Sasa Je kama muhimu ni kuondoa CCM tu, Na tuseme Lowasa akawa raisi wa JMT halafu ghafla akageuka kuwa Museveni (raisi wa Uganda) akafuta Upinzani na kuweka Udikteta kwa kufuta vyama vingi, akatumia Katiba iliyopo inayompa madaraka makubwa na kujimillikisha gesi na rasilimali zote yeye na wenzake tunawezaje kuirudisha tena nchi yetu ktk kwake?
Nasema hivi kwa maana mpaka sasa hivi hakuna chochote kinachoonyesha ni nini Lowasa anasimamia, ni ipi itikadi ya Lowasa/UKAWA hivyo ni kama kamari kuna kupata na kukosa ndivyo unavyotaka kusema?
Lakini kama ni hivyo huwezi kucheza kamari na Nchi hapa tunaongelea Nchi na siyo Kampuni au familia bali ni nchi yenye Watu milioni 45 sasa kutaka tu kubalisha Uongozi kwa kutegemea kamari kwangu mimi ni hiyo haitoshi!