Sasa Nimeamini JF ni kila kitu, hatimae am in a relationship!!!

Sasa Nimeamini JF ni kila kitu, hatimae am in a relationship!!!

Hongereni sana grand-mal na mwenzi wako.. Mungu awabariki sana.
nimechoka na hongera zako wewe toka 2010 hujapata tu humu dalaliiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii utuwekee thread nakuni mention khaaaaa ntaanza mkakati wakukutafutia hakianani huwezi kaa ubachela mpaka miaka 35 !!!!!!lol
 
All the best mkuu
na wewe uuage ubachela mpaka usutwe tafuta tafuta humu tukacheze kwaito maana kanga moko na zile ngoma nyingine marufuki toka 2008 hujapata kimwana humu khaaaaaaaaaaaaaa
 
Kumbe yote yawezekana kwani hamkusikia zile harusi za kwenye tv?mnaoana hata kama hamjuani teh teh teh, hongera
 
Habari wana MMU,

Naomba nichukue fursa hii kuwashukuru kwa ushirikiano mkubwa mlionipa ikiwa, ni pamoja na ushauri na uungwaji mkono mkubwa uliofanywa na wote walioniandikia private messages katika huu uzi https://www.jamiiforums.com/love-connect/405796-a-serious-woman-to-join-in-marriage.html. Ulikuwa ni mtihani mzito kwangu, kwani ni kazi sana kuanzisha mahusiano na mtu ambaye hamjawahi kuonana wala hamjuani lakini imewezekana.

Nimekuwa kwenye mchakato kwa muda mrefu, nimeongea na wengi, nimeonana na baadhi. Wengi wanafaa kuwa wake lakini nilikuwa nahitaji mmoja tu. Nashukuru kwamba mmoja huyo nimempata, japo tuko bado katika kipindi cha matazamio. Tumeongea tumeelewana na tunadhani 'we are compatible' , naendelea kuomba ili malengo yetu yatimie. Tumekubaliana kwamba tunaweza kuishi pamoja lakini tuwe kwenye uhusiano wa kawaida wa sasa, nasisitiza uhusiano wa kawaida. Yeye ni member humu, na tunategemea wakati muafaka ukifika tutaweka mambo hadharani, na najua itakuwa surprise kwa wengi, lakini jamani inawezekana.

Tumepanga tukijaaliwa ndoa ifungwe jamiiforums kuonyesha shukrani zetu. Siku hiyo tunataka mkuu Invisible awe visible, mkuu Paw hatutapenda kuona pingu zako siku hiyo, kwani itakuwa full shangwe na watu wataruhusiwa 'ku-misbehave' bila kupewa ban.

Nitaomba dada yangu lara 1 awe mbali na mchumba wangu mtarajiwa asije akaanza kumpa ushauri wa kuingia nusunusu, yale mambo yake ya mguu ndani mguu nje hapana, hatuyataki. Sisi tuko serious na tunategemea kupendana kwa dhati kama tulivyoanza.

Mkuu Mtambuzi na Nicas Mtei ninawashukuru sana kwani nyuzi zenu zilinifariji sana na kunifanya nisikate tamaa.

Kaunga michango yako imetuunganisha. Nawshukuru wote humu hata ambao sijawataja.

Siku hiyo natamani iwe kesho kwani itakuwa furaha sana, Smile na wote wengine itakuwa ni smile tu.

Nasema tena nashukuru sana na tuombeane heri ili mambo yetu yaende kama tulivyopanga. Inawezekana kupata mwenza popote. Mungu anaweza kutumia njia yoyote kukupa mwenza kama ukimuomba.

Kwa uzi huu pia naomba niseme imetosha, no more private messages.

Nina furaha sasa jamani.

Its me grand-mal.

Congrats na karibu kwenye chama cha waliooa
 
Hongera sana,haya ndo matunda ya mtu kuwa serious na kile unachonuia.nakutakieni kila la kheri kwenye safari yenu
 
hongera sana Grand mal na bidada kwa kuji-find; l hope yours gonna be JF real love of the year.
na asante sana kwa feedback, inasaidia wengine ambao wanafikiri kukutana mtandaaoni ni ufake fake tu.

Changamoto mliyo nayo ni kuaminiana na kuhakikisha wale waliokuwa kwenye mchujo wanabaki huko.
 
Last edited by a moderator:

Similar Discussions

Back
Top Bottom