali zinavyochotwa bila kuleta tija yoyote kwa wananchi,ona wanyama wanavyoisha,angalia ufisadi ulivyokithiri!unahitaji kuwa mjinga kukielewa hiki chama,period!

mlemavu wa akili huyo hata ukimuelezea sana haelew!!!!!!!sisi twende mbele kwa mbele lowasa lowasa ukawa daima
 
Akili zako zimeishia hapo subiri uone time will tell mabadiliko ni sasa.

Kwa nini haya mabadiliko yanatafutwa na wana kaskazini tu! Lowasa, Mbowe, Mbatia na top management yote ni toka huko. Maalimu Sefu yupo kama ngazi tu. Au watu wa moshi na arusha ndo watu pekee wenye uchungu na nchi hii?!!
 
ubaguz tu ndo unachokiwaza hiyo ni dalili mbaya ya kufeli kimawazo na kifikra ukishafikia hatua hiyo utaish kwa mateso sna na utapoteza sifa za kuwa mtanzania hatujalelewa ktk misingi hiyo na watanguliz wa taifa hili..... je unataka viongoz watoke wap? au kuna sehemu ni maaluumu kwa kutawala taifa hili? tanzania ni nchi moja makabila na ubaguz peleka rwanda ,burund na kenya hapa big noooo.
 
Huenda tukawa sawa kuhusu chaguo ila kama anamchango kwenye kuuondoa mfumo uliopo madarakani ntaungana na juhudi zake.

Mfumo uliopo uko vipi hebu tujadili. Na je umeletwa na chama au watu walioko katika kikundi fulani?
Hebu twende sawa ..
 
Back
Top Bottom